Procedure za kupitia law school ni kuwa ukishamaliza degree ya sheria unafanya application law school kwa course inayoitwa Postgraduate Diploma in Legal Practice.
Course inatumia muda wa miezi 7,ambayo miezi minne unakuwa darasani na miezi mitatu unakuwa field,ukimaliza law school na kufaulu masomo yote then law school watapeleka jina lako kwenye Council for Legal Education ambao watalifikisha kwa Chief Justice,utatakiwa uandike Petition kwa Chief Justice ikiambatana na Certificate of Character then petition yako ikipita jina lako litatoka gazetini ili kama kuna mtu ana pingamizi usiapishwe aweze kulitoa.Kama hakuna pingamizi dhidi yako utapangiwa siku ya kufanyiwa a short interview na Chief Justice then utasubiri siku ya kuapishwa.