SoC02 Namna ya kujikwamua kiuchumi kwa mtaji wa milioni 5

SoC02 Namna ya kujikwamua kiuchumi kwa mtaji wa milioni 5

Stories of Change - 2022 Competition

swedi muzungu

Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
5
Reaction score
4
UTANGULIZI
kwa mtaji wa milioni 5 unaweza kujikwa mua kichumi kwa kuanzisha mradi wa uuzaji wa vipuri na virainishi vya pikiki almaarufu bodaboda kwa maeneo ya pembezoni mwa miji(mji)

Tumependelea kutumia maeneo ya pepembezoni mwa mji kwa kuwa ndio sehemu zenye huduma nyingi za pikipiki au boda boda kwa kuwa ni usafiri unaeza kuwafikisha watu kayika maeno ambayo vyombo vingine vya usafiri haviwezi kufika.Pia kutokana na changamoto za kiutendaji kwa baadhi ya miji ni ngumu au kuna sheria ndogo zinazozuiwa vyombo hivi vya usafri (boda boda) kufika katikati ya miji.

kwa kuwa mradi wetu utakuwa pembezoi mwa mji hivyo ni rahisi kupata eneo kwa ajili ya kuweka karakana ndogo kwa ajili ya kuuzihudumia hizo pikipiki.

KIINI
kutoka na umuhimu wa usafiri huu pia hata vitendea kazi vyake vinahitajika kufanyiwa huduma za kimatengenezo pindi zinapopata hitilafu. unaweza kuanzisha duka lako la kuuza vipuri na vilainishi vya pikipiki kwa mtaji wa milioni tano kwa kuanzia na kukua kadri mzunguko wa biashara unavyokwenda.

Ili biashara iwe na mzunguko mkubwa/mzuri itakubidi uwe na sehemu amabayo unaweza kuwa na karakana dogo na kuwaalika mafundi wazuri/wenye uwezo wa kuzihudumia hizo pikipiki kwa maana hao ndio watakusaidi kukutangaz na kukuletea waje wengi zaidi . Kwa kawaida mafundi watajilipa wenyewe pindi wanaziuhudumia hizo pikipiki bila kuathiri kitu chochote kwenye biashara yako kwa kuwa pesa ya ufundi na vipuri italipwa tofauti tofauti( vipuri dukani na ufundi kwa fundi)

MCHANGANUO WA MILIONI 5
kodi ya jengo(nje ya mji kama vile mbagala,chanika,gongo lamboto.. n.k) 80,000/= kwa mwezi utalipa kwa muda wa miezi sita , leseni ya biashara utalipa mara moja kwa mwaka laki moja ,malipo ya kodi TRA utalipa mara nne kwa mwaka ambalo kwa mtaji wa milioni 5 unaweza kulipa TRA kila baada ya miezi mitatu shilingi laki moja na ishirini 12,000/=.(Mcanganuo wa kiasi cha kulipa TRA kinategemea na namna wakavyokukadiri namna ya ulipaji kwa mwaka na utakata maranne kwa vipindi vya miezi mitatu mitatu)

Utanunua viburi ya pikipiki aina ya boxer 150 BM kwa 1,490,000/=amabapo utapata vupuli jumla 106 vya aina tofauti tofauti vya muundo huu wa pikipiki, GN 125 kwa 1,193,000/= ambapo utapata vipuri tofauti tofauti jumla 100 kwa idadi tofauti tofauti

TVS 125 kwa 370,000/= utaanzia na vipuri aina tofauti tofauti 31 vya kuanzia.

Vilainishi kwa 1,076,800./= utapata aina 14 pamoja na bidhaa zingine 13 kama vifungashio(bolts and nuts) pamoja na gundi mbali mbali zinzotumika kwenye huduma ya pikipiki pamoja na vihakisi mwanga
matumizi mengine utamlipa mtu amabaye utamuweka hapo (utakaa mwenyewe) kwa siku shilingi 5000/= kwa hiyo matumizi ya mwezi ni shilingi 150,000 umeme na matumizi mengine elfu 30,000/= kwa mwezi.

Kama kuna ulinzi ni bora kushirikisha serikari ya mtaa kwa kuwa maeeneo mengi ususani jijini dar es salaam wanatumia ulinzi shirikishi kwa kuwalipa kwa mwezi kiasi cha juu shilingi elfu tano.

