Namna ya kujipatia fedha kwa bidhaa yako (mpango wa siku tatu)

Namna ya kujipatia fedha kwa bidhaa yako (mpango wa siku tatu)

MAMESHO

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
1,432
Reaction score
1,738
NAMNA YA KUANZA KUJIPATIA FEDHA KWA BIDHAA YAKO (MPANGO WA SIKU TATU).
Kutengeneza bidhaa
Mpangilio huu utakuongoza kutengeneza bidhaa ambayo mauzo yake yatakuwezesha kuingiza mapato.
Karibu uanze kutengeneza bidhaa zenye faida.
Tafuta kinywaji(au upendacho jwisi, soda n.k). Nakupeleka mkono kwa mkono ndani ya masomo ya siku tatu na kukuweka kwenye njia itakayokupatia fedha kwa bidhaa yako ndani ya siku tatu zijazo.
Sijasema miezi mitatu kuanzia sasa, wala sio miaka mitatu, ni siku (3) tatukuanzia sasa. Bidhaa yako inaweza kutengenezwa, na unaweza kuona mauzo yanakuja na hata kama huna wazo leo utalipata. Sio tu kwamba inawezekana, lakini njia hii imethibitishwa- nimewasaidia watu na wamefanikisha. Na leo nakupeleka shule kuhusu sanaa ya haraka, na utengenezaji wa bidhaa bora.
Mimi ni mwalimu wa ''kuanzisha'' na hiki ndo kinaniweka mjini: Nawaleta watu kununua unachouza. Hivyo wacha nikupatie kitu kipya cha kuuza ndani ya siku tatu.

Itakubidi uchakarike kuleta bidhaa inayouzika ndani ya siku tatu, kwa kweli ni kitu rahisi kama ifuatavyo:
Hatua 1: Weka mawazo yako mahali husika. Hii ndio sehemu ngumu na muhimu kuliko zote.
Hatua 2: Tengeneza jawabu linalouzika la tatizo MOJA. ni rahisi na hatua muhimu
Hatua 3: peleka nenda kauze. unaweza kuchukua dakika 30- 60. Kama natania? Inawezekana? Tutajadili!
Wazo la kutengeneza bidhaa na kuuza ndani ya siku tatu inaweza kufanya vichwa vya watu vizunguke. Lakini kuzungusha vichwa ndio kunahusu mambo ya mauzo.
Haya tuendelee- tuanze na kukupatia wewe na bidhaa zako kuvutia wanunuzi kila mwezi

