Namna ya kupata faida kubwa kwa wakulima wa green house !

Namna ya kupata faida kubwa kwa wakulima wa green house !

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
233
Reaction score
413
Habari wana jamvi Leo nakuja kwenu tena kueleza namna ambavyo Mkulima aliewekeza kwenye Kilimo cha kisasa kwa kutumia green house anavyoweza kupata faida
Naanza kwa kusema kuwa Kilimo ni Biashara kina hasara na faida zake na kama ilivyo kwa Biashara nyingine pale unapowekeza mtaji mkubwa na faida inakuwa kubwa pia provided there is Good management (usimamizi bora)

Teknolojia ya green house inakuja kwa kasi nzr na wakulima wengi wanahamasika lakini usipokuwa makini utaona Kilimo hiki ni kibaya na hakilipi kabsaa,

Nipende kuwakosoa wataalamu wengi wanaowapa wakulima hawa wa green house expectations kubwa kuliko uhalisia hasa wazee wangu wastaafu wamekuwa wakiambiwa oh Mara green house unaweza kukupa million mia (siku zote tupende kuuliza how?)

Naona nieleze sasa namna green house inanyoweza kukupa faida

Green house ni structure ambayo hukinga mazao na adhari za kimazingira kama mvua kubwa, upepo, jua Kali, wadudu n.k kwa sababu adhari hizi hufifisha ubora na ujazo wa mazao kwa hyo tunapolima ndani ya green house tuna kuwa na uhakika wa kupata mazao mengi na yenye ubora

1.Lima mazao ambayo ni ngumu kwa wakulima wa open field kulima (strawberry, lettuce, beetroots , courier flower , etc) hii itasaidia ww kupata bei nzr sokoni na kuongeza faida yako

2. Panda mazao ambao yana demand kubwa lakini Fanya kwa ubora zaidi na mazao haya yawe ya muda Mfupi mfano mzr ni Matango ambayo ndani ya siku 45 unavuma , panda Matango yako yatunze vzr yakiwa mazuri utaweza kuuza sehem kubwa kubwa kama supermarket na utapata faida nzr

3.Tengeneza calendar yako hasa kwa zao la nyanya, nyanya ni zao ambalo huadhiriwa sana na mvua kwa hyo wakati wa mvua kubwa nyanya huwa bei ghali sana na hapa ndipo pa kupigia pesa

Mfano panda nyanya yako mwezi wa 11 mwshoni mpka mwez wa 12 hudumia nyanya yako mpka mwezi wa pili katikati na hapo utaanza kuvuna mwez wa tatu mvua za masiki zikianza ww ndio unakuwa kwenye harvesting pick na utauza nyanya kama mfalme

Haya ni machache tuu lakini kuna njia nyingi ambazo Mkulima wa green house anaweza kupata faida kubwa

Unaweza kuongezea hapa namna nyingine zaidi
 
UKO POA SAAANA PIA WAAMBIE AIN ZA NYANYA KWA KIPINDI HIKO NI ZIPI ZINAFAA ILI WAUZE KWENYE SUPER MARKETS
 
Back
Top Bottom