NAMUNGO FC WATOA SHUKRANI KWA MAJALIWA...DC RUANGWA ASEMA TIMU ZA LIGI KUU ZIJIPANGE.

Joined
Mar 22, 2019
Posts
46
Reaction score
55
Na Bakari Chijumba,Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mh. Hashim Mgandilwa amewataka wakaazi wa Ruangwa kuwa na utamaduni wa kusaidia timu ya Namungo Fc iliyo na maskani yake wilayani humo.

Mgandilwa amesema timu ya Namungo inaendeshwa kwa misaada ya wananchi ila kumekuwa na kusuasua kwa michango kutoka kwa wakazi wa Ruangwa.

Ametoa kauli hiyo hii leo 05 Mei 2019, wakati wa halfa ya kuipongeza timu ya Namungo Fc ambayo imefuzu katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Hafla hiyo ya kuipongeza Namungo kwa kufuzu ligi kuu, imefanyika katika kitongoji cha Namungo kilichopo katika kijiji cha Chingubwa, kata ya Mbekenyera, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

"Tusiwaachie watu wa nje pekee yao kutuchangia, tunapaswa tuoneshe mfano na si lazima uchangie kiasi kikubwa hata iwe shilingi 1000 inapokelewa changieni timu yenu, uzalendo kwanza" amesema Mgandilwa na kuongeza kwamba;

"Niwahakikishie kila mtu wa Ruangwa atacheza kwa wakati ili kufanikisha kufanya vizuri kwenye mashindano ya ligi kuu na huko hatuendi kushiriki tunaenda kushinda "

Mgandilwa amesema,sasa kuna timu ya Namungo ambayo ipo Wilayani Ruangwa hivyo hakuna sababu ya wakaazi wa maeneo hayo kushangilia timu nyingine.

"Uzalendo kwanza, tuache timu zetu za zamani tuhamishie mapenzi kwa Namungo na tuendele kwenda kuishaingilia timu yetu kila inapocheza kama tulivyofanya msimu wa ligi iliyopita" amesema Mgandilwa.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaasa wachezaji kuwa mpira ni ajira hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha nidhamu, kujituma na ushirikiano una tawala kati yao.

"Hakuna mafanikio yanayokuja bila kujituma, hamuwezi kupanda bila jitihada, mpira ni ajira yenu muipende na kuithamini mtafika mbali " amesema Mgandilwa.

Naye Naibu mwenyekiti wa timu Francis Mwigila,ametoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa anaoendela kuutoa kweny timu tangu inaanza mpaka ilipofikia

Mwigila ameishukuru pia ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ushirikiano walioutoa wa ndani na nje kwa timu hiyo.
IMG-20190505-WA0085.jpeg
PMO_8443-1024x646.jpeg
IMG-20190505-WA0089.jpeg
IMG-20190505-WA0083.jpeg
IMG-20190505-WA0087.jpeg
 
Kama ilipanda kwa kubebwa kisa inatoka kwa PM, basi itashuka au kulia njaa sana msimu mzima. Mpira ni biashara wasitegemee sana hisani za wananchi. Wabuni miradi
 
Na Bakari Chijumba,Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mh. Hashim Mgandilwa amewataka wakaazi wa Ruangwa kuwa na utamaduni wa kusaidia timu ya Namungo Fc iliyo na maskani yake wilayani humo.

Mgandilwa amesema timu ya Namungo inaendeshwa kwa misaada ya wananchi ila kumekuwa na kusuasua kwa michango kutoka kwa wakazi wa Ruangwa.

Ametoa kauli hiyo hii leo 05 Mei 2019, wakati wa halfa ya kuipongeza timu ya Namungo Fc ambayo imefuzu katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Hafla hiyo ya kuipongeza Namungo kwa kufuzu ligi kuu, imefanyika katika kitongoji cha Namungo kilichopo katika kijiji cha Chingubwa, kata ya Mbekenyera, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

"Tusiwaachie watu wa nje pekee yao kutuchangia, tunapaswa tuoneshe mfano na si lazima uchangie kiasi kikubwa hata iwe shilingi 1000 inapokelewa changieni timu yenu, uzalendo kwanza" amesema Mgandilwa na kuongeza kwamba;

"Niwahakikishie kila mtu wa Ruangwa atacheza kwa wakati ili kufanikisha kufanya vizuri kwenye mashindano ya ligi kuu na huko hatuendi kushiriki tunaenda kushinda "

Mgandilwa amesema,sasa kuna timu ya Namungo ambayo ipo Wilayani Ruangwa hivyo hakuna sababu ya wakaazi wa maeneo hayo kushangilia timu nyingine.

"Uzalendo kwanza, tuache timu zetu za zamani tuhamishie mapenzi kwa Namungo na tuendele kwenda kuishaingilia timu yetu kila inapocheza kama tulivyofanya msimu wa ligi iliyopita" amesema Mgandