Namna ya kusajiri Website hapa Tanzania

gumya

Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
92
Reaction score
28
Habari,kwanza kabisa Heri ya chrismas na mwaka mpya 2017 kwa wote.Kwa wale wenye kumiliki Website zilizosajiriwa au yeyote mwenye uelewa juu ya namna ya kusajiri website hapa tanzania naomba kujuzwa hatua kwa hatua namna ya kufanya ili kusajiriwa.
Hapa nazungumzia website zinazotoa huduma za bure na zakulipia kama vile KUPATANA.COM,kwa mfano mimi nahitaji jina la biashara liwe "wanaJF Ltd" halafu website yake na ambayo ndo itakua inatoa huduma iwe "wanajf.com".
Je,hapo ni hatua zipi natakiwa kuzifuata ili kukamilisha usajiri na itanigharimu kiasi gani?
Je,kwa usajiri huo naweza kuongoza website hiyo mwenyewe au masharti ya usajiri yatalazimisha waongozaji wa website hiyo wawe zaidi ya mmoja? Asanteni na karibuni.
 
Kumikiki website unatakiwa jufuata hizi hatua
1. Sajili jina mfano wanajf.com ni bure ukihosti kwetu
2. Lipia hosting bei ya kuanzia ni 70,600/mwaka hii ni pamoja na domain name
3. Utapewa control panel ya kwako ambayo utatumia kusimamia website yako. Inaruhusu pia mtu zaidi ya mmoja kusimamia website
4. Tayari umemiliki website
Tembelea kwa ma elekezo zaidi
https://webmaster.co.tz,
 
Asante mkuu,Lakini utakua hukuelewa lengo la uzi wangu.Nachotaka kujua ni kwamba tayari una website yako sasa kama hiyo WEBMASTER.CO.TZ ulifata taratibu zipi kuisajiri kwa serikali ya nchi hii?
 
Asante mkuu,Lakini utakua hukuelewa lengo la uzi wangu.Nachotaka kujua ni kwamba tayari una website yako sasa kama hiyo WEBMASTER.CO.TZ ulifata taratibu zipi kuisajiri kwa serikali ya nchi hii?
Wasiliana na hawa watakupa muongozo https://www.tznic.or.tz/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…