Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
Ni wazi kuwa kwa sasa kuna tatizo kubwa la ajira nchini. Ni jambo la kawaida kabisa Watu 1000 kugombea nafasi tano za kazi. Rejea Ajira za Elimu na Aya zilizotolewa na Tamisemi mwaka Huu 2021.
Pamoja na changamoto nyingi za Kujiajiri lakini tunaweza kuanza taratibu hatimaye Kujiajiri kupitia Vipaji, taaluma au ujuzi tulionao.
Kila mtu ana jambo hapa angalau moja na kila mtu hutamani kitu hicho kiwe chanzo cha kipato, wengine hutamani kipaji chao kifikie watu wengi zaidi na kuanza kulipwa au ujuzi au taaluma zao ziwalipe.
_
Kila mtu ana kipaji, wachache wamegundua vipaji vyao na wachache zaidi vipaji vyao vinawalipa na kuwapa mafanikio makubwa.
Wenye ujuzi pia hawajui namna wanavyoweza kulipwa. Ndo maana utaona mtu anakwambia nina uwezo mzuri wa kuongea mbele ya watu lakini mtu huyo hajawahi kulipwa ata senti. Au una uwezo wa Kutangaza, kuendesha shughuli, kuchora, kucheza na ala za muziki nk.
Wenye taaluma hawa ni wengi hasa wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati ambao hawawezi kugeuza taaluma zao kuwa ajira mpaka waajiriwe, wakikosa ajira basi watakaa kulaumu serikali, wazazi na waalimu.
Kuna hatua tatu ambazo unaweza kupitia mpaka kuanza kulipwa kupitia hicho ulichonacho.
Wewe unajua nini unacho, lakini wengine hawajui, Ili watu wakujue inapaswa uwaonyeshe, na Kwakua hawakujui unapaswa kuomba nafasi.
Hatua hii inakufanya uombe kuonyesha kipaji kwa watu bure, wakati mwingine unalipia ili uonyeshe ulichonacho watu wakujue.
Kwenye Ajira rasmi hii ni kama kuomba nafasi ya kazi kujitolea bila malipo.
wakati mwingine kwenye hatua hii unaweza kupewa pesa kidogo ya nauli.
Huu ni wakati mzuri zaidi wa kujitangaza, kuonyesha nini ulichonacho na kuongeza thamani yako.
Huwezi kulipwa wakati watu hawajajua thamani yako, hawajajua uwezo wako.
Kwani wewe unaweza kukubali kunyolewa na Kinyozi ambaye hajawahi kunyoa sehemu yoyote na ukamlipa pesa nyingi?
Au kufanyiwa upasuaji na Daktari ambaye hajawahi fanya upasuaji ata kwa usaidizi?
Mara nyingi watu hupenda kulipwa kabla hawajaonyesha thamani na kuaminika, matokeo yake hushindwa kupenya kwenye soko la Taaluma, ujuzi au vipaji vyao.
Baada ya Kupitia Hatua hizo Hapo juu sasa kuna
mambo ya kuzingatia ili ulipwe.
a) . Zingatia Ubora.
Unapoamua kuajiriwa au kujiajiri fahamu kuwa unakuwa kama bidhaa sokoni.
Sokoni bidhaa zipo nyingi tena zinazofanana kwa muonekano wa nje, jiulize unapokuta bidhaa zinazofanana kitu gani kinakupa maamuzi ya kuchagua moja kati ya nyingi?
Saikolojia inaonyesha wanunuzi huangalia kwanza ubora wa bidhaa kabla ya kuuliza bei na mambo mengine.
Pia wanunuzi wako tayari kulipa gharama zaidi kwa kitu kilicho bora.
Hivyo kama unataka kujiuza vizuri sokoni ni lazima kwanza uwe bora, Wengi wanataka tenda, wengi wanataka kuonekana, wanataka ajira kama wewe lakini nini cha ziada ulichonacho, Ubora gani unao kuzidi wengine, faida gani unazitoa kuzidi wengine.
Kabla mtu hajakupa nafasi anajiuliza hivi huyu atakidhi haja yangu, atatoa thamani?
Kabla hujalalamika hupati nafasi, kwanza jitathmini ubora na ufanisi wako.
b) Jitangaze.
Ukishakuwa bora fuata hatua ya pili ya kujitangaza, Tumia platform zako zote mtaani, ofisini, kanisani, Jamii Forum, linkedlin nstagram Facebook nk.
Wewe ni bidhaa kabla mtu hajakupa nafasi uwe na uhakika anakufatilia ili kujiridhisha kwanza.
Weka nguvu kwenye kujiuza(Kuuza ulichonacho) , unavyojiuza ndivyo unavyonunulika.
Watu hawawezi kukupa nafasi wakati hawajui ulichonacho. Ili wajue nini ulichonacho unapaswa kuwaonyesha.
Unawaonyesha kwa kujitangaza. Huwezi kujua na kupata mteja au mtu wa kukushika mkono kama hujajitangaza.
Kelvin Kibenje
0762815104
Pamoja na changamoto nyingi za Kujiajiri lakini tunaweza kuanza taratibu hatimaye Kujiajiri kupitia Vipaji, taaluma au ujuzi tulionao.
Kipaji (Talent)
Kipaji ni uwezo wa asili alio nao mtu wa kufanya jambo fulani kwa namna ya kipekee.Ujuzi (Skills)
Ni uwezo wa kufanya jambo kwa ufanisi.
Taaluma ( professional)
Ni elimu uliyoisomea au uliopata sehemu fulani.Kila mtu ana jambo hapa angalau moja na kila mtu hutamani kitu hicho kiwe chanzo cha kipato, wengine hutamani kipaji chao kifikie watu wengi zaidi na kuanza kulipwa au ujuzi au taaluma zao ziwalipe.
_
Kila mtu ana kipaji, wachache wamegundua vipaji vyao na wachache zaidi vipaji vyao vinawalipa na kuwapa mafanikio makubwa.
Wenye ujuzi pia hawajui namna wanavyoweza kulipwa. Ndo maana utaona mtu anakwambia nina uwezo mzuri wa kuongea mbele ya watu lakini mtu huyo hajawahi kulipwa ata senti. Au una uwezo wa Kutangaza, kuendesha shughuli, kuchora, kucheza na ala za muziki nk.
Wenye taaluma hawa ni wengi hasa wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati ambao hawawezi kugeuza taaluma zao kuwa ajira mpaka waajiriwe, wakikosa ajira basi watakaa kulaumu serikali, wazazi na waalimu.
Kuna hatua tatu ambazo unaweza kupitia mpaka kuanza kulipwa kupitia hicho ulichonacho.
1. Kuomba nafasi ya kuonyesha uwezo wako.
Wewe unajua nini unacho, lakini wengine hawajui, Ili watu wakujue inapaswa uwaonyeshe, na Kwakua hawakujui unapaswa kuomba nafasi.
Hatua hii inakufanya uombe kuonyesha kipaji kwa watu bure, wakati mwingine unalipia ili uonyeshe ulichonacho watu wakujue.
Kwenye Ajira rasmi hii ni kama kuomba nafasi ya kazi kujitolea bila malipo.
2. Kupewa nafasi ili ufanye bure.
Katika hatua hii watu wanakua tayari wameanza kujua nini ambacho unafanya. Hatua hii haulipwi sababu watu wanakua hawajakuamini bado.wakati mwingine kwenye hatua hii unaweza kupewa pesa kidogo ya nauli.
Huu ni wakati mzuri zaidi wa kujitangaza, kuonyesha nini ulichonacho na kuongeza thamani yako.
3. Kulipwa.
Baada ya watu kukujua na kukuamini hapo wanakua tayari kukulipa.Huwezi kulipwa wakati watu hawajajua thamani yako, hawajajua uwezo wako.

Upvote
2