Namna ya uvaaji wa mwanaume kwenye mazingira rasmi

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Kumekuwa na uvaaji holela wa mavazi ya wanaume na wanawake. Ila naomba kujua haya kwa wanaume
1. Mkanda huwa utapita kulia kutokea kushoto au kushoto kutokea kulia

2. Shati/tshirt- urefu wa mikono unapaswa kuishia robo ya mkono wa juu (robo, nusu au kumaliza kigimbi ) na kuna wanaovaa shati imebanwa mbavuni inaunda shepu kama za kike ni sahihi au ni alama mbaya

3. Saa inavaliwa mkono gani kulia au kushoto?

4. Kunyoa: anapaswa kunyoa pank, kawaida kama mwanafunzi au kiduku kama cha lissu

5. Tai: urefu wa tai inatakiwa ifike kwenye mkanda, ivuke au iishie nusu y shati yaani kwenye tumbo

6. Koti: urefu wa mikono uzibe mikono ya shati au miishilizo ya shati ionekane kidogo

7. Suruali- inafaa modal, kuacha mwili, ibane chini juu pana au kama sandawili (juu mpaka chini upana unaendana). Iwe na pindo chini au isiwe na pindo

Mengine wadau wataongezea, tumejisahau sana kwenye uvaaji hadi kwa waheshimiwa wabunge na mawaziri
Picha kwa hisani ya google pictures kwa reference tu
 

Attachments

  • images.jpeg
    33.7 KB · Views: 7
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…