Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,501
Jamani naombeni ushauri wa dhati katika hili, ni jambo langu mwenyewe. Kuna mdada nampenda sana na nina mwaka mmoja tupo katika mapenzi. Mara kwa mara amekuwa akinishutumu kuwa eti bibi zangu wanamsumbua na nikimwambia anitajie huyo anayemsumbua amekuwa hasemi. Mimi najijua fika kuwa sina mwanamke mwingine ambaye niko committed naye wa kuweza kufikia hatua ya kumsumbua. Nimemvumilia najua labda ni mapenzi tu. Wiki mbili zilizopita alinipigia simu akiniuliza nimwambie kama kweli nampenda kwa dhati ili asijilaumu na maamuzi yake. Nikamwambia ni kweli nampenda kwa dhati. Akasema anashukuru kwa jibu langu maana kuna mtu anamsumbua. Nikamuuliza nani anamsumbua na kwa kipi anachomsumbua, hakuniambia na akazima simu na kupotea kama siku tatu nne bila kupatikana. Kwa sasa nimekaa kimya natafakari na sijui nimuelewe vipi. naomba mnisaidie kama ni mwanamke anayenifaa kweli au la. Nisaidieni tafadhali ukweli ni kwamba ninampenda sana ingawa nashindwa kumuelewa na bahati mbaya sana tuko mikoa tofauti kwa sasa