Namna ya kui trick express vpn ili upate kuitumia bila kulipia

Kwani kujua ki-inglish au kutojua kumeingiliana vipi. Nimeuliza wenye uwelewa kwan mwanzo sikujua kama kuna google?? We ulipaswa ukae kimya mkuu kama hukuwa na nia ya kunielewesha.
Kwa hiyo kukwambia uende google nimefanya kosa, au kuongelea Kiingereza (kitu ambacho ni kweli kwamba maelezo yapo kwa lugha hiyo)? Basi samahani. Subiri watakuja kukuelewesha...
 
Samahani wadau habari za muda huu?

Naomba mwenye uwelewa wa hii kitu inayoitwa VPN!

Hii kitu unakuwa unatumia internet free au ni nini?? Sielewi naskiaga tu vpn vpn.
Sio internet free ila ukitumia VPN wanaintelijensia wakijaribu kupata location yako hawawezi. Pia kwenye nchi ambazo internet au whatsapp, Facebook zimekuwa blocked, watu hutumia VPN ili kuipata hii mitandao bila wasiwasi na bila ya serikali kujua wala kuwatambua.
 
Ahsante sana mkuu.
 
VPN - Virtual Private Network.

Ni teknolojia inayotumika kuunganisha mitandao iliyopo mbali kana kwamba ipo sehemu moja.Mfano:Ukiwa na ofisi Dar na tawi lingine likiwa Mwanza, kwa kutumia VPN unaweza kuziunganisha(kimtandao) ofisi zako zikawa kana kwamba zipo sehemu moja i.e ukaprint document ukiwa ofisi ya Dar(Computer yako ikiwa Dar) na karatasi ikatoka kwenye printer iliyopo ofisi za Mwanza n.k.Bila VPN hili haliwezi kufanyika(labda ujilipue na public IPs ...).

Teknolojia hii ya VPN ina matumizi mengine mengi ila inafanya kazi hivyo hivyo.Kama mkuu alivyogusia hapo juu, unaweza ukazichukulia hii mikoa miwili(ofisi mbili, Dar na Mwanza) kama nchi.Mfano ikitokea kuna website au app iliyofungiwa hapa nchini, kinachozuiwa mara nyingi ni utambulisho wa hiyo website (i.e IP address).Hizi IP address huwa zinasajiliwa/kusambazwa kwa nchi, kila nchi ina range yake.Hivyo kama website imefungiwa hapa nchini, inabidi utafute VPN yenye uraia/utambulisho wa nchi nyingine ili uweze kuifungua hiyo website i.e unaifungua hiyo website kana kwamba upo nchi nyingine kumbe upo TZ.
 
mkuu free vpn nzuri ni ipi?
 
Samahani wadau habari za muda huu?

Naomba mwenye uwelewa wa hii kitu inayoitwa VPN!

Hii kitu unakuwa unatumia internet free au ni nini?? Sielewi naskiaga tu vpn vpn.
Acha uvivu Cortana yupo Google ipo kawaulize[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Shukrani sana bro 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…