FAIDA NA HASARA
FAIDA

kwa siku ukiweza kuuza na kupata mauzo ya chini ya shilingi elfu 50,000/= kwa mwezi ni shiling 1,500,000/ uliota pesa uhendeshaji shilingi 1,080,000/= utabaki na faida ya shingi 420,000/= ambayo faida hii itakusaidia kukua kiuchumi(muda mwingine inaweza kukua zaidi ya hiyo au kupungua kidogo).

kwa kuwa kiwango ch achini kwa siku cha mauzo utakiweka kisiwe chini ya elfu 50,000/= zipo siku kinaweza kuzidi zaidi ya hapo na pengine kupungua (zitajisawashiza zenyewe katika kupanda na kushuka)

Mfumo wa vipuri na vilainishi huwa vitu vyake vingi havina muda ma mwisho matumizi au muda mrefu sana mpaka kufika muda kuharibika inapelekea kutokuwepo kwa changamoto ya bidhaa kukaa mud a mrefu na kukosa au kupungua ubora wake hii inapeleke bidhaa kuwa kwenye soko hata kwa muda mrefu sna.

Upatikanaji wa bidhaa hizi ni rahisi katika soko hivyo ni vigumu kukosa kipulu pindiunapokwenda kujumua jumla sokoni

HASARA
Biashara utapata hasara ikiwa utakuwa na mafundi ambao sio waaminifu katika utendaji wao wa kazi.Hii itapelekea badhi ya wateja kuhama kwako na kwenda kungine.

Pia hepuka kuwabambikia vipuri visivyo na ubora wateja wako kunaweza kusababisha hasara kubwa ya kukimbiwa na wateja.

MADENI/MIKOPO
Changamoto kubwa ya biashara hii madereva wengi kukopa na kuchelewa kulipa au kuto lipa kabisa na kuacha kuja dukani.

Hakuna biashara yeyote isiyo na changamoto hii hivyo hauna budi kuikabili kwa kuweka muundo mzuri wa kiutendaji katika kujiendesha. moja ya njia unaweza kutumia ili kutatua changamoto hii ni kama ifuatvyo
  • Kuhakikisha kila mwenye kukopa ni mteja hai katika duka lako
  • Kuweka kitu cha thamani kama dhamana inapobidi
  • kuandaa utaratibu wa mtu kulipa kidogo kidogo ikiwa atahitaji kipuli cha pesa nyingi na wakai huo uwezo wa kulipa kwa pamoja hana
  • kuwa na kitabu cha kumbukumbu za wadaiwa /wanaotaka kukopa mamoja na anuani zao
  • sio lazima kuwa na hichi kipengele cha kukopeshana ingawa kitawasaidia baadhi ya wateja wako hai
CHANGAMOTO ZA WIZI WA KIMAZINGARA/CHUMA ULETE
kuna hadithi nyingi katika biashara ikihusishw na wizi wa kimazingara au chuma ulete kwenye biashara. Si hakika kuwa kitu hiki kipo duniani maana kinausiswa zaidi na imani za kishirikina.

Cha kuzingatia ni kuweka mkazo kati utunzaji wa kumbukumbu zote za mapato na matumizi kwa kila siku, mwisho wa juma,na mwisho wa mwezi utaona mtililiko wote wa biashara yako( Ikiwa pamoja na kufanya sensa mara kwa mara kwa bidhaa zilizopo dukani kwako)

VITU VYA KUFANYA DUKANI KWAKO
  • Fungua duka lako mapema kdri inavyoweza ili kuweza kupta wateja wote
  • Hakikisha mafundi wapo muda wote
  • Kauli nzuri kwa wateja(lugha ya ushawishi)
  • Jitahidi karibu vipuri vyote na vilainishi vinavyohitajika mara kwa mra kuwepo dukani(epuka kuuza hakuna)
  • Tengeneza mazingira ya uhaminifu katika duka lako itasaidia wateja kuja bila kuwa na mashaka yeyote ile
VITU VYA KUACHA KATIKA DUKA LAKO
  • Kugeuza ndio kituo cha kupiga soga.
  • Mafundi wasio na weledi wa kazi zao kutowaruhusu kija kwenye karakana yako(hii utaijua maaba ya kupokea maoni kutoka kwa wateja)
MWISHO
Uwekaji wa bidhaa bora dukani kwako ndio chachu ya maendeleo ya biashara yako.
Pia penda kuzungumza na wateja kujua kama huduma unayotoa inakizi vigezo au kitu gani uongeze maana hao ndio waraji wa bidhaa yako.

kujituma na kufanya kazi kwa bidii ndio hiwe kauli mbiu yako katika kufanisha mradi wako.

Nawasilisha
 
Upvote 8
Back
Top Bottom