Namna ya kupata mafanikio mwaka 2020

Sir josh

New Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
1
Reaction score
1
Mafanikio yoyote yale unayoyafahamu hapa ulimwenguni yalianza kama wazo na wazo huja baada ya kubadilisha mtazamo ili kufupisha mambo kila mmoja aendelee na mambo yake.

Basi niende kwenye point ya muhimu sana.

Mwaka 2015 nilianza kuwa na utambuzi wa kufuatilia vitu vinavyoendelea mtandaoni lakini jambo ambalo nilikuwa nalifurahia sana ilikuwa ni sikukuu za mwisho wa mwaka yaani Christmas na Mwaka Mpya ilikuwa kabla ya mwaka kuisha mchungaji anahubiri anasema huu mwaka ni wa kwetu, kama Mungu kakusahau mwaka jana basi huu mwaka ni wa kwako.

Kabla ya mwaka kuisha basi ni lazima jambo hili nilisikie. Niliendelea kuwa na Imani juu ya maneno ya mchungaji jambo ambalo ni zuri ila maisha yangu yakawa ni yale yale hayabadiliki jambo ambalo limenifanya nitulie nitafakari shida inakuwa wapi, wapi panakwamisha mikakati nikaja kugundua hili jambo.

Ukweli ni kwamba maneno ya mchungaji wako kanisani hayawezi kubadilisha hali yako ya maisha kiafya kiuchumi kiakili n.k bila kufanyia kazi sehemu hizo.

Kwa upande wetu sisi Wakristo kuna kijana mmoja anaitwa Jacob ambaye alipewa baraka na baba yake Isaka. Baraka zilifanya kazi pale ambapo Jacob alifanya kazi.

Inamaanisha kwamba ni lazima kuchukua hatua kwanza ili mwaka huu uwe mwaka wako huwezi ukawa ni mtu wa kukaa tu na kusema kwamba mchungaji alisema huu ni mwaka wangu. Biblia pia inasema asiyefanya kazi na asile.

Kwahiyo ushauri kwa ndugu zangu Wakristo, kama una mipango katika mwaka huu nakwambia kabisa maombi yako hayatoshi lazima ufanye kazi kwa bidii sana lazima utumie nguvu ya ziada kuweza kutimiza malengo yako ya mwaka 2020.

Naamini kila mmoja ana uwezo na nguvu pia ya kufanya kila kitu kiwezekane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…