NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Msoto wa mtaa huwa ni mkali sana pale ambapo mtoto asie na support akishindwa kuendelea na shule au akithitimu chuo ila hakuna ajira, msoto umefanya hadi baadhi ya waathirika waishie jela, kufanya kazi zilizo kinyume na maadili, kufanya kazi ngumu sana zenye vipato vidogo, n.k.
Binafsi baada ya kufeli form 4 nilipigwa na msoto mkali sana ikanibidi ni fight sana kuanza maisha ya kujitegemea maana nyumbani hali ilikuwa mbaya kiuchumi, kupitia msoto si jambo la kujisifia kama wengi waavyodhani, ilinibidi nijinasue katika maisha hayo ya shida na karaha kwa kuanza kufikiria ni vipi ntapata pesa, ilinibidi nijitoe kwa jasho, damu na machozi kujifunza useremala maana nilifundishwa mtaani na watu wa mtaani, haikuwa rahisi hata kidogo, nikikumbuka huwa naona ni heri nimfundishe mtoto wangu mapema fani yangu ili asije kupitia msoto.
Kwa sasa nimeamua kummegea mtoto wangu ujuzi huu nilionao kwa njia ambayo ana enjoy kujifunza bila stress nilizopitia za kufokewa, kutishiwa kufukuzwa, kukaripiwa na kulaumiwa nilizopitia nikiwa najifunza mtaani, Namfundisha akiwa bado na umri mdogo hivyo najua atakuwa bora na mzoefu kuzidi mimi akiwa hata na miaka 20 tu.
Yupo shule ya msingi na shule inaendelea kama kawaida na ninamsapoti kwa vingi sana, hata shule anayosoma nimeona nimpeleke english medium japo ni ya serikali.
Mtoto wangu natamani aje kupata cheti chake safi na aajiriwe sehemu yenye hadhi lakini kwa hali ya sasa ilivyo haya mambo yanabaki kuwa ndoto maana wasomi kibao hawana ajira,
Hivyo basi nimeona nimpe ujuzi huu ili iwe ni bima yake endapo shule itamshinda (sitarajii lakini inaweza tokea) au atasoma lakini akakosa ajira, Yote hii ni kumkwepesha msoto wa mtaani, mambo yakibugi aingie fasta kwenye kujiajiri akiwa tayari mzoefu.
Lakini pia sioni ubaya wowote hata akiajiriwa anaweza kujiongezea kipato kwa kuunganisha kipato cha kuajiriwa na kujiajiri.
Pia siwezi kujua kesho yangu kama mzazi, Naweza nikapatwa na majanga kwa hio imenibidi nianze kumuandaa mapema ajue namna ya kupambania tonge
Ushauri kwa wazazi wanakwepa kufundisha watoto wao:
Kazi hizi ambazo wengi tumejiajiri mtaani tusione aibu kuwafundisha watoto wetu kisa zinaonekana ni kazi za watu wa chini ama wa kawaida, Ni wengi tunapenda watoto wetu waje kupata kazi zenye hadhi maofisni lakini sikuhizi, hakuna uhakika wa ajira, Mtaani pagumu sana wazazi wenzangu hasa wale tunaoujua msoto, Hatuna sababu ya kuwapitisha watoto wetu msoto tunaoweza kuwafundisha kuukwepa.