mkulu senkondo
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,862
- 3,574
Tanzania ni miongoni mwa nchi za ulimwengu wa tatu. Kwa kawaida, nchi za ulimwengu wa tatu (nchi zinazoendelea) hukabiliwa na tatizo kubwa la umaskini kwa raia walio wengi. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, raia katika nchi maskini hukabiliwa na matatizo kama; huduma mbovu za jamii, umaskini wa kipato, makazi duni, , magonjwa ya kuambukiza, utapiamlo na udumavu.
Hali ya uchumi kwa Watanzania.
Licha ya bidii na jitihada nyingi zinazoendelea kufanyika kwa ajili ya kupambana na adui umaskini, bado umaskini umewang'ang'ania Watanzania walio wengi. Nchini Tanzania, viashiria vya umaskini wa kipato kama; makazi duni, ukosefu wa ajira, huduma duni za kijamii, utapiamlo na udumavu hujidhirisha wazi katika maeneo yote ya nchi.
Hatua 5 muhimu katika kukabiliana na tatizo la umaskini nchini Tanzania.
Zipo njia nyingi za kukabiliana na umaskini ambazo tayari zilishawahi kufanyiwa kazi kwa vitendo ambapo baadhi zilionesha mwanga wa matumaini huku nyingine zikifeli kabisa. Kwa ujumla, mbinu nyingi za kukabiliana na tatizo la umaskini nchini Tanzania ni za muda mfupi tu! hivyo haziwezi kuondoa tatizo sugu la umaskini. Kwa kuzingatia muhtasari huo, andiko hili linakuja na mtazamo mpya na wa muda mrefu ili kufuta kabisa tatizo la umaskini wa kipato linalotukabili Watanzania.
Kuwekeza kwenye ujuzi na maarifa.
Hii ni mbinu ya kwanza kabisa na ya kudumu ya kukabiliana na umaskini. Watanzania lazima wafundishwe na waelewe kuwa, maendeleo yanaanzia kichwani na sio kwenye majukwaa au kupitia rasilimali asilia kama wanavyoaminishwa. Kuwa na rasilimali peke yake haitoshi kwa sababu akili ndio inayozipa rasilimali thamani. Ujuzi na maarifa ndio nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto. Ujuzi na maarifa husaidia sana katika kutatua matatizo na kuzivuna rasilimali. Kama nchi, ni muhimu sana kuwekeza kwenye kutafuta Ujuzi na maarifa ili kukabiliana na umaskini.
Kuishi kwenye uhalisia.
Ni lazima Watanzania wafundishwe kuwa umaskini walio nao hautaondoka kwa maombi au kutegemea miujiza! Umaskini ni mbaya na ni halisia. Umaskini hautafungashwa virago kwa kuroga, kuzindika, kuabudu sana wala kujiunga na Freemason! Watanzania lazima wafahamu kwamba, dini ni imani na imani ni suluhu ya kiroho ya matatizo yanayomkabili binadamu. Hivyo, tatizo halisia la umaskini haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kiroho. Dini ni moja ya eneo ambalo Watanzania wengi huwapotezea muda, kuwapumbaza, kuwafanya wasijiamini na kukwepa wajibu wa kupambana na tatizo la umaskini kwa kisingizio cha kumuachia Mungu. Sio nia ya andiko hili kupinga imani za watu lakini ni vema suala hilo likafanyika kwa kiasi na kubaki kuwa sehemu ya kuwaunganisha watu sambamba na kuyalinda maadili yetu.
Tatizo sugu la uvivu.
Mara baada ya Wakoloni Wajerumani kuanzisha mashamba katika koloni lao la Tanganyika mwishoni mwa karne ya 19 walilazimika kuingiza vibarua kutoka mashariki ya mbali (ref.collies experiment) wakiamini kwamba, Waafrika (Watanzania) hawawezi kufanya kazi. Wajerumani waliamini kuwa, Watanzania kiasili wamezaliwa wavivu (inborn lazy). Hata hivyo, baadae waligundua kuwa, sio kwamba Watanzania ni wavivu kiasili, bali wanapenda kupumzika kabla ya kuchoka (wavivu). Yaani hawataki kufanya kazi! hii ndio sababu ya Wajerumani kuwalazimisha Watanzania kufanya kazi kwenye mashamba yao (Forced labour).
Maana na nia ya kutanguliza maelezo hayo mafupi ni kuonesha ni kwa kiasi gani Watanzania hawapendi kufanya kazi na namna tatizo hilo lilivyo la kihistoria. Ni kweli Tanzania kuna rasilimali watu ya kutosha lakini kwa bahati mbaya haifanyi kazi! vijana (productive age) wapo wengi lakini hawafanyi kazi. Hakuna umaskini utakaotoka kwa jamii ya watu wavivu. Ni muhimu sana kwa jamii na serikali kuhakikisha kuwa, nguvu kazi ya taifa (vijana) inatumika ipasavyo kwani kundi hilo ndio jeshi la kupambana na kumshinda adui umaskini. Pia, kujali muda kiwe kipaumbele muhimu katika nyanja zote za maendeleo.
Kutengeneza mifumo imara kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
Wengi tunapenda maendeleo lakini hatupendi kulipia gharama za maendeleo! maendeleo kama hatua muhimu ya kuuaga umaskini ni matokeo ya jamii imara iliyokubali kuiishi misingi ya mifumo imara kiuchumi, kisiasa na kiuajibikaji. Ili kuondokana na adui umaskini ni muhimu kwa nchi kukubali kutengeneza na kuiishi mifumo imara ya kisiasa, kielimu na maisha kwa ujumla. Kamwe hatutaweza kumwondoa adui umaskini kwa kuwekeza kwenye vitu rahisi kama; udaku, umbea, habari za Simba na Yanga nk.
Kukabiliana na ubinafsi.
Ni muhimu sana kuwa na vipaumbele vya kitaifa. Tatizo la ubinafsi huleta utengano katika kukabiliana na adui umaskini. Ni jambo la kawaida kabisa Mtanzania kukimbilia Bandarini na TRA kwa ajili ya kwenda kupigania maslahi yake binafsi. Pia, ili kuleta jamii yenye usawa na kuondoa tatizo la umaskini ni muhimu kukawa na mgawanyo mzuri wa keki ya taifa na kupunguza makali ya umaskini. Na hili linawezekana kwa kuondoa mfumo wa kujuana, kamleteni, kamwambieni aje na kuhongana ili kupata nafasi ya kuhudumu serikalini. Mbali na kupunguza umaskini, kuondoa ubinafsi kutasaidia sana katika upatikanaji wa watumishi imara na mahiri waliokidhi vigezo.
Mwisho, kama mbinu ya jumla ya kukabiliana na adui umaskini, mwandishi anawaasa Watanzania wenye akili kujihusisha na siasa kwa sababu wakikwepa wajibu wa kujiingiza kwenye siasa wataongozwa na watu wenye akili ndogo. Watanzania lazima watambue hatma ya maisha yao na kesho yao ipo mikononi mwa watu wachache wanaoitwa wanasiasa. Hivyo, wasikwepe wajibu wa kujihusisha na siasa ili kutengeneza na kusimamia Sera, miongozo, kanuni na sheria nzuri zitakazokuwa nyenzo muhimu ya kupambana na adui umaskini.

Upvote
1