Wakuu tumeona namna ndugu zetu MPs Msigwa na Lema wanavyojiuma uma katika kujieleza Kwa kingereza ili dunia iweze kuwaelewa.
Humu JF kuna wataalamu wengi sana wanaojua vizuri English japo kuwa hawajaishi nchi zinazoongea English kama lugha ya taifa hivyo tunaweza peana mbinu za kumudu hii lugha.
Mimi Kwa uzoefu wangu naamini kusoma sana vitabu mbali mbali vya kingereza itasaidia sana kuongeza vocabularies katika English na itasaidia sana kunyoosha sentensi maana nyingi zitakuwa ni marudio ya vitabu ulivyosoma.Pia kujaribu kuangalia sana movies hasa series inaweza saidia kusikiliza matamshi ya maneno mbalimbali.
Hizo ni Kwa mtazamo wangu hivyo naomba tubadilishane mbinu ili tusiwe kama Lema (Mr Actually) na wengine wengi wanaoweza kututia aibu huko majukwaa ya kimataifa.
Karibuni Kwa michango yenu!