Namna ya kuokoa nyumba isiuzwe kwa kushindwa kulipa mkopo

IJUE SHERIA

Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
11
Reaction score
147
NAMNA YA KUOKOA NYUMBA ISIUZWE KWA KUSHINDWA KULIPA MKOPO.

upload_2018-2-2_10-24-10.jpeg

Na Mwanasheria Wetu.

Wakopaji nao wana haki zao. Yapo mambo ya msingi ambayo wanapaswa kuyajua ili yawalinde iwapo mambo yamewaendea vibaya.

Ukweli ni kuwa ni busara unapokopa kulipa deni lakini iwapo sababu za kibinadamu zimejitokeza ambazo ziko nje ya uwezo wa mkopaji na ambazo kwa namna yoyote hawezi kuzizuia basi ni vema mkopaji awe na njia ya kujiokoa yeye pamoja na mali yake.

Uwepo wa sababu za kibinadamu zinazoweza kumzuia mtu kulipa deni ndizo zilizopelekea kuwapo baadhi ya mambo katika sheria ambayo humlinda mkopaji pamoja na mali yake ikiwa ameshindwa kulipa mkopo au amechelewa kwa mujibu wa makubaliano.

Si kweli kuamini kuwa mtoa mkopo ndiye mwenye ulinzi wa sheria peke yake, hapana hata mkopaji naye anao ulinzi wa sheria ikiwa mambo yatamwendea vibaya kama tutakavyoona.

Kwanza tuangalie sababu za kibinadamu ambazo zinaweza kumfanya mkopaji ashindwe kulipa deni kwa wakati.

1.SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MKOPAJI ASHINDWE KULIPA DENI.

( A ) MATENDO YA MUNGU ( Acts of God ).
Matendo ya mungu hujumuisha magonjwa/ugonjwa ambao huweza kumsababisha mtu ashindwe kabisa kuendelea na biashara kwa namna yoyote ile. Mtu hawezi kuwa amelazwa na hajitambui au anajitambua lakini ugonjwa wake ni mkubwa ( serious) halafu ukategemea afanye biashara na arejeshe deni kwa wakati.

Ni jambo ambalo haliingii akilini. Ugonjwa ni matendo kati matendo ambayo husababishwa na mungu na yako juu ya uwezo wa mwanadamu yeyote. Zaidi, matendo ya mungu hujumuisha vitu kama mafuriko, matetemeko ya ardhi, ukame, vimbunga, na kila kitu ambacho hakiwezi kusababishwa na mwanadamu. Ni vigumu mkopaji kurejesha deni iwapo moja ya matendo haya yameikumba biashara yake.

( B ) AJALI ISIYOZUILIKA ( innevitable accident) .
Ajali ni ajali suala la msingi ni kuwa ajali isiwe imesabaabishwa kwa makusudi na mkopaji ili akwepe kurejesha deni. Kwa mfano juzi tumeshuhudia ajali ya basi lililoangukiwa na lori njia ya mbeya. Mle ndani walikuwamo watu wana biashara zao ambazo zimetokana na mkopo na nyingi zimepotea kabisa. Katika mazingira yanayotambulika kama hayo hakuna namna ambavyo unaweza kulazimisha kuuza nyumba/kiwanja cha mtu eti kwakuwa amechelewa kulipa ilihali kilichomchelewesha kinajulikana.

Hiyo ni ajali isiyozuilika na lazima watoa mkopo waizingatie. Pia tulishuhudia ajali za meli kule Zanzibar ambazo lazima ndani yake walikuwamo wafanybiashara wakiwa na biashara za fedha za mikopo. Itakuwa sio sawa kuharakia kuuza dhamana ya mfanyabiashara kama huyu wakati sababu iliyomchelewesha kurejesha ikiwa wazi.

AVita ndani ya nchi pia huingia katika ajali isiyozuilika na ni sababu ya msingi ya kuzingatia iwapo mkopaji ameshindwa kurejesha mkopo.

( C ) SABABU ZA KIDOLA/KIUTAWALA. (Executive Authority ).
Kwa mfano mkopaji ameweka biashara yake mahali fulani halafu serikali ikaja na sera ya kumuondoa eneo lile kwa lengo la kuweka mradi fulani kwa ajili ya taifa, au serikali imebadili utaratibu wa fedha ghafla kwa kuongeza viwango vya riba tofauti na vile alivyokopea mkopaji au mabadiliko yoyote ya kisera ambayo moja kwa moja yanaathiri kwa kiwango kikubwa biashara na mkopo wa mkopaji.

Sababu hii itakuwa nje ya uwezo wa mkopaji na yafaa izingatiwe kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kuuza mali yake.

( D ) SABABU ZITOKANAZO NA SHERIA/MAHAKAMA ( statutory/judicial acts).
Yawezekana mtu amechukua mkopo lakini wakati akiendelea na biashara amehukumiwa kifungo au hajahukumiwa lakini yupo rumande na hana dhamana. Mtu huyu ni vigumu kurejesha mkopo. Au mtu amefungua biashara lakini kuna matatizo ya kisheria yamejitokeza na mahakama imetoa amri ya kumzuia kuendelea na biashara au amri ya kulifungia eneo lake la biashara.

Pia mtu kama huyu hututarajii arejeshe mkopo kwa wakati kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.

2.NAMNA YA KUOKOA NYUMBA/KIWANJA KISIUZWE KWA KUSHINDWA/KUCHELEWA KULIPA MKOPO.

Tutaongozwa na Sheria Namba 4 na 5 za ardhi pamoja na Sheria ya rehami za mikopo " Mortgage Financing (Special Provisions) Act, 2008".

Ni hivi, ikiwa zipo sababu za msingi za kushindwa/kuchelewa kulipa mkopo kama nilizotaja hapo juu basi waweza kuzuia nyumba/kiwanja chako kisiuzwe. Njia kubwa , nzuri na ya uhakika ni mahakama.

Utaratibu wake ni kuwa utafungua kesi mbili yaani ndogo na kubwa.
Katika kesi kubwa utakuwa ukieleza kilichotokea kwa ukamilifu mpaka ukashindwa kulipa deni na ndani ya kesi ndogo utakuwa ukiomba nyumba/kiwanja chako kisiuzwe kwakuwa wewe si msababishaji wa kilichotokea.

Kesi ndogo itafunguliwa chini ya hati ya dharula( certificate of urgency) ili iweze kusikilizwa kwa muda mfupi na kutolewa maamuzi ili kuwahi wauzaji kabla hawajauza.

Maamuzi ya kesi ndogo yaweza kutolewa hata ndani ya siku moja kutegemea na udharula wenyewe.

Zingatia kuwa ikiwa thamani ya mkopo au eneo linalotaka kuuzwa inaanzia milioni 50 kesi itafunguliwa mahakama kuu , na ikiwa chini ya hapo itafunguliwa baraza la ardhi na nyumba la wilaya.

Hata hivyo ikiwa chini ya milioni 3 itafunguliwa baraza la ardhi la kata. Ila hapa utaratibu wa kufungua utakuwa tofauti kidogo. Hapa utatoa tu maelezo kwa mdomo na kesi itakuwa imefunguliwa tayari.

Pia zingatia kesi ya namna hii hufunguliwa katika kata, wilaya lilipo hilo eneo linalotaka kuuzwa.

Kwa kufuata utaratibu mzuri waweza kuokoa nyumba/kiwanja chako kisiuzwe kwa kuwa hiyo nayo ni haki yako kama mkopaji.

MAONI +255784482959
 
NAMNA YA KUOKOA NYUMBA ISIUZWE KWA KUSHINDWA KULIPA MKOPO.

View attachment 689171

Asante kwa uwasilishaji
 
Weka vifungu mwanasheria, naona umeanza kwa kusema utatumia sheruia namba 4 na 5 pamoja ile ya Mortgage, vifungu gani?
 
Huo uamuzi mdogo,wanaokudai,si watakata rufaa?Au huo uamuzi ukishinda,haukatiwi rufaa?
 
Kwa mujibu wa sheria uamuzi mdogo (interlocutory decision) haukatiwi rufaa mpaka kesi ya msingi itakapomalizika ama kwa mahakama kutoa hukumu au kufuta kesi au vinginevyo. Hii ni kwa mujibu Haya (d) ya Kifungu Kidogo cha (2) cha Kifungu cha 5 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa [Sura ya 141 Toleo la Mwaka 2002] yaani The Appellate Jurisdiction Act, 1979 kwa rufaa za kwenda mahakama ya rufaa na Kifungu Kidogo cha (2) cha Kifungu cha 74 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Madai [Sura ya 33 Toleo la Mwaka 2002] kwa rufaa za kwenda mahakama kuu na hii kunga ya sheria iliingizwa kwenye vifungu vya sheria tajwa kupitia mabadiliko ya Sheria Zilizoandikwa (Mabadiliko Mchanganyiko) ya mwaka 2002 yaani The Written Laws (Miscellaneous Amendment) Act, 2002 ambayo ni Sheria Na. 25 ya Mwaka 2002. Mahakama kupitia hukumu za kesi kadhaa imetamka kwa kauli moja kuwa uamuzi mdogo ambao haufikishi kesi katika ukomo hauwezi kukatiwa rufaa , pamoja na kesi zingine uamuzi kama huu ulifanywa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya DENNIS FRANCIS NGOWI APPELLANT VS ASTERIA MORRIS AMBROSE, CIVIL APPEAL NO.90 OF 2014.

