Namuhurumia Samatta

Ukute hata familia yako inakushinda kuiendesha ila upo busy na kumponda Samatta
 
Ukute hata familia yako inakushinda kuiendesha ila upo busy na kumponda Samatta
Kwanza, familia yangu hainishindi.

Pili, huo ni mtazamo wa kimichezo. Na kuandika kuwa Samatta anatakiwa ajiongeze ili afanikiwe kuzishinda changamoto zinazomkabili sio kumponda.

Kuna tetesi kuwa A.Villa wanataka kumtoa kwa mkopo kwenda Fenerbahce ya Uturuki. Hili jambo sio zuri hata kidogo kwenye maisha yake ya soka. Pale Villa kuna wachezaji wa kawaida na anaweza kupambana na kuonesha uwezo aliokua nao. Kwa sababu asipofanya hivyo, atakua ametuangusha sana sisi watanzania wapenzi wa soccer tunaojidai kuwa tuna mchezaji epl.

Lakini pia akianguka ki soccer, haitamgharimu yeye tu, bali itaweka mazingira magumu sana kwa mchezaji mwingine kutoka Tanzania kuweza kushiriki league ya uingereza. Imani kwa wachezaji wetu itapungua. Kwaiyo hizi kelele zetu na kumshtua shtua kidgo kuwa akazane ni for the greater good. Sio kwa ajili yake tu, bali ni kwa ajili ya wanamichezo wetu wote. Kinachofanya wachezaji wa America kusini kusajiliwa sana ligi za ulaya ni kwa sababu ya rekodi bora zilizowahi kuwekwa na kaka zao waliowatangulia. Think Big, Brother

Huo mfano wa KDB nimeona ni mfano hai kwa sababu na yeye alitokea Genk lakini alikazana sana mpaka akafikia hapo alipofika saivi even though alikutana na challenges kama za samatta za kutokuaminiwa na kocha.

Siku zote anayekuonya, huwa anakujali ila kama kusema ukweli mchungu kwako ni kuponda, so be it.
 
Samata amekosa kujiamini, kila mpira anaopata anataka kutoa pasi wakati timu haina muunganiko mzuri anapaswa awe anajaribu hata kudribble na kushoot mwenyewe asitegemee assist.
 
Ukute hata familia yako inakushinda kuiendesha ila upo busy na kumponda Samatta
Mkuu, mleta mada hii, sidhani kama ameileta kwa ajili ya KUMTAKIA MABAYA SAMATTA.
Ametoa tahadhari, na kumtolea mfano KDB, kuwa pamoja na uzuri wake, hao CHELSEA, hawakutambua hilo. Hata Samatta, ajue kuwa hao jamaa wanaweza wakamtosa, pamoja na uzuri wake, ambao bado hajauonyesha. Lakini kwa vile SIASA zimetuharibu, hata mtu akitoa ushauri mzuri ambao hauhusiani kabisa na SIASA, wadau watakuja kupinga na kejeri juu!
 
Tumpe muda Samatta,mpira siyo karata hata kina Mohammad Salah na huyo KDB walionekana magalasa...... Saizi wanaimbwa
 
Imedhihirika, yuko uturuki saa hii Fehnebach kwa mkopo akitoka pale utaskia yanga, mara mpoki sportclub mara mwembeni mchikichini mara huyooo hatumuoni tena.
Imeisha hiyo kwa umri wake ndii imetoka
 
Wewe badala ya ujihurumie wewe na familia yako unakaa kumuhurumia mtu alokuzidi kila kitu.
 
Kwanza mou mwenyewe hakumuuza kdb alisema mwenyewe ni bodi ndio iliyomuuza sio yeye walipoenda tour asia akarudi akakuta kauzwa.
 
Tusiongopeane wakuu kwa samatta umri umeenda, mpira na umri ni vitu viwili tofauti
Tp Mazembe kacheza miaka 5
Genk kacheza miaka 4
Aston vill na fernabache kacheza miaka 2
Jumla ni miaka 11

Na wabongo sisi tunajuana kwenye umri hapa bongo lazima alitoka akiwa 24 au 23 na ukijumlisha mpaka sasa anaweza akawa na 35

Age number doesn't lie
 
Umri umeenda, halafu akavuta na jiko! Hapo lazima kiwango kitakua ni cha kawaida tu.
 
Kazi na umri...kama hakuwekeza basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…