Hatua 1: Weka mawazo yako mahali husika.
Hapa naangalia vitu vitatu ambavyo winaweza vikasimama kati ya ''wewe sasa hivi'' na ''wewe na bidhaa yako mpya ya kuuza ndani ya siku tatu'' uoga, ubinafsi na imani zinazokuzuia
Hapa nataja uoga, ubinafsi na imani potofu kama mtaji usio na lazima kwa sababu nataka uone hivi vitu vitatu havina manufaa na vya kipuuzi. Vitakukwaza na kukuzuia kusaidia watu, kutatua matatizo yao na wewe kufanikiwa.
Kwa nini nasema haya
Uoga: upo maishani kila siku
Kuna wakati uoga ni mzuri na ni wenye afya. Mfano unataka kuvuka barabara, magari yanakuja kwa kasi. Akili zako zitakwambia ''wewe acha usivuke, yatakugonga'' unasubiri mpaka yaishe au yasimame. Wakati huu uoga ni mtaji. Unakuwezesha kuishi, na kama wewe ni mwenye akili timamu lazima uupe nafasi.
Lakini tatizo linakuja wakati unaweka imani potofu na kuamini kilakitu uoga unasema, kwa sababu unaanza kuwa na hisia kuhusu vitu ambavyo havikuui vinakufanya usiwa sawasawa au mjinga. Vitu hivyo ni kama:
Uoga wa kukataliwa: unaweza ukakataliwa wakati umeomba utoke out na mtu, au unaweza kujaribu kuuza bidhaa usiwe na mnunuzi. Hii ni kawaida na ni hatua njema. Ni kitu cha kawaida katika hatua uliyofikia
Uoga wa kushindwa: unaweza kujaribu wazo zuri na ukagundua kuwa haliwezekani. Watu wanaewza kufikiri ''humalizi ulichokianza'' au ''hilo lilikuwa wazo bovu'' basi nikwambie! Kwa uhalisia watu wanaosaka pesa wanaita haya makosa jiwe la kukupandisha ( na watu ambao hawachukui hatua mara nyingi huonea wivu wale wanaotenda- hata kama wanafanya makosa)
Uoga wa kazi: inaonekana ni wa kitoto, lakini ni uoga mkubwa kwa wengi wetu. Mradi unaonekana MKUBWA! ( hivyo, ufanye kuwa mdogo na utakuwa taratibu) Mradi unaonekana MGUMU (hivyo tafuta namna ya kuufanya rahisi) Mradi unachukua JITIHADA KUBWA wakati kuna vingi vya kufanya! ( hahahaa ndio hayo wanaofanikiwa hufanya) hivyo itakubidi ufanye kazi kwa bidii sana? Hii haitishi. Lakini sii rahisi. Fanya kazi achana na fikra hizo waingereza wana msemo wao wanakwambia ''mbwa mzuri hupata thawabu'' chagua kuwa mbwa mzuri kuliko mbwa ''koko''
Uoga una mahali pake- wakati unaokoa maisha yako, au unapozuia janga, ni mzuri. Lakini kwa umakini, tunaongelea kuhusu kutengeneza bidhaa haraka ya kuuza katika njia ambayo biashara yako itakua kila mwezi kidogo kidogo. Ni mbinu nitakayokupa nan i kitu unaweza kufanya hata bure- hivyo huna haja ya kutoa kisingizio na kusikiliza uoga kwa dakika chache.
Usifikiri kutengeneza bidhaa haraka ni KITU CHA KUTISHA; fikiria kama ni jaribio. Watu wataweza kukukatalia, lakini wengine watanunua. Inaweza isifanye kazi kama unavyotegema lakini utakuwa umepata matokeo badala ya kuwa na mawazo yasiyo na tija.
Nakwambia, itakuwa ni kazi lakini ni kazi ambayo itakuinua na kukufanya makini
Umuhimu wa kutengeneza bihdaa ya KWANZA / ua ya PILI sio wa kukufanya wewe kuwa tajiri, ni wa kukupa kipato kitakachokuwa kinakuwa kila mwezi. (unaweza kuamua nini cha kufanya kukupa utajiri kama ukitaka baadaye. Siwezi kumwambia kila mtu hilo)

UBUNAFSI: Ngumi ya tumbo iletwayo na uoga
Mara nyingi nawaambia wateja hakuna haja ya kuwa mbinafsi, mara nyingi huwa wanachukia na kuuliza ninamaanisha nini. ( hunilipi fedha yoyote, lakini nataka nikupe mbinu sawa na ninazotoa kwa wateja, wacha nikuelezee)
Kama unahisi unaogopa kutengeneza bidhaa wewe UNA UBUNAFSI. Uoga wako ni wa kipuuzi kwa sababu inazuia shuluhu kwa watu wenye tatizo linalohitaji kutatuliwa.
Kama kuna mtu ana umwa kifua na wewe una sanduku la dawa, je? Utajiskia vibaya kumuuzia? Je utasitasita? Je hutamuona na kuzungumza nae ajue una nini cha kumsaidia? Hapana! Utamuuzia hiyo dawa na kujiskia vizuri kwa kile ulichofanya.
Sasa angalia. Unajua ulichonacho. Hicho kinaweza kuwasaidia watu kutatua matatizo yao. Inamaanisha unatatua matatizo yao au kusaidia kupata taarifa wanayohitaji haraka. Au labda unajua namna ya kuwafanya watu wawe na furaha kwa kuwaburudisha au kuwatia moyo. Na ni kuwa unajua namna ya kufanya maisha/biashara/ au chochote
Kwa hivyo umeona namna ambavyo huwezi kutengeneza bidhaa kwa sababu ni ngumu, au hakuna atakayependa kununua au hujiskii kuuza au hadithi yoyote unayojiambia, fikiria unamwambia hayo mgonjwa wakati una sanduku la dawa zinazoweza kumtibu. Usingeweza, maana ungefikiria mahitaji ya mwingine badala ya kuwa na ubinafsi.
Hapa sikwambii kuwa kama hautatumia ujuzi wako kuzalisha bidhaa zako wewe ni mbinafsi. Hakuna kinachokuzuia ujuzi wako wa kuzalisha. Lakini fikiria kuwa; kama una uuoga na hofu kuhusu kuuza maarifa yako ni kwa sababu mtazamo wako uk kwako mwenyewe na SII kuwasaidia watu.
Kama utajali mahitaji yao- kwa uhakika, pima kiwango utakachoweza kutoa- haafu kuuza bidhaa zako kutakuwa kwa kufurahia. Wewe hujaribu kupata fedha kwa watu , wewe unajaribu kuwapa fursa kwa matatizo yao kutatuiwa. Na unajiskia vizuri.
Hivyo unapokuwa na uoga na hofu inabisha hodi, jiambie acha ubinafsi. Weka mawazo yako kwa watu ambao unaweza utawahudumia.
Imani zinazokuzuia: Hufunga milango ya mafanikio.
Ni rahisi kufikiria ambayo ''huwezi kufanya'' au ''ambayo huna'' vitu unavyohitaji. Naweka ''huwezi'' na ''sina'' kwenye mabano kwa kuwa muda mwingi tunasema maneno hayo kwa kujidanganya na kuyatumia kama kisingizio ili tusifanye kazi inayotakikana kufanikisha.
Kwanza, tunaposema '‘hatuna'' au ''hatuwezi'' wakati mwingi tunamaanisha ''hatuta''(hatutafanya) lakini hanuna uwezo kutamka wazi wazi.
Kwa mfano, wakati naongea na simu na mtu akiniambia ''hawezi'' kuwa na muda kufanya mradi mpya( kama vile kutengeneza bidhaa kwa siku tatu, Namuuliza utaangalia kipindi gani kwenye runinga wiki hii. Nawauliza muda gani watautumia kwenye facebook na whattsup ku ''jenga biashara''
Mara nyingi hukaa kimya, ni dhahiri kuwa hutambua wana muda, lakini hawatautumia kwa kile kinachowanufaisha. Hivyo ni kazi yangu kuwaambia ''najua unajiskiaje na ndio hivi nilifanya iliponitokea'' (hii ni mada ya siku nyingine)
Au mtu anakwambia sitaweza kutangaza redioni, au kwenye internet au kuchapisha vipeperushi au sijajipanga kufanya mauzo makubwa. Hivyo mimi huwakumbusha kuwa hizo ni imani zuilifu, kwa kuwa wanaweza kufanya mengi zaidi ya wanayoyafikiria kwa sasa.
--------------------------------------------------------------------------
Asante kwa kusoma kwa leo somo linaishia hapa tutaendelea

updates tarehe 29/6/2014

Namna ya kuondokana na imani zuilifu ni kuondokana na neno ''siwezi'' swali la kujiuliza ni ''nini unaweza'' kufanya kwa sasa. Imani zilifu zinanguvu pale tu ambapo unafikiria kuhusu kile ambacho huwezi/hujawa/huna.

Hatua ya pili: Tengeneza suluhisho la kuuzika la tatizo moja

Kutengeneza bidhaa ndani ya masaa 24 ni kitu kinachowezekana. Inaweza kuwa ngumu kuamini kama unafikiri ''bidhaa'' ni kitu kigumu kuandaa na huchukua muda mrefu kukamilisha. Hapa unafikiria bidhaa unazonunua dukani.
Kama unawazo hilo kuhusu bidhaa, kidogo litakutisha. Lakini nataka ufikirie bidhaa kwa maana ifuatayo
Kwamba ni kitu/kifaa chenye kazi moja kwa ajili ya kutatua tatizo husika au kumuwezesha mtu kupiga hatua tofauti na alivyokuwa. Kinaweza kuwa tu kitu kimoja ambacho jamii inakihitaji.
Chuma ya kutundikia nguo (hanger) VS kabati la nguo
hanger.jpg kabati.JPG
Namna unavyofikiria ''bidhaa'' labda unafikiria kabati. Kabati lina kila kitu maana unafikiri watu wanahitaji kila kitu. Sio kosa lako, ingawa wauzaji wanaweka vitu vingi kwenye bidhaa na kuzifanya zitishe ili ufanye mengi kuzikamilisha.
Nataka ubadili mtazamo wako na ufikirie chuma ya kutundikia nguo badala ya kabati. Kwa umakini ninapohitaji kutundika nguo, siangalii mtu mwenye kabati- natafuta chuma ya kawaida ya kuundikia nguo. Sawa nitakuwa na furaha nikipata kabati yenye sehemu ya kutundikia nguo kama ina sehemu hiyo lakini sitakataa kifaa ambacho kitaweza kufanya kazi ile ile.
Jamii ina matatizo yanayohitaji kutatuliwa. Huhitaji kuyatatua yote ili kupata fedha. Unaweza kutoa suluhisho moja kwa muda- kitu ambacho wanaweza kutumia haraka ( na baadae waje kwako kuchukua tena)
Tuongelee namna ya kufanya- naamini ukitumia muda mchache wa ziada unaweza ukapata bidhaa yako ndani ya siku tatu.
(hili wazo wengi wanaona haliwezekani, nataka nikwambie ambao wamejaribu limefanya kazi, na baadhi wameanza mauzo haraka) fuata hatua zifuatazo:

  1. Chukua kalamu na karatasi. Fikiria kuna mtu anahitaji ushauri katika eneo ambalo umebobea/fani / hata nje ya fani yako na una dakika 20-30 za maongezi
  2. Fikiria swali la muhimu(moja tuu) ambalo watu wengi wanakuuliza/ wanakujia uwasaidie/ wanauhitaji nalo
  3. Jibu swali lako kwa kuainisha point za muhimu
  4. Fafanua point zako
Unapata wazo gani?

Hatua ya tatu: uza wazo lako
Zamani ilikuwa kazi ngumu kuuza. Lakini sikuizi mitandao ya kijamii inasaidia kufanya kazi hii. Whattsup, facebook, viber, blog na kadhalika na kusaidia kutangaza biashara yako. Pamoja na njia za kawaida za kutembeza bidhaa au huduma.Nataka nikwambie kuwa watu hununua vitu madukani kwa kuwa wanataka suluhisho la haraka. Fikiria bidhaa kama mkate- mtu ananunua kwa kuwa inamchukua muda na utaalamu kutengeneza kwake, na pengine atahitaji kitu cha kula cha haraka, haina maana mkate ni bora sana. Fikiria mmbu wanakusumbua utatoka utafute dawa ya kuua mbu. Fikiria unga umeisha, Badala ya kulima mahindi usage mwenyewe unakwenda kununua unga. nakutakia mafanikio, ukianza mapema utapata uzoefu na kukuza biashara yako. utakapopata wazo lako unaweza kuliboresha zaidi kwa hudhuria mafunzo ya wajasiliamali, kujisomea vitabu, majarida au kujifunza kwa vitendo kwa wanaoto bidhaa au huduma. asante.

_____________________mwisho____________________________________________________________________________________
 
Mwenye kuweza kuandika kwa kugha rahisi atufafanulie kidogo tafadhali
 
Back
Top Bottom