Nampa maua yake ndugu Odero C Odero kutokana na mdahalo wa jana kwa nafasi ya mwenyekiti CHADEMA

Nampa maua yake ndugu Odero C Odero kutokana na mdahalo wa jana kwa nafasi ya mwenyekiti CHADEMA

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Jana usiku kulikuwa na mdahalo kwa wagombea wa Uenyekiti wa CHADEMA Taifa ili kunadi sera zao na wapiga kura kuwapima kama wanatosha kushika nafasi hiyo. Katika mdahalo huo mgombea muhimu sana allingia mitini kwa sababu anazozifahamu yeye.

Nipende kumpongeza Ndugu Odero kwa ujasiri aliokuwa nao na uwezo wa kupanga meneno yaliyowafanya wasikilizaji kukubali kwa asilimia 100 sera zake. Kwa kweli Ndugu Odero alijipanga vema kwa mdahalo huo.

Nipende kushauri kuwa kwa yeyote atakayechaguliwa kwa nafasi ya Mwenyekiti kama Ndugu Odero hatachaguliwa basi huyo Mwenyekiti amjumuishe katika nafasi ya juu katika Chama. N

dugu Odero ni asset katika CHADEMA. Ndugu Odero kama msikilizaji napenda nikupe maua yako kwa kazi nzuri uliyoonyesha jana.
 
Naunga mkono hoja,
Yani kama sio ishu ya upepo na nyota ya Lissu basi huyo mzee ni hazina kubwa kwa chama na Taifa ana uwezo mkubwa wa kufikiri na nikiongozi hasa.
 
Back
Top Bottom