Namshukuru sana prof. Kapuya kufuta mitihani ya Taifa mwaka 1998.

Namshukuru sana prof. Kapuya kufuta mitihani ya Taifa mwaka 1998.

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Nakumbuka mwaka 1998 kulikuwa na sakata la kuvuja kwa mitihani ya NECTA.
Mitihani ilianza Siku ya Jumatatu kwa kuanza na hesabu sikuwa nazijua kabisa na sikuzipenda.nilijiamini kupita kiasi kwakuwa nilikuwa na majibu toka nje na kila mwanafunzi alipata mitihani ile na ilikuwa yenyewe kweli
Mwalimu wetu wa historia alitusovia maswali kumbe alikosea kusoma na kuelewa maelekezo wote tukaongia chaka.
Nilipofika nyumbani sijasikia taarifa ya habari wazir mafuta mitihani na itarudiwa baada ya muda
Nilifurahi sana na tangi Siku hiyo sikujihusisha tena na wizi wa mitihani
Namshukuru sana mzee kapuya.
Tuliokumbwa na lile janga tukutane hapa kwa uzoefu ndugu zangu
 
Duuu,
Hapo mzee mzima nipo nyumbani nafundishwa "a, e, i ,o ,u" na dada wa kazi.
 
Zee lile roho mbaya kama nini. Halikutaka wengine wafanikiwe.

Na wewe nakushangaa kuliunga mkono, lilisababisha watu wakose ulaji.

Mizee yenye roho mbaya kama Likapuya huwa inazeeka na kufa vibaya.
 
Mimi nakumbuka 2008 tulifutiwa Mathematics tukapewa muda kama wa week mbili hivi kujiandaa then tukarudia, kwa kweli nilifurahi mno maana nilipata muda mzuri wa kusolve maswali mengi ambayo yalinisaidia kufaulu Math kwa kiasi chake. Namshukuru sana waziri wa kipindi hicho anamchangi sana kwa hiki nilichonacho sasa.
 
Mkuu kumbe tupo wengi tuliomaliza mwaka ule wa majanga....
nakumbuka Kwenye somo la geography Kwa mtihani wa Kwanza walikuja na map reading ya mkoa wa Lindi na baada ya kufutwa na kurudia tena wakaja na mkoa wa Lindi tena huku wakitofautisha maeneo.
...aisee jamaa wa necta ni wajanja sana
 
Sio vibaya kukiri dhambi uliyowahi kuifanya.
 
Nakumbuka mwaka 1998 kulikuwa na sakata la kuvuja kwa mitihani ya NECTA.
Mitihani ilianza Siku ya Jumatatu kwa kuanza na hesabu sikuwa nazijua kabisa na sikuzipenda.nilijiamini kupita kiasi kwakuwa nilikuwa na majibu toka nje na kila mwanafunzi alipata mitihani ile na ilikuwa yenyewe kweli
Mwalimu wetu wa historia alitusovia maswali kumbe alikosea kusoma na kuelewa maelekezo wote tukaongia chaka.
Nilipofika nyumbani sijasikia taarifa ya habari wazir mafuta mitihani na itarudiwa baada ya muda
Nilifurahi sana na tangi Siku hiyo sikujihusisha tena na wizi wa mitihani
Namshukuru sana mzee kapuya.
Tuliokumbwa na lile janga tukutane hapa kwa uzoefu ndugu zangu
Kwenye shule yetu,huko Kijijini kuvuja kwa mitiani,tulikuwa tunasikia tu,
Nakumbuka paper two ya physics nili chora michoro kwa kutumia peni,maana niliona nikitumia karamu haitaonekana vzr,ticha wangu akaja kimya kimya akaniambia nitapigwa penati,nilichanganyikiwa,maana nisingeweza kuanza kuchora upya,maana muda ulikuwa umeisha, nilidata,harafu msimamizi alikuwa mnoko,hakutaka tutumie calculator hata kwenye chemistry,nilipotoka nje,nilijua ndoto yangu ya kuwa engineer Basi Tena,
Pepa ilipofutwa,nirifurahi sana,nilipo rudi January kupiga paper,sikufsnya makosa,leo nakula matunda ya PCM
 
Back
Top Bottom