Nampongeza Dkt. Bashiru Ally lakini...

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Nampongeza sana Dr Bashiru Ally, Ambassador kuteuliwa kuwa Chief Secretary. Ila nina reservations mbili tu.

Moja, hana uzoefu mkubwa katika ku-run Goverment machinnery, ukifikiria kuwa asili yake ni mwalimu UDSM. Na hajawahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara yoyote ya serikali. Hilo ni moja.

Pili, ukitaka kumuondoa mtu sehemu mpaishe aende juu.

Pale CCM akiwa Katibu Mkuu alianza kuweka mambo sawa ila sijui kama kisiasa alikuwa ana rhyme na misimamo tunayoiona.
Misimamo ya Bashiru ilikuwa ya kisomi.

Je, CCM itaendelea kuwa vipi?

Maoni pls.
 
Awamu hii watu wanateuliwa kwa misingi ya uchama! Vyeo ambavyo vilistahili kupewa watu ambao wamefanya vizuri katika idara mbalimbali za serikali, wanazawadiwa makada wa chama.

Huu utaratibu wa kuirudisha Nchi miaka ya 1970's, 1980's, haukubaliki hata kidogo.
 
Kuendesha serikali si mchezo.

Bashiru atapata shida kuelewa procedures, checks and balances katika kudhibiti utendaji wa technocrats.
 
Katibu mkuu kiongozi inataka mtu mwenye experience kubwa mwenye kujua taratibu mbalimbali za kuendesha nchi.

Watu ambao washapita idara mbalimbali za serekali na kujua jinsi serekali inavyoendeshwa.

Bashiru katoka UDSM kaja chamani sasa gafla KMK
 
Aweke mwenye experince na mwenye kufuata taratibu za kiutumishi na serekali ili AHOJIWE KILA ANALOFANYA?
 
Hiyo reservation namba mbili haipo clear.
 
Mlitaka apewe nani ili muache maneno ya kwamba fulani hafai au hatoshi kwenye nafasi hii?

**Akizungumza baada ya kula kiapo, ameeleza kuwa kwa maadili na utamaduni, kazi za Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi sio kazi za maneno bali ni za kusikiliza, kujifunza na kuchambua, kuamua na kutenda
-
Amesema, "Wale waliotegemea kwamba nitazungumza tena kwa kweli nitazungumza kwa tahadhari na umakini kwasababu kiapo mmekisikia. Ni Katiba, Sheria, taratibu, mila, desturi"
-
Aidha, amezungumzia suala la umuhimu wa mawasiliano ndani ya Serikali na kati ya Serikali na Umma akisema watasimamia hilo**

Maneno ya Bashiru hayo....anaenda kujifunza kazi
 
Tulishasema kitambo kuwa ccm wanaturudisha kwenye zama za ujima
 
Uteuzi wake kwanza ni batili kuringana na sheria /Katiba ya Nchi asa Ibara ya 116 .Katibu mkuu kiongozi anateuliwa na Rais kutoka kwa Maafisa waandamizi wa Utumishi wa Umma.

Je, Bashiru amekua lini mtumishi wa umma na mwandamizi?

Labda Rais atumie tu mile kipengere kua ata akivunja sheria hamna wa kumuajibisha.
 
Angepewa mmoja kati ya very senior long serving Pemanent Secretaries, ingalau confidence ingekuwepo.

-
**Akizungumza baada ya kula kiapo, ameeleza kuwa kwa maadili na utamaduni, kazi za Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi sio kazi za maneno bali ni za kusikiliza, kujifunza na kuchambua, kuamua na kutenda
-
Amesema, "Wale waliotegemea kwamba nitazungumza tena kwa kweli nitazungumza kwa tahadhari na umakini kwasababu kiapo mmekisikia. Ni Katiba, Sheria, taratibu, mila, desturi"
-
Aidha, amezungumzia suala la umuhimu wa mawasiliano ndani ya Serikali na kati ya Serikali na Umma akisema watasimamia hilo**

Maneno yake hayo

Means anaenda kujifunza kazi akiwa ofisini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…