Namna ya kupata uwezeshaji katika kilimo.

Namna ya kupata uwezeshaji katika kilimo.

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Habari ndugu watanzania,
natumaini munaendelea vyema na jitihada za ujenzi wa taifa letu hili changa kiuchumi,

nikiwa kama mtanzania kijana ninapambana kwa ustawi wa taifa langu na familia yangu naomba kuwashirikisha katika swala zima la kupata uwezeshwaji katika maswala ya kilimo hapa nchini.

kwasasa nina miliki takribani zaidi ya hekari 11 za shamba mkoani Tanga, na ninashukuru Mungu nimefanikiwa kuzitumia hekari 5 kwa kilimo cha mihogo kulingana na uwezo wangu, pia mazao mengine kama migomba, mipapai, miembe, mitiki, mnukanuka na mikorosho miwili mitatu.

dhumuni langu hasa nikulifanya shamba langu liwe la tija hasa katika uzalishaji.... eneo la shamba langu ni upande karibia na nchi ya jirani kenya ambapo ni rahisi kutumia soko la nchi hio jirani kwa mazao ya kibiashara kama italazimika ili kupata faida kubwa.

eneo la shamba hilo linaweza kustawi mazao mbali mbali ikiwa ni pamoja na machungwa, mikorosho, maembe, alizeti na mazao mengine yasiyohitaji hali ya hewa baridi.

hivyo naomba msaada wa taasisi ama shirika linalotoa msaada au mkopo katika uwezeshaji wa kilimo hapa nchini ili nipate kuendeleza shamba langu na liwe lenye tija. mimi ni mtu binafsi na si kampuni.

pia ikiwezekana endapo nikapata mtu binafsi ambaye nitaweza kufanya nae makubaliano vizuri tukafanya partnership nikotayari kwa hilo.

ninatumaini kupata ushirikiana wenu katika hili!
kila la heri.
kunipata zaidi unaweza ni PM.
 
Back
Top Bottom