Namna ya kutoa utetezi thabiti uwapo kizimbani

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Mimi sio mwanasheria, wala sikubahatika kusomea taaluma ya sheria, kwa taaluma mimi ni mhandisi wa umeme na kompyuta, lakini uzoefu wangu wakujisomea machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu vya sheria, nimeweza kufahamu haya machache katika uga wa kujitetea uwapo mbele ya mtoa roho kwa mbeleko ya Pilato.

( 1 ) Kama unahojiwa na Wakili mahakamani usijibu bila kutafakari alichokuuliza.

( 2 ) Wakili asikuogopeshe kwa ukali anapokuuliza kwani ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha ulichopanga kusema.

( 3 ) Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu.

( 4 ) Penda sana kujiamini kwakuwa kujiamini hupunguza uwezo wa Yule anayekuuliza, hata awe Jaji/Hakimu.

( 5 ) Jitahidi kupata ushauri wa wanaojua sheria kwa kila hatua unayopiga katika kesi.

( 6 )Kama we ni shahidi hakikisha unajadiliana vya kutosha na Yule unayemtolea ushahidi kabla hamjaingia mahakamani.

( 7 )Usipaniki kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa ,kejeli, au tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa la kuidharau mahakama.

( 8 )Katika kesi ya jinai usikubali kosa haraka kabla hujajua kitaalam kosa hilo linaundwa na nini(vipengele vya kosa).

( 9 )Kama hukuelewa vizuri kosa ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwakuwa ukikaa kimya unaandikiwa umekataa kosa.

( 10 )Kanuni ya sheria ni kuwa, Ni kazi ya aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa na si kazi yako kuthibitisha kuwa haujatenda kosa.

( 11 )Katika kesi ya jinai msikilize kwa makini anayekushitaki na hakikisha unapata lolote lenye kutia shaka katika maelezo yake na iambie mahakama shaka hilo hii ni kwasababu huwezi kuwa na hatia kama kuna shaka katika maelezo.

(12)Kama ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahakama kuwa ulitenda kosa ukijilinda(self defence) inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa.

( 13 )Kama ndugu yako hana akili tinmamu na ametenda kosa iambie mahakama.Hii ni kwasababu kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya wasio na akili.

( 14 )Inakubalika na ukaachiwa huru ukisema kuwa ulilazimishwa kutenda kosa kama kweli ulilazimishwa.

( 15 ) )Inakubalika na ukaachiwa huru kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati likitokea kama kweli haukuwapo.

( 16 )Kama kosa ni kupita taa nyekundu ikiwaka barabarani,swali lako kwa shahidi traffic lilenge kumbana kama sehemu aliyokuwa amesimama alikuwa na uwezo wa kuangalia vizuri na kutambua rangi za taa. Mfn. jua kali linawaka yeye ameuonaje mwanga wa taa kutoka mbali.

( 17 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi muhoji maswali mafupi. Mfn. ulikaa upande wa pili barabara, si ndio, jua kali lilikuwa linawaka , si ndio, ulifanya kazi ya kuangalia magari mengine pia si ndio, na mbele kulikuwa na miti si ndio, sasa kama hali ilikuwa hivyo uliwezaje kuona taa nyekundu ikiwaka wakati nakatiza.

18 )Ukipewa nafasi ya kumhoji shahidi wako uliyemleta katu usimuulize swali ambalo mlikuwa hamjalijadili na hivyo hujui atatoa jibu gani.

( 19 ) Kama wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa kuna kipindi aliwahi kuchangnyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu kabla, ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake mpaka aaminike kwa anayoyatolea ushahidi leo.


"Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao"
 
please, Mh. msomi sana Yeriko, naomba unisaidie document ya power of attorney
 
Nini tofauti ya ushahidi chini ya kiapo na ushahidi bila ya kiapo...picha mnato au video zinakubalika kama ushahidi mahakamani....yaani nilinunua shamba na kwa bahati nikawa nachukuwa video ya vikao vyote mpaka kuoneshana mipaka ya shamba tukiwa na wazee wa ukoo,lakini baada ya muda nikashitakiwa kwa kuvamia shamba
 
Ushahidi chini yakiapo huwa unaaminika mahakamani na shahidi akitoa ushahidi KWA kiapo huwa anawajibika kujibu maswali. Ushahidi bila ya kiapo ni kinyume ya huo hapo wa kiapo.

Kwa faida ya msomaji, kuna makundi mawili tu ambayo yanaweza kutoa ushahidi bila ya kiapo
1. Mtoto chini ya miaka 14 ambaye hajui maana ya kiapo.

2. Mshitakiwa halazimishwi kutoa ushahidi kwa kiapo hivyo anaweza kutoa Maelezo yake bila ya kiapo
 
Shukran mwanajf mwenzetu yericko nyerere!
 
asante sana kwa maelezo yako mazuri na uhakika yana msaada mkubwa sana kwa wanajamiiforum..keep it up kazi nzuri sana
 
Jf katika ubora wake.. Nimepata abc za sheria hapa.,asante Yericko
 
jaman hii thread iko poa sana vp kuhusu kuhojiwa na polisi maana unahojiwahuku ukila kichapo mwisho unakubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…