Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,683
Mahitaji:
Jinsi ya kutayarisha:

Jinsi ya kutenganisha kiini cha yai kutoka kwenye ute wa yai:

- Mayai 8
- 250g sukari
- 300g lozi zilizosagwa tumia blender kusaga na machine ya kusagia viungo
- Kijiko kimoja cha chai cha mdalasini ulosagwa
- Vanila kijiko kimoja cha chai
- Maganda ya limau na chungwa yalosagwa
- Icing sugar
Jinsi ya kutayarisha:
- Tenganisha viini vyai kutoka kwenye weupe wa yai.
- Piga weupe wa yai mpaka ukazane.
- Tumia bakuli jingine kupiga viini vya yai,sukari na vanilla
- Changanya mdalasini,maganda ya limau na chungwa pamoja na lozi
- Mwisho changanya mchanganyiko wako na weupe wa yai uloupiga fanya kama unafold in taratibu usikoroge kwa nguvu.
- Tumia bati la keki la mduara size ya kati lipake siagi kabla hujaweka mchanganyiko wako
- Choma keki yako kwenye 175 degrees kwa muda wa dakika 45
- Keki ikishapoa nyunyuizia Icing sugar juu.

Jinsi ya kutenganisha kiini cha yai kutoka kwenye ute wa yai:
- Unahitaji mabakuli mawili moja la kuwekea viini na jingine ute wa yaivunja yai
- Vunja yai,weka bakuli chini ya yai ukiliwa unalitenganisha weka kiini cha yai kwenye ganda moja wapo na fanya kama unalichuja ili ute umwagikie kwenye bakuli na unaweza kulipokeza kwenye ganda la pili mpaka ute wote umwagikie bakulini
- Weka kiini cha yai kwenye bakuli jingine.
- Njia nyingine ni kutumia mikono.Unavunja yai kisha unatenganisha kiini na ute kwa kutumia mikono yako.

