Namna ya kukabili harufu mbaya ya miguuni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
NAMNA YA KUKABILI HARUFU MBAYA YA MIGUUNI.

Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.


Miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wakiwa wanaume.

Katika nyakati hizi za mvua, tatizo hili linaonekana kuzidi kuwa sugu, hali inayosababisha kuwepo na harufu mbaya hasa kwenye mikusanyiko ya watu kama vile kwenye daladala.

Lakini watu wengi wenye tatizo hili huwa wagumu kukubaliana na hali yao hata kutafuta tiba mahususi inaweza kuwaondolea kero hiyo.


Licha ya kuwepo sababu mbalimbali zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli utabaki kuwa uchafu ndiyo chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.


Kwa kiasi kikubwa uchafu huo ndio unasababisha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu na kuwakera wanaokumbana na harufu hiyo.


Pamoja na tiba nyingine za kitaalamu ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kupata, usafi ni jambo kubwa analopaswa kuzingatia zaidi hasa kipindi hiki cha mvua.


Ukigundua una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.


Kila unapovaa viatu vya kufunika, hakikisha unavaa soksi safi na kavu. Epuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vyema kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu.


Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.


Kama utahisi tatizo ni kubwa zaidi ni vyema utumie sabuni zenye dawa za kuua vijidudu pamoja na mafuta maalumu yanayoweza kutumika miguuni. Ikishindikana, nenda kwa wataalamu wa afya.

Kwa Ushauri wa Maswali na Matibabu ta Maradhi yoyote yale wasiliana na mimi Kwa njia ya email Baruwa ya

pepe Email Address yangu hii hapa

fewgoodman@hotmail.com Pia waweza kunitembelea kwenye Blog yangu bonyeza hapa Mzizi Mkavu

 

Attachments

  • 10245397_10154027619410198_4255074470281263401_n.jpg
    9.5 KB · Views: 210
  • 10169182_10154027620165198_7571485632811871157_n.jpg
    17.9 KB · Views: 209
  • 10168198_10154027619880198_1190400205886429264_n.jpg
    23.6 KB · Views: 193
jamani miguu yangu inanikosesha raha kabisa yaani inanuka, unajua kunuka mpaka baasi naweza kubadili soksi hata mara tatu kwa siku lakini bado haisaidii, msaada tafadhali.
 
Nunua mafuta Miski(Misk nyekundu itakua ni nzuri...nyeupe sio mbaya pia)..na uwe unairowanisha io misk na vipamba vidogo na uweke katika pachikwa za vidole....
 
Nunua mafuta Miski(Misk nyekundu itakua ni nzuri...nyeupe sio mbaya pia)..na uwe unairowanisha io misk na vipamba vidogo na uweke katika pachikwa za vidole....

Hapo ndugu yangu deal na fungus na siyo harufu hata ukibadilsha ngoz yaweza isisaidie kwan we sio mchafu kama waweza badili soksi had mara2 tatzo ni bakteria hvo anza nao hao na pia badil mazingra yanayo wavutia kama miguu kuwa na unyevu muda mrefu hasa utokanao na kuvaa viatu muda mrefu.
 
Wadau nimenunua pair 4 za viatu vya ngozi mtumba,sasa tatizo vinatoa harufu kali!Kwa wale mliowahi kukutana na tatizo hilo na mkalishinda naombeni ushauri!!!
 
Pair 4 zote ziwe zinanuka?

Hizo zitakuwa ni soksi zako au miguu yako.
 
Lakini mimi kila ninapovaa ninabadilisha soksi!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…