Namna ya kuhalalisha gari ulilouziwa limeingizwa nchini kimakosa

Namna ya kuhalalisha gari ulilouziwa limeingizwa nchini kimakosa

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
JF ndio kisima cha majibu, ndio Tanzania, ndio dunia. Hapajawahi kuniangusha humu.

Naomba mwaka huu wadau wenye masihara wafanye kubadilika. Kipindi cha kazi na umakini.

Niulize hivi ukiuziwa gari ukaja kugundua nyaraka zake si halali na liliingizwa nchini kimakosa kama yale ya namba pacha.

TRA wanatoa mwanya gani ulihalalishe. Habari ya kumpata muuzaji fanya hakuna namna tena.
 
Utashtakiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji gari
 
Jf ndo kisima cha majibu, ndo Tanzania, ndo dunia. Hapajawai kuniangusha humu. Naomba mwaka huu wadau wenye masihara wafanye kubadilika. Kipindi cha kazi na umakin. Niulize hivi ukiuziwa gari ukaja kugundua nyaraka zake si halali na liliingizwa nchin kimakosa kama yale ya no pacha. TRA wanatoa mwanya gani ulihalalishe. Habar ya kumpata muuzaji fanya hakuna namna tena.
Kidogo swali lako linachekesha kwa sababu unauliza namna ya kuhalali kitu kilichopatika kwa njia haramu kuwa halali! Jibu ni kuwa unatakiwa kuhakikisha kila kitu unachonunua kuwa ni halali na kina nyaraka zote. Hakuna short cut.
 
Ndo kusema hilo gari unalitupa au?
 
Kama sijaelewa hapa mwishoni
Iko hivi. Umenunua gari kwa mtu. Umetumia. Baadae ukagundua gari ulouziwa nyaraka zake si halali ni duplicate za gari ingine kama hiyo. Una gari si la wizi ila liliingia nchin njia za panya ukapigishwa. Na aliyekuuzia unagundua huwezi mpata tena. Bila hata kuhitaji kuhangaishana na serkali kusubir mkamatane unaweza kuilipiaje iwe halali? Au unaitupa?
 
Jf ndo kisima cha majibu, ndo Tanzania, ndo dunia. Hapajawai kuniangusha humu. Naomba mwaka huu wadau wenye masihara wafanye kubadilika. Kipindi cha kazi na umakin. Niulize hivi ukiuziwa gari ukaja kugundua nyaraka zake si halali na liliingizwa nchin kimakosa kama yale ya no pacha. TRA wanatoa mwanya gani ulihalalishe. Habar ya kumpata muuzaji fanya hakuna namna tena.
Gari la namna hiyo inamaana halipo kwenye taarifa za TRA. Kwahiyo ulilipata kwa njia isiyohalali na linaweza kuwa gari chafu likahusishwa na uhalifu. Makosa yake ni kukwepa kodi, kutakatisha gari (pesa), kuhusika katika genge la uhalifu. Adhabu yake ni uhujumu uchumi hakuna dhamana. Chakufanya kalitolee maelezo kituo cha polisi, hayo maelezo yatakupa uhalali wa kwenda TRA ili wakukadilie kodi ambayo utatakiwa kulipa.

Njia ya pili ni ya kanjanja na wengi tunaitumia. Zunguka au ongea na mafundi gereji na wanaokata bodi za magari kwa ajili ya spare tafuta gari lenye bodi zinazofanana alafu ulizia nyaraka zake alafu ziapdate kama rangi piga. Engine hakuna mtu wa eti mpaka achungulie namba!
 
Ukisikia utakatishaji magari ndiyo huo sasa,

Ukibainika kinachofuata ni gari kutaifishwa, unalipishwa faini, jela unaenda na huko jela unaweza ukafanyishwa kazi ngumu pia.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom