SoC01 Namna ya kujiajiri kupitia udhamini

SoC01 Namna ya kujiajiri kupitia udhamini

Stories of Change - 2021 Competition

BAAJUN POET

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
6
Reaction score
11
Je, huna mtaji na ungependa kujiajiri?
Je, una wazo zuri la mradi au biashara lakini hujui uanzie wapi sababu ya kipato? Leo nitakufungulia njia kidogo na kukupa mwangaza!


Leo hii ningependa kuwajuza njia bora ya kujiajiri (kwa vijana wasio na ajira), na kupanua biashara (kwa wale wenye biashara) ambao kwao mitaji imekuwa tatizo kupitia Maombi ya Udhamini.
Kutokana na tatizo kubwa la Ukosefu wa ajira nilipendelea kujua namna ambavyo naweza kupata taarifa muhimu zitakazoweza kuwasaidia vijana wenzangu ambao pengine wao kuna mahali hawajafika kama wengine walipofika. Na hiyo ndio ikawa sababu ya mimi kuwaandalia makala hii vijana wenzangu ili mnufaike.

Aidha, kwa unyenyekevu mkubwa ninakuomba ndugu yangu msomaji, mara baada ya kusoma na kunufaika na makala hii, unipe VOTE yako kwani kura yako moja ni muhimu sana.
***
Yafuatayo ni baadhi niliyoyapata katika tafiti zangu ndogo ninazozifanya kupitia uzoefu wangu wa kazi au shughuli ambazo nimekuwa nikijishughulisha nazo hasa kwa upande wa hizi Agencies za mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa vijana (UN Agencies), pamoja na makampuni binafsi na taasisi mbalimbali (NGO's).

Kiukweli kuna fursa nyingi na kama zikitumika vizuri basi vijana wanaweza kujiajiri (hasa wakiwa ni kikundi). Ila nimegundua ya kuwa taarifa kuhusu fursa hizo ndio kimekuwa kikwazo. Kwani huishia juu kwa juu.
Kabla ya kuwaambia nilowaandalia ningependa niwajuze kitu kimoja kwanza,
"Mtaji ni mawazo ya kiubunifu sio pesa. Pesa ni kitendea kazi".
Kwani unaweza ukawa na pesa lakini usiweze kujua kipi sahihi cha kufanya.
Na kuna watu wana mawazo mazuri ya kibunifu pesa hawana lakini kupitia udhamini wametoboa!

Kikubwa ni kuacha mapuuza na mazoea. Kuwa pengine hizi fursa za udhamini ni za watu fulani. Hapana!
Kikubwa ni kufuata maelekezo kwani wengi wetu hatudhaminiwi kutokana na kukosa maarifa ya mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuomba udhamini.

SASA TUZIJUE HATUA MUHIMU ZA KUOMBA UDHAMINI:

1/ Andaa mswada (Proposal) kuelezea wazo la mradi/biashara yako:

Hii itakusaidia uonekane upo serious na uwe Qualified kwa kile unachotaka kukifanya. Mswada huo utatumika katika kuwa approach Donors pamoja na Agencies mbalimbali ikiwemo NGOs na FUNDS GRANTS ambazo hutoa misaada kwa mawazo mbalimbali ya kiubunifu kwa miradi ya vijana.
Mswada ni mkusanyiko wa maelezo yako juu ya wazo la mradi wako. Ni vizuri mradi huo ukawa na faida pia kwa jamii. Hasa katika kutatua changamoto fulani katika jamii.
Iwapo hujui kuandaa mswada ni vema kufuatilia katika mitandao kama google ili ujue namna bora ya kuandika mswada (proposal).
Pia unaweza kuangalia kupitia link hii:

Business Writing Courses Online or Onsite | Instructional Solutions › ... How to Write a Winning Business Proposal [Updated 2021]

Na kwa sampo za miswada tazama hapa:
Free Microsoft Word Templates and Services | Hloom › more › pr...
Web results 32 Sample Proposal Templates in Microsoft Word | Hloom
.
.
.
2/ Hakikisha umetafuta na kujiridhisha na Shughuli za uyo donor yaani hiyo taasisi au Agency, malengo yake na vipaumbele vyake katika kutoa misaada hiyo (grants) kabla ya kuandaa na kutuma mswada wako. Hakikisha wazo lako linatokana na vipaumbele vyake.

Kwa mfano: kama anahusika na masuala ya uwezeshaji mabinti, basi hakikisha mradi wako utagusa kuleta maendeleo kwa mabinti.
Mfano, Jina la mradi: "Uundaji wa Karakana ndogo ya utengenezaji wa Taulo za mabinti" N.k.

Au kama anahusika na masuala ya mazingira basi hakikisha mradi wako utagusa kuleta maendeleo katika mazingira. Mfano, Jina la mradi: "Uundaji wa Karakana ndogo ya utengenezaji mkaa wa taka laini" N.k.


N.B.
Gharama na maelezo yote yanayohusu mradi wako utayataja katika mswada.


Kwa taarifa kuhusu GRANTS, makampuni na misaada inayotolewa kusapoti miradi ya vijana tembelea google au kupitia link hii:

fundsforNGOs – Grants and Resources for Sustainability › tag
Web results Latest Grants for NGOs and individuals in Africa fundsforNGOs
.
.
.
3/ Jambo la tatu la muhimu ni kuandaa Appointment Letter pamoja na Cover Letter:
Hizi ni barua mbili ambazo inabidi uziandae, Cover Letter ni kwaajili ya kuomba udhamini, na utaelezea pia kidogo kuhusu mradi wako na faida zake kwa jamii. Na Appointment letter ni kwaajili ya kuomba siku ya kukutana na mkurugenzi au msimamizi mwandamizi wa taasisi husika.
Pitia google kufahamu zaidi na kupata sampo ya barua hizo.


4/ Hatua inayofuata ni kutuma mswada wako pamoja na barua hizo na mswada wako kwa Donor wako yaani taasisi husika. Vizuri zaidi utume barua yako kwa kuifikisha mwenyewe Ofisini, pamoja na email address (kama unayo).


N.B
Jua kuwa nadhifu siku unayopeleka barua na muswada wako ofisini, na siku utakayoitwa kwa Appointment.


5/ Subiri matokeo. Na penda kujaribu sehemu nyingi zaidi. Usijaribu sehemu moja pekee. Hakika utafanikiwa!

Shukrani sana. VOTE hapo chini kuonesha upendo.
images (2).jpeg


Imeandaliwa na
OMARY BAAJUN,
Toka CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA (TPSC),
+255684956676
DAR ES SALAAM, TANZANIA

MWISHO.
 
Upvote 4
Mods wazito sn kufanya updates, sisi tunaitumia app HAKUNA hyo option ya ku vote. Au mi ndo siha update?
 
Back
Top Bottom