Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Suala la posho ya vikao kwa wanasiasa Tanzania limekuwa ni aibu tupu kwa Taifa, ndani na nje ya Tanzania. Imefikia hadi wanathubutu kudai TShs million moja kwa siku. Watalaam kama madaktari na walimu wakiwa kwenye makongomano muhimu kama vile ya utafiti wa magonjwa kama ukimwi hawalipwi posho yo yote ya vikao, wao hulipwa tu posho ya kujikimu ambayo mara nyingi ni chini ya TShs 80,000/. Posho ya vikao hulipwa haswa wajumbe Bodi za mashirika ya umma ambayo nayo mara nyingi haizidi TShs 50,000/ kwa siku.
Tupendekeze jinsi ya kuondokana na aibu hii ya posho za vikao kwa wanasiasa wetu ambayo imejitokeza tena hivi karibuni kwenye vikao vya Bunge maalum la Katiba. Ninaanza na mapendekezo yafuatayo:
Tupendekeze jinsi ya kuondokana na aibu hii ya posho za vikao kwa wanasiasa wetu ambayo imejitokeza tena hivi karibuni kwenye vikao vya Bunge maalum la Katiba. Ninaanza na mapendekezo yafuatayo:
- Viwango vya posho vitangazwe na kujulikana kabla watu hawajaomba kupendekezwa kuteuliwa kuwa wajumbe kwenye vikao au tume hizi.
- Kabla ya mtu kuteuliwa ajaze fomu ya kukubali kuteuliwa kwa kiwango cha posho na masharti mengine yalizoainishwa kwenye fomu hiyo.
- Hata kwenye chaguzi za vyeo mbali mbali za kisiasa kama Uraisi, ubunge na udiwani viwango vya mishahara na posho zionyeshwe wazi kabla watu hawajaomba kuchaguliwa kwenye nafasi hizo. Mtindo wa sasa ni kuwa tunawachagua kwanza baada ya hapo tunawaachia wajipangie wenyewe mishahara na posho wanazopenda, tena tunawaambia hiyo iwe ni siri yao!
- Viwango vya posho hizi ziwe standarized kwa wanasiasa, watalaam na watendaji wengine wa serikali. Kusiwe na tofauti kubwa sana kati ya makundi haya. Hii keki ni ya sisi wote. Wale wanaoona posho hizi haziwatoshi wasiombe kuteuliwa au kuchaguliwa kwenye nafasi hizo.
- Kuhusu ombi la wajumbe wa Bunge la Katiba la kuongezewa posho ya vikao, kama Mheshimiwa Raisi ataliafiki, tunaomba idadi ya siku za vikao hivyo zipunguzwe ili jumla ya fedha zilizokuwa zimepangwa zisiongezeke na kusababisha madhara kwenye shughuli zingine za serikali kama vile huduma za afya na kupanda kwa kodi. Hili linawezekana kama atachaguiwa spika mwenye viwango na spidi. Kama NEC iliweza kujadili rasimu hiyo kikamilifu ndani ya siku 2 tu, nadhani hili linawezekana.