Naomba kuwasilisha.
 
Safi sana mwanasheria maana sio mchoyo ya elimu hii ya sheria maana watz haya mambo yametupiga chenga kali mno.
 
Wewe mtoa mada ni ngumu sanaa raia wa kawaida kuelewa kesi ndogo na kubwa ktk mashauri hayo, waelezee watu ni vitu gani ivyo, mtu anaanzaje kuvifungua, na anasemaje sasa akitaka kuvifungua.
 
Vizuri.. Wakopaji wengi wamepoteza mali walizoweka kama dhamana.

Mara nyingi, utakuta nyumba inabandikwa matangazo ijumaa jioni kuwa itapigwa mnada kesho yake j1 au j2, so muda wa kufungua hzo kesi unakuwa haupo.

Kwny mazingira kama hayo mhanga anaweza kujiokoa vipi?
 
jamaa hajarudi kukujibu
 
Umenikumbusha tukio la kuvunjwa kwa FOUR WAYS BAR (ilikuwa pale Mwenge njia ya kwenda Coca cola) na Halmashauri ya Kinondoni! Timing na hesabu zilikuwa kama unavosema!
 
NAMNA YA KUOKOA NYUMBA ISIUZWE KWA KUSHINDWA KULIPA MKOPO.

View attachment 689171

Na Mwanasheria Wetu.

Wakopaji nao wana haki zao. Yapo mambo ya msingi ambayo wanapaswa kuyajua ili yawalinde iwapo mambo yamewaendea vibaya.

Ukweli ni kuwa ni busara unapokopa kulipa deni lakini iwapo sababu za kibinadamu zimejitokeza ambazo ziko nje ya uwezo wa mkopaji na ambazo kwa namna yoyote hawezi kuzizuia basi ni vema mkopaji awe na njia ya kujiokoa yeye pamoja na mali yake.

Uwepo wa sababu za kibinadamu zinazoweza kumzuia mtu kulipa deni ndizo zilizopelekea kuwapo baadhi ya mambo katika sheria ambayo humlinda mkopaji pamoja na mali yake ikiwa ameshindwa kulipa mkopo au amechelewa kwa mujibu wa makubaliano.

Si kweli kuamini kuwa mtoa mkopo ndiye mwenye ulinzi wa sheria peke yake, hapana hata mkopaji naye anao ulinzi wa sheria ikiwa mambo yatamwendea vibaya kama tutakavyoona.

Kwanza tuangalie sababu za kibinadamu ambazo zinaweza kumfanya mkopaji ashindwe kulipa deni kwa wakati.

1.SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MKOPAJI ASHINDWE KULIPA DENI.

( A ) MATENDO YA MUNGU ( Acts of God ).

Matendo ya mungu hujumuisha magonjwa/ugonjwa ambao huweza kumsababisha mtu ashindwe kabisa kuendelea na biashara kwa namna yoyote ile. Mtu hawezi kuwa amelazwa na hajitambui au anajitambua lakini ugonjwa wake ni mkubwa ( serious) halafu ukategemea afanye biashara na arejeshe deni kwa wakati.

Ni jambo ambalo haliingii akilini. Ugonjwa ni matendo kati matendo ambayo husababishwa na mungu na yako juu ya uwezo wa mwanadamu yeyote. Zaidi, matendo ya mungu hujumuisha vitu kama mafuriko, matetemeko ya ardhi, ukame, vimbunga, na kila kitu ambacho hakiwezi kusababishwa na mwanadamu. Ni vigumu mkopaji kurejesha deni iwapo moja ya matendo haya yameikumba biashara yake.

( B ) AJALI ISIYOZUILIKA ( innevitable accident) .
Ajali ni ajali suala la msingi ni kuwa ajali isiwe imesabaabishwa kwa makusudi na mkopaji ili akwepe kurejesha deni. Kwa mfano juzi tumeshuhudia ajali ya basi lililoangukiwa na lori njia ya mbeya. Mle ndani walikuwamo watu wana biashara zao ambazo zimetokana na mkopo na nyingi zimepotea kabisa. Katika mazingira yanayotambulika kama hayo hakuna namna ambavyo unaweza kulazimisha kuuza nyumba/kiwanja cha mtu eti kwakuwa amechelewa kulipa ilihali kilichomchelewesha kinajulikana.

Hiyo ni ajali isiyozuilika na lazima watoa mkopo waizingatie. Pia tulishuhudia ajali za meli kule Zanzibar ambazo lazima ndani yake walikuwamo wafanybiashara wakiwa na biashara za fedha za mikopo. Itakuwa sio sawa kuharakia kuuza dhamana ya mfanyabiashara kama huyu wakati sababu iliyomchelewesha kurejesha ikiwa wazi.

AVita ndani ya nchi pia huingia katika ajali isiyozuilika na ni sababu ya msingi ya kuzingatia iwapo mkopaji ameshindwa kurejesha mkopo.

( C ) SABABU ZA KIDOLA/KIUTAWALA. (Executive Authority ).
Kwa mfano mkopaji ameweka biashara yake mahali fulani halafu serikali ikaja na sera ya kumuondoa eneo lile kwa lengo la kuweka mradi fulani kwa ajili ya taifa, au serikali imebadili utaratibu wa fedha ghafla kwa kuongeza viwango vya riba tofauti na vile alivyokopea mkopaji au mabadiliko yoyote ya kisera ambayo moja kwa moja yanaathiri kwa kiwango kikubwa biashara na mkopo wa mkopaji.

Sababu hii itakuwa nje ya uwezo wa mkopaji na yafaa izingatiwe kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kuuza mali yake.

( D ) SABABU ZITOKANAZO NA SHERIA/MAHAKAMA ( statutory/judicial acts).
Yawezekana mtu amechukua mkopo lakini wakati akiendelea na biashara amehukumiwa kifungo au hajahukumiwa lakini yupo rumande na hana dhamana. Mtu huyu ni vigumu kurejesha mkopo. Au mtu amefungua biashara lakini kuna matatizo ya kisheria yamejitokeza na mahakama imetoa amri ya kumzuia kuendelea na biashara au amri ya kulifungia eneo lake la biashara.

Pia mtu kama huyu hututarajii arejeshe mkopo kwa wakati kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.

2.NAMNA YA KUOKOA NYUMBA/KIWANJA KISIUZWE KWA KUSHINDWA/KUCHELEWA KULIPA MKOPO.

Tutaongozwa na Sheria Namba 4 na 5 za ardhi pamoja na Sheria ya rehami za mikopo " Mortgage Financing (Special Provisions) Act, 2008".

Ni hivi, ikiwa zipo sababu za msingi za kushindwa/kuchelewa kulipa mkopo kama nilizotaja hapo juu basi waweza kuzuia nyumba/kiwanja chako kisiuzwe. Njia kubwa , nzuri na ya uhakika ni mahakama.

Utaratibu wake ni kuwa utafungua kesi mbili yaani ndogo na kubwa.
Katika kesi kubwa utakuwa ukieleza kilichotokea kwa ukamilifu mpaka ukashindwa kulipa deni na ndani ya kesi ndogo utakuwa ukiomba nyumba/kiwanja chako kisiuzwe kwakuwa wewe si msababishaji wa kilichotokea.

Kesi ndogo itafunguliwa chini ya hati ya dharula( certificate of urgency) ili iweze kusikilizwa kwa muda mfupi na kutolewa maamuzi ili kuwahi wauzaji kabla hawajauza.

Maamuzi ya kesi ndogo yaweza kutolewa hata ndani ya siku moja kutegemea na udharula wenyewe.

Zingatia kuwa ikiwa thamani ya mkopo au eneo linalotaka kuuzwa inaanzia milioni 50 kesi itafunguliwa mahakama kuu , na ikiwa chini ya hapo itafunguliwa baraza la ardhi na nyumba la wilaya.

Hata hivyo ikiwa chini ya milioni 3 itafunguliwa baraza la ardhi la kata. Ila hapa utaratibu wa kufungua utakuwa tofauti kidogo. Hapa utatoa tu maelezo kwa mdomo na kesi itakuwa imefunguliwa tayari.

Pia zingatia kesi ya namna hii hufunguliwa katika kata, wilaya lilipo hilo eneo linalotaka kuuzwa.

Kwa kufuata utaratibu mzuri waweza kuokoa nyumba/kiwanja chako kisiuzwe kwa kuwa hiyo nayo ni haki yako kama mkopaji.

MAONI +255784482959
Asante kwa maaelezo mazuri sana, mimi tatizo langu biashara nilionayo imekufa hivyo nimeshindwa kulipa mkopo wangu hapo natakiwa kufanya nini?
 
Back
Top Bottom