Namna ya kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa binti

Namna ya kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa binti

Mr.creative

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2011
Posts
492
Reaction score
117
nataka nikajitambulishe nipeni kwanza vitu viwili cha kwanza kuna madhara yoyote ya kufanya hivyo ?pia je mchakato unaanzaje? ni hayo to great thinkers
 
Inategemea na kabila gani unako kwenda kujitambulisha,wengine hawana mila hizo za kujitambulisha tusubiri wana JF watupe majibuzzz...
 
Muuulize huyo mtarajiwa wako, yeye ndiye anayetakiwa kukupa taratibu za mila zao, anachotakiwa ni yeye kuwa kiongozi wako, kama na yeye kakulia mjini hajui mila za kwao, basi tafuta mzee wa kabila la mtarajiwa wako, atakupa darasa na kisha uanzie hapo. nadhani hii itakusaidia.
 
Andaa mahela na ng'ombe hasa kama binti ni mweupe, kamaliza la saba, mnene, meno meupe afu ana mwanya.

mengine ni mbwembwe.
 
nataka nikajitambulishe nipeni kwanza vitu viwili cha kwanza kuna madhara yoyote ya kufanya hivyo ?pia je mchakato unaanzaje? ni hayo to great thinkers

Mkuu unavyosema madhara kwani ni mwanafunzi au under 18?
 
Wakileta mbwembwe za mahari kubwa piga mimba waambie kama vp wamtunze mtoto au wakuachie kimyakimya
 
Kujitambulisha kwa wazazi wa binti ina maana ifuatayo:

1. Unapeleka posa rasmi kwa wazazi wa binti kuwa unamchumbia binti yao na siku si nyingi utafunga naye ndoa
2. Kujitambulisha na kupeleka posa rasmi unatangaza kwamba sasa umeji-commit kwa huyo binti na utatambuliwa rasmi na familia pamoja na ukoo mzima wa upande wa binti.
Kujitambulisha kunaambatana na kupangiwa mahari (kulingana na taratibu za kabila husika)
3. Ukishapangiwa mahari utatoa sehemu ya hiyo mahari au yote siku hiyohiyo (kutegemeana na taratibu zao), unatakiwa kufanya homework kabla hujaenda ili kujua mahari ikoje au inahusisha mambo/vitu gani.

Mambo muhimu ya kuzingatia:

1. Usiende wewe peke yako au vijana wa rika yakeo pekee
2. Unatakiwa uende na mzazi wako au mzazi mlezi au mwakilishi wa mzazi wako ambaye ana umri sawa na baba yako mzazi atakayekuwa mzungumzaji kwa niaba yako, wewe utatambulishwa kwa wazazi wa binti na huyo mzazi wako. Pia andaa mtu mwingine atayekuwa mshenga wako, atakayekuwa anawasiliana na familia ya binti pale kutakapokuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
3. Kujitambulisha ni tukio kubwa kwa upande wa wazazi wa binti, hivyo usiende kwa kushtukiza, mwambie binti awaambie wazazi wake kuwa kuna ugeni muhimu unakuja siku fulani kwa shughuli fulani (kadri utakavyokuwa umepanga), maana familia nzima, ndugu na ukoo wa binti utajiandaa kuwapokea, hakikisha unaenda siku hiyo.
4. Fanya homework yako mapema ya mahitaji muhimu yanayotakiwa kwa shughuli husika (kama vile barua ya uchumba, ama anakabidhiwa binti mapema ili apeleke kwa wazazi wake) siku kadhaa kabla haujaenda.

N.K.
 
Thank u mr. ngereja! kumbe ni jambo kubwa sana unaweza ukakurupuka aksante sana aise
 
Muulize mchumba wako,kila makabila wana taratibu zao,wakristo unatakiwa uje na barua ya kutoka kwa mchungaji unakoabudu.
 
Back
Top Bottom