Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 490
- 704
Nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wa Tamisemi Mh Bashungwa kwa hatua aliyochukua kuhusu kero ya maegesho ya gari toka Tarura walipojikita na mfumo wao.
Ni kweli Tarura walifikia hatua ya kujisahau kazi yao ya msingi na kuamua toza tozo za maegesho ndiyo maana hata kero walikuwa hawajali.
Hatukatai lipia maegesho lakini tatizo kubwa lilikuwa hujui unadaiwa nini na kwa sababu gani unakuta tu adhabu tena za kutengenezewa.Mh Waziri nikupe hongera sana kwa kusikiliza kilio chetu na kukifanyia kazi well done.
Niombe na Mh Waziri wa Mambo ya ndani na waziri wa Nishati nanyi mfate nyayo kwani sasa hivi tunapitia changamoto za hawa vijana wanaojiita panya road na hii ya bei ya mafuta.
Nikianza na panya road hawa vijana wakiendelea na tabia hii inaweza leta vurugu kwani ni vijana wadogo na wanaweza pia kutumika . Samaki mkunje bado mapema.Inaweza fika mahali watu wakachoka na kuanza chukua sheria mikononi .
La mafuta mhe Waziri mafuta ndiyo kila kitu kama diseli imepanda hivo kumbuka magari ya kusafirisha mizigo ( vyakula n.k) abiria na mitambo yote ikiwa pamoja na mashine za kusaga nafaka vinatumia nishati hiyo, leo bei kwa Dar es salaam ni 3200 ni kichocheo kwa bidhaa na huduma kupanda maradufu.Naomba Mh uliangalie swala hili maana uchumi utateketea hali ya maisha tayari ni ngumu.