Namshauri kocha wa simba kuendelea kumtumia Mugalu kwenye match ngumu za Klabu Bingwa

Namshauri kocha wa simba kuendelea kumtumia Mugalu kwenye match ngumu za Klabu Bingwa

TUPAMBANE

Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
62
Reaction score
88
Mimi ni shabiki wa timu ya simba Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wakitaka kocha wa simbs amtumie Kagere badala ya Mugalu Ila wengi wanaendeshwa na mihemko. Naomba niwalinganishe watu wawili kagere Na Mugalu.
Kagere udhaifu
1. Kwanza hajui Kukaba
2. hajui kujiposition
3. hajui kupora Mipira
4. anawafanya mabeki kurelux
5. hatishi

ubora wa Kagere

1. mwepesi kufunga pale anapopata mpira.

udhaifu wa Mugalu
1. kukosa magoli ya wazi

ubora wa Mugalu
1. anajua kujiposition
2. Anajua kukaba
3. anajua kukaba
4. mabeki hawana nafasi ya kurelux kwa huyu mwamba
5. anatisha akiwa hana mpira na akiwa na mpira
6. uwezo wa kumtumia kama mshambuliaji mmoja anafa sana kwa mfumo huo

zingatia
Kazi ya mshambuliaji ni kushinda ila soka limebadilika sasa kazi ya mshambuliaji ni kusaidia timu yake kushinda hivyo ndicho Mugalu anakifanya kwa kuhold mpira wenzake wasogee na wakishasogea anawapa mpira anakimbilia kwenye nafasi wakati huo ameshagongwa gongo viatu vya kutosha anakuja kupata mpira ameshachoka matokeo yake yanatokea mnayolalamikia. sasa hapa kocha anaweza kufanya mabadiliko kwa kumwelimisha tu mugalu kwamba ukipata mpira angalia mtu aliyepo karibu umpe tufunge basi.

Kumbuka
timu ya france ilichukua kombe la dunia kwa mshambuliaji wake jirudi kutokufunga goli hata moja lakini match zote alichezeshwa japo watu walikuwa wanapiga kelele sana hivyo kocha wetu anamwona Mugalu yuko sawa kwa maana kuna kuna kitu anampatia tofauti na kagere
 
Nashangaa mtu anasema kagere hawezi kujiposition et Mugalu ndio anaweza kujiposition. Wakati muda mwingi hua yupo offside. Kagere pamoja na kukosa muda was kucheza Ila anaongoza kwa magoli. Ina mana anafunga bila kujiposition?
Goli la pili la jana la Kagere angekuwa Mugalu ingekuwa ofside pale.
 
Huyu Mugalu kawaroga aiseeh, yaani unasema kabisa kwa kujiamini eti "Kagere hajui kuji-postion?
" daaah[emoji3][emoji3].

Kama issue ni kwamba Kagere anafunga magoli mepesi, mbona huyo Mugalu anakosa magoli ya wazi? Ikumbukwe kuwa, hakuna timu inayosajili mshambuliaji Ili aje akabe, thamani ya mshambuliaji ipo katika uwezo wake wa kufunga, hilo ndo jukumu lake la kwanza uwanjani na Mugalu haliwezi.

Utasikia mara Mugalu ni "Mshambuliaji mkabaji"[emoji3].Kiufupi Mugalu anabebwa na wachexaji wengine pale Simba,yani kama team isingekuwa inapata matokeo, kwasasa yule asingekuwa na tofauti na Ditram Nchimbi maana hata yeye anakaba,shida ni kufunga tu.
 
Bro achana na hii mambo ya kuchambua mpira. HAUNA UWEZO!
Mimi sio mchambuzi ila ninajua wazi kuwa kazi kubwa ya Mshambuliaji ni kuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo kwa kutumia nafasi chache anazopata.
Mchezaji wa calibre ya Mugalu hana uwezo huo. Yule anafaa kwenye mechi ambazo hazina ulazima wa kulazimisha matokeo bali zenye ulazima wa kujilinda hususani za ugenini.
Kama unakuwa unafuatilia mpira kwa uzuri utagundua kuwa Kagere kacheza dakika chache sana kwenye ligi ya Mabingwa ila chances zake alizojaribu kuleta hatari ni nyingi zaidi.
Mugalu hana lolote zaidi ya ile Penalt ya kule Kongo.
 
Mugalu ni galasa, striker ambaye anakosa nafasi za wazi sio striker, kazi kuu ya Striker sio kukaba wala ku hold mipira, kwa maelezo yako basi tumpeleke Nyoni hiyo nafasi, striker anakosa vipi nafasi za wazi nyingi halafu anataka tumsifie kwa kukaba, hata Ditram Nchimbi na Sarpong pia wanajua kukaba.
 
Timu ambazo Simba SC inaweza kucheza nazo fainali ya Klabu Bingwa Dunia mwaka huu
1.Man City
2.Chelsea
3.Real Madrid
4.PSG"
 
We KACHAMBUE MCHELE huko, huwezi KUCHAMBUA MPIRA

kamtizame tena kagere, tena kwa makini ulete bango lako upya.. Kagere ana njaa ya magoli, kagere msumbufu, kagere anajua mno kujiposition, kagere anakaba kuanzia juu (tizama kuna baadhi ya game alishafunga goli kadhaa kwa kumfata tu golikipa wa upinzani)

Kwangu, kwanini mwalimu anaanza na MUGALU na si KAGERE nitasema mwalimu ndio anajua zaidi na hatujui mazoezini nani anaonesha zaidi,kuna mwaka sikumbuki tevez pale man u alikuwa anatokea sana sub na anaamua mechi mzee fergie akaulizwa kwanini asianze,akajibu mazoezini haoneshi.. Ila kwa sababu zangu za kisoka KAGERE ni mzuri kuliko MUGALU kwa hivyo vipengele ulivyowashindanisha kwa asilimia kubwa tu.
 
Mimi ni shabiki wa timu ya simba Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wakitaka kocha wa simbs amtumie Kagere badala ya Mugalu Ila wengi wanaendeshwa na mihemko. Naomba niwalinganishe watu wawili kagere Na Mugalu.
Kagere udhaifu
1. Kwanza hajui Kukaba
2. hajui kujiposition
3. hajui kupora Mipira
4. anawafanya mabeki kurelux
5. hatishi

ubora wa Kagere
1. mwepesi kufunga pale anapopata mpira.

udhaifu wa Mugalu
1. kukosa magoli ya wazi

ubora wa Mugalu
1. anajua kujiposition
2. Anajua kukaba
3. anajua kukaba
4. mabeki hawana nafasi ya kurelux kwa huyu mwamba
5. anatisha akiwa hana mpira na akiwa na mpira
6. uwezo wa kumtumia kama mshambuliaji mmoja anafa sana kwa mfumo huo

zingatia
Kazi ya mshambuliaji ni kushinda ila soka limebadilika sasa kazi ya mshambuliaji ni kusaidia timu yake kushinda hivyo ndicho Mugalu anakifanya kwa kuhold mpira wenzake wasogee na wakishasogea anawapa mpira anakimbilia kwenye nafasi wakati huo ameshagongwa gongo viatu vya kutosha anakuja kupata mpira ameshachoka matokeo yake yanatokea mnayolalamikia. sasa hapa kocha anaweza kufanya mabadiliko kwa kumwelimisha tu mugalu kwamba ukipata mpira angalia mtu aliyepo karibu umpe tufunge basi.

Kumbuka
timu ya france ilichukua kombe la dunia kwa mshambuliaji wake jirudi kutokufunga goli hata moja lakini match zote alichezeshwa japo watu walikuwa wanapiga kelele sana hivyo kocha wetu anamwona Mugalu yuko sawa kwa maana kuna kuna kitu anampatia tofauti na kagere
hahaha ila hata hivyo tuache utani mugalu ana nyota asee
 
Mugalu ana muda mchache sana wa kucheza ukilinganisha na Kagere. kujiposition ninakozungumzia mimi ni kukaa kwenye njia ya kufunga kitu ambacho kinawafanya mabeki kuwa na wasiwasi Muda wote kukaba ninakozungumzia mimi ni kule timu Inapozidiwa yeye hurudi na kusaidia au hukaa na mipira mbele akisubiria wenzake kitu ambacho kagere hajui. Mugalu ni muda tuu utakuja kuutafuta uzi wangu na kunishukuru
 
Kwahiyo kaja simba kujifundisha hayo mambo??
 
miongoni mwa vitu disappointing kwenye mpira, ni kuona jitu limejaaliwa mwili, urefu, halafu hajui kucheza mpira. in the contrary unakutana na messi, mfupi, hafanani na mpira ila anaujua vilivyo. mugalu ni wa kutupa mbali kabisa na siku ile angeingia yeyote yule simba walikuwa wanashinda.
 
Huu ushauri mzuri ila Simba wanamkumbatia

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom