SoC01 Namna ya kuweza kutunza mshahara wako ukutane na wa mwezi unaofuata

SoC01 Namna ya kuweza kutunza mshahara wako ukutane na wa mwezi unaofuata

Stories of Change - 2021 Competition

Chishako1994

Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
7
Reaction score
8
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya mishahara ya waajiriwa wengi kutokutana yaani mishahara kuwahi kuisha kabla ya muda wa kupokea mshahara mwingine. Hii hupelekea walio wengi kuamua kuzidharau kazi za kuajiriwa na kudai mishahara iongezwe bila kufikiria kuwa hata wenye mishahara mikubwa zaidi yao pia wanalalamikia suala hilo hilo.

Sababu zinazopelekea kuisha kwa mishahara kabla ya mwezi kuisha ni;
1. Mahitaji mengi kuliko kipato chako
2. Kuwa tegemezi kwa watu wengi
3. Kutokuwa na chanzo kingine Cha kukuwezeshea kipato
4. Kutokuwa na bajeti ya kueleweka

Kwahiyo, kutokana na kutozijua sababu Kama hizo waajiriwa wengi huanza kuzichukia kazi za kusubiria mshahara mwisho wa mwezi na kuamua kujiajiri wenyewe.

Hivyo basi, fanya yafuatayo ili uweze kubaki na mshahara wako mpaka mwezi uishe
1. Punguza utegemezi kutoka kwa watu wengi. Hapa watu wengi hasa ukiajiriwa unaonekana ndio una hela kuliko watu wengine katika familia, hivyo huna budi kupunguza wanaokutegemea ubaki na wake wa lazima kama vile mke na watoto pamoja na kushirikiana na ndugu wengine kuwatunza wazazi wenu na sio wewe pekeyako.

2. Panga bajeti ya matumuzi yako ya lazima kabla ya kuupokea mshahara ili uepishe matumizi yaliyi nje ya bajeti.
3. Tafuta namna nyingine ya kipato tofauti na mshahara wako, mfano kama una mke au mme mfungulie hata genge la matunda,atakusaidia hata katika masuala ya nauli na chakula. Au Kama una nafasi ya kufuga wanyama na ndege fanya ivo.
4. Kubali kuwa mtu wa kawaida sana, hapa unatakiwa kuepuka kuiga maisha ya watu wengine, wewe ishi kawaida tu.

Kwa kuhitimisha ningependa kutoa ushauri kwa waajiriwa wenzangu kuwa hatuna budi kujituma sehemu zetu za kazi na kujiongezea sifa nzuri kwa watu maana hujui kesho yako itakuwaje, huenda ukapandishwa cheo, au sifa zako zikawavutia wengine kukuhitaji na kukupandishia mshahara.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom