Namtabiria Shilole kuja kuwa msanii wa kike mwenye pesa ndefu kuliko wote

Namtabiria Shilole kuja kuwa msanii wa kike mwenye pesa ndefu kuliko wote

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ninamtabiria huyu mwanadada Zuwena Muhammed(Shishi baby) baada ya miaka mitano atakuwa ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye pesa nyingi zaidi hapa nchini.

Kitu kikubwa ambacho kinanisukuma kusema haya ni kutokana na tabia ya kujituma sana huku akiweka aibu pembeni mpaka pale jambo lake alitakalo litakapo fanikiwa.

Mbali na hilo Shishi ndiye msanii wa kike anayependwa zaidi hapa nchini kuliko msanii yeyote yule wa kike ,na yote hii ni kutokana na tabia yake ya kupenda kujichanganya na kila aina ya watu kuanzia wa hali ya chini kabisa mpaka wale wenye mpunga mrefu. Kwa kigezo hiki kwa namna moja au nyingine kinamfungulia milango ya ridhiki kila kukicha.


Mpaka sasa makampuni kadhaa zimejitokeza na nyingine nyingi zinazidi kujitokeza ili kuingia mkataba naye ambapo wanamlipa pesa iliyonona.

1)Hapa akisaini mkataba na TTCL
shilolekiuno_badgirlshishi-20180826-0001.jpg


2)Hiki ni kitabu chake kipya kilichoingia sokoni hivi punde.
shilolekiuno_badgirlshishi-20180826-0002.jpg

Shilole pia ni msanii wa kike anayeoma mbali sana na hilo lilijidhihirisha pale alipokubali kuolewa na fundi gereji ambaye kwa siku kipato chake hakizidi hata elfu 10.

Wengi walimcheka sana Shilole nikiwemo mimi,nilimponda vibaya sana ila kila kukicha amezidi kutu proove wrong kwamba hakukosea kukubali kuolewa na Uchebe ambaye hakuwa na mbele wala nyuma .

Watu wenye pesa zao wamelisumbukia sana penzi la Shilole bila mafanikio yoyote mwisho wa siku akaangukia mikononi mwa Uchebe na tangu aoelewe na Uchebe ,milango ya ridhiki inazidi kumfungukia kila kukicha.

Mungu azidi kum'bariki mwanadada huyu aweze kutimiza mahitaji ya moyo wake ikiwemo kujua kiingereza.
 
Broken [emoji813], anyway it's all fine

Sent from my iPhone 6s using Tapatalk
 
Mimi simpendi na tabia zake mbovu za kudunda viben ten vyake.

Barnaba,Nuhu wamedundwa sana tu.
 
Back
Top Bottom