Namuanzaje mamamkwe-mrejesho

Mshukuru Mungu kakuonyesha udhaifu wa huyo mwanamke mapema na ukishamjua mbwa hakupi taabu!
 
Bado hakuna kitu cha kuprove hapo.
Suppose mama hakutaka ujue, unafikiri angesema nilimwambia 'Ester' achukue pesa kwenye account yako?

Kwanini hukumpa live mchumba wako kitu ulichoongea na mamamkwe, ingekuwa ngumu kutunga uongo wa haraka2.

Maybe, ni yeye alichukua hiyo pesa na akatumia kwa kitu ambacho wewe hukipendi au ulimkataza; so akaamua kusema uongo ili apunguze ugomvi, such a big deal!

Kaka mimi nafikiri, umuache tu huyo dada hakufai kabisa! Yaani katumia laki tano zako bila ruhusa wala maelezo ya maana! Si mwaminifu halafu ni mwizi na si ajabu ametumia kuhonga wanaume. Yaani ningekuwa mimi ningemuacha long time!
 
Kwanza pongezi kwa kutupa feedback. Hapo kweli pagumu kaka, jaribu kuvumilia kidogo labda ukirudi bongo utapata jua ukweli wa mambo sembuse mwanamama alitumia pesa kwa sababu za msingi kabisa thou sio vyema kwamba hakukuweka wazi. Ukijua A-Z ndo uamuzi ufanyike.
 

Dadaangu Kaunga kumbuka kwanza niko mbali na yeye ndiye mwenye account yangu kwa sasa. Kwa hiyo kitendo chochote kitakachopelekea yeye kujua kwamba ninaujua ukweli kinaweza kunigharimu sana. Nimeona bora yeye aendelee kudhani mimi sijui wakati ambapo natafuta namna nzuri ya kurudisha kila kitu mikononi mwangu. Kama kweli itakuwa mamamkwe ndiye alizikopa na kaogopa kusema bado kwangu mimi sio jambo baya pia!

Kumpiga chini au kutompiga yatakuwa ni maamuzi ya mwisho baada ya kurudi home na kuweka kila kitu wazi!..(hilo jina la 'esther' umenikumbusha mbali kidogo)..otherwise pamoja sana!
 
Mkuu umefanya vizuri kuongea na mama yake. Binafsi kitu ninachoona hapa ni kuwa huyo bidada hafai kwa vigezo vya uaminifu, umemuamini kwa kiasi kikubwa sana, alishindwa nini kukuambia hata kama ingekuwa kweli kuwa ni mama yake amezitaka?! Mbona wachumba huambizana hata mambo ya ndani sana ya familia zao? Usidanganyike, hata ingekuwa elfu hamsini bado ni hela yako na angetakiwa kukushirikisha, hapa siyo suala la u-malaika bana hivi uaminifu unaanzia wapi? Watu tumetofautiana sana, binafsi mtu wa aina hiyo ni kutafuta namna ya kuipata ATM card yako halafu unaachana naye kistaarabu tu.
 
Sasa Bw. Snowball ninachokushauri ni kwamba hili sio tatizo la kukufanya usitishe uchumba. Ni kweli mtu wa karibu kiasi hicho kukuzunguka inauma sana. Lakini ni mambo yanayotokea hata kwenye ndoa. Isitoshe huwezi jua huenda mkeo mtarajiwa alifanya hivyo kwa kurubuniwa na mama yake. Huenda alitoa hizo hela kinyume kabisa na dhamiri yake, labda alishindwa kumkatalia mama yake mzazi. Hayo yote unapaswa kuyafikiria kabla hujafanya maamuzi. Binafsi sioni sababu ya kutosha kufikiria upya uhusiano wako na mchumba wako. Jiulize, je angekuwa mke tayari, kwa hili tu ningeanza mchakato wa kutafuta talaka?
 

If this is the way you approach life, then call yourself A BIG LOSER!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…