Namna ya kupika bagia kwa haraka!

Namna ya kupika bagia kwa haraka!

Humble African

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
4,781
Reaction score
14,415
Mapishi ya Bagia dengu
Mahitaji
Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.

Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini.

Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Karibuni!!

Kind regards,
Humble african.
 
Mapishi Matamu ni blog ya kujifunza jinsi ya kupika mapishi mbalimbali ya kitanzania, mapishi ya kiswahili kama mapishi ya wali, Pilau, Biriani. Jinsi ya kupika mboga mbalimbali kama, mapishi ya kuku, samaki, maharage nakadhalika. Pia Mapishi matamu blog ina mapishi ya vitafunio mbalimbali kama, mapishi ya keki, maandazi, vitumbua, kachori nakadhalika.
Saturday, 28 August 2010
Mapishi ya Bagia dengu



Mahitaji

Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)
Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa. Karibuni!!

Kind regards,
Humble african.

Unauchoma unga wote kwa pamoja au unakuwa na kikaangio kama cha vitumbua vile halafu unakuwa unaweka unga kidogo kidogo katika kila kishimo cha kikaangio?
 
Hayo maji hapo pia ungeweka makisio km nusu kikombe au km kimoja ili mtu ajue pa kuanzia. Otherwise hapo kwenye uzito na wepesi panaweza kutucheza na nso mapishi yenyewe hapo au?
 
Hayo maji hapo pia ungeweka makisio km nusu kikombe au km kimoja ili mtu ajue pa kuanzia. Otherwise hapo kwenye uzito na wepesi panaweza kutucheza na nso mapishi yenyewe hapo au?
Na Mimi hapo ndio napasubiri, mtoa madaaaa, njoo huku bwana utupe ufafanuzi kidogo.
 
Hivi jamani dengu kwa lugha ya kizungu (English) ni nini? Ukiwa kwa wenzetu huwezi uliza dengu. Pia, hivi hamira (yeast) huwa haiwekwi kwenye dengu? Nauliza ili kujua maana kuna nyingine ukila ni kama zimeumuriwa vile na zinakuwa na uchachu fulani hivi!
 
Hivi jamani dengu kwa lugha ya kizungu (English) ni nini? Ukiwa kwa wenzetu huwezi uliza dengu. Pia, hivi hamira (yeast) huwa haiwekwi kwenye dengu? Nauliza ili kujua maana kuna nyingine ukila ni kama zimeumuriwa vile na zinakuwa na
uchachu fulani hivi!

Unga wa dengu ni chickpea flour au gram flour
 
Hivi jamani dengu kwa lugha ya kizungu (English) ni nini? Ukiwa kwa wenzetu huwezi uliza dengu. Pia, hivi hamira (yeast) huwa haiwekwi kwenye dengu? Nauliza ili kujua maana kuna nyingine ukila ni kama zimeumuriwa vile na zinakuwa na uchachu fulani hivi!
nijuavyo mie hamira unaweka wakati unataka anza pika maana ukiweka wakati unachanganya vitu huwa bagia zinaharibika. Na pia unaweza weka kotmiri kwa ladha zaidi!!!
 
Kuna dogo anazipenda hizi hatari, nimezimiss, ngoja kesho nizipike.
 
Back
Top Bottom