Blue Icon Consultancy
Member
- Sep 11, 2020
- 9
- 8
Soko la Wafadhili (The market of potential donors) kwa Taasisi zinazofanya vizuri katika maeneo yao ya kiutendaji ni kubwa. Ili kuwa na ufanisi katika kuliendea soko hili; Taasisi inapaswa kuligawa (market segmenting). Namna rahisi kwa Taasisi kugawa soko la Wafadhili ni kama ifuatavyo;
- Soko la Wafadhili wenye kutoa msaada wa kifedha (The market for cash donations). Kimsingi; kundi hili hujumuisha wafuatao; (a) Matajiri wenye uwezo wa kutoa kiasi kikubwa cha fedha (b) Watu wa kipato cha kati ambao hutoa kiasi cha wastani; mara nyingi utoaji wa watu hawa huwa ni kupitia ada za uwanachama wa Taasisi husika n.k (c) Watu wa Kipato cha Chini; mara nyingi kundi hili hutoa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya miradi ya Taasisi, na hutoa pindi wanapoguswa na tatizo linaloenda kushughulikiwa na Taasisi husika.
- Soko la Wafadhili Wenye Kutoa Msaada kwa njia ya Kujitolea (The market for volunteers) Kundi hili hujumuisha; (a) Kundi la Wanafunzi katika Kada Fulani ; kwa mfano wanafunzi wanaosomea UDAKTARI. Watu hawa huweza kutoa huduma kwa wagonjwa waishio na virusi vya Ukimwi na HIV wanaohudumiwa na Mradi utekelezwao na Taasisi yako. Kimsingi watu hawa wanaweza wasihitaji malipo ya aina yoyote, isipokuwa kutoa kwao huduma; huwaongezea UZOEFU, pia huweza kuwaongezea alama katika masomo yao ya vitendo. (b) Wastaafu katika Taaluma Fulani (Retirees with professional skills) Taasisi inaweza kuwatumia wastaafu hawa kama washauri (pro bono consultants) katika Mradi unaotekelezwa na Taasisi yako, ushauri wao utaweza kukuwezesha kutekeleza Mradi wako kikamilifu na kupata matokeo unayotarajia. (c) Kundi la watu wenye juzi mbalimbali ambao huweza kusaidia katika shughuli za Utawala kwenye Taasisi yako kipindi cha utekelezaji wa Mradi.
- Soko la Wafadhili kutoka Mashirika ya Kibiashara (Corporate Donors) Kundi hili huweza kutoa msaada wa vifaa, nyenzo pia hata fedha kwa ajili ya Miradi inayotekelezwa na Taasisi za Kiraia. Katika kuyaendea haya mashirika; ni vyema ukatenganisha mashirika ambayo shughuli zao zinaendana na shughuli za Taasisi yako (companies whose businesses somehow relate to your NGO) na yale mashirika ambayo shughuli zao haziendani na shughuli za Taasisi yako. Kutenganisha huku kutakusaidia kutofautisha mbinu (strategies) kwenye "fundraising activity" . Ni vyema sana ukaanza kujikita na mashirika ambayo yapo jirani na mahala ambapo Taasisi yako ipo/mradi unapofanyika; kwa mfano Taasisi ambazo zipo kwenye maeneo ambayo kuna uchimbaji wa madini, huweza kuanza na Kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji madini katika kuomba ufadhili kwa ajili ya Miradi yao.
- Soko la Makundi ya Kijamii (Community clubs and associations) Kundi hili linaweza kutoa ufadhili kwa kuendesha mfano; tukio la utoaji (charity event) na mapato yatakayopatikana moja kwa moja yataelekezwa kwenye Mradi unaotekelezwa na Taasisi yako.
Taasisi pia inapaswa kufahamu kwamba wafadhili hawatoi fedha kwa sababu tu wameguswa na Mradi wako (cause) ni lazima ufahamu "motivation" zinazowasukuma wafadhili (potential donors) kutoa fedha kwa ajili ya Miradi, kama ilivyo ni muhimu kwa Afisa Masoko kufahamu ladha na kipaumbele cha mteja wake (taste and preferences of customer). Mashirika mbalimbali ya Kibiashara hupenda kutoa ufadhili kwa Miradi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wao na jamii (public relations) hivyo unapowafuata kuwaomba ufadhili; ni vyema ukawaonyesha; watakapokufadhili ni kwa namna gani wataweza "ku-strengthen their public relations"
Mashirika mengine huweza kutoa ufadhili kwa Taasisi yako ili tu waweze kuwafikia wanufaika wa Mradi wako (end recipients). kwa mfano; unapoomba ufadhili kwa Taasisi ya Kifedha kama benki kwa ajili ya kufadhili mradi wa Ujasiriamali kwa Wanawake, wao watakachoangalia ni kwa namna gani watanufaika na hawa akina mama (ambao ni wanufaika wa Mradi) mfano kwa wao kuja kufungua ACCOUNTS zao kwenye benki husika, kuja kuwa wateja wa mikopo itolewayo na benki husika n.k
Nimalizie tu kwa kusema kwamba; Taasisi ambayo kwanza itawatenga wafadhili kutokana na makundi yao kama nilivyoainisha hapo juu kisha ikajua "motivation" ya kila mfadhili kabla ya kuanza mchakato wa "fundraising" itakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa katika mchakato wake wa harambee.
Ahsante
Blue Icon Consultancy
+255 719 518 367
Dar es Salaam