Namna ya kuomba ajira ya ualimu wa sekondari Serikalini

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,093
Reaction score
7,229
Salamu wana JF,

Ninaomba msaada wa kujua utaratibu wa kufata unapotaka kuomba ajira ya ualimu wa sekondari serikalini kwa mwenye shahada ya kwaanza ambaye yuko kwenye mfumo wa taasisi binafsi, mlengwa ni muhitimu wa wa shahada ya elimu mwaka 2012 , hasa ukizingatia kuwa nafasi za ajira ya ualimu wa sekondari hazitangazwi kwenye vyombo vya habari. Mlengwa anatamani sana kujiunga na ajira ya ualimu wa sekondari katika serikali ila sijajua namna ya kufanya . Ikumbukwe kuwa ajira za ualimu 2014/2015 bado hazijatangazwa mpaka sasa na serikali , hivyo nadhani inaweza kuwa nafasi mwafaka kwangu kupata nafasi hii adimu ili niweze kulitumikia taifa langu.

Kwa yeyote Mwenye kujua nini cha kufanya au utaratibu upi wa kufuatwa , au kuniunganisha na wahusika muhimu wataomsaidia , tafadhali tuwasiliane hapa jukwaani, na pia kwa maelezo zaid naomba uni PM .

Asanteni kwa mawazo yenu na ushauri mtaonipa.
N.B:Matumizi ya lugha ya staha ni muhimu .
 
Mimi sio mwalimu ila kunajamaa yangu alikuwa na shida kama yako akaambiwa aandike barua ya maombi TAMISEMI, ila ngoja waje wadau wanaofaham zaidi
 
Mimi sio mwalimu ila kunajamaa yangu alikuwa na shida kama yako akaambiwa aandike barua ya maombi TAMISEMI, ila ngoja waje wadau wanaofaham zaidi

Natumai ushauri wako umeelewaka vema , ni swala la mimi kutekeleza tu.Shukrani sana mkuu.
 
Kama ulishawahi kuajiriwa ukapewa check namba na ukakimbia kituoni imekula kwako
 
cha muhimu andika barua tamisemi na uipeleke manual na hakikhsha unaifanyia folo up
 
iyo mail kua nayo makin kunawatu watakuja wakwambie wao ndomaduka wa inshu hizo kumbe matapel
 
Andika barua tamisemi kwa katibu mkuu, jitahidi uandike kabla ya mwezi wa kumi na moja maana kuna mtu kanielekeza kuwa ndio mchakato unaanza wa kutoa ajira itakayotangazwa machi 2015,
Tuma kwenda
TAMISEMI
PO Box 1923
Dodoma tanzania
+255262322848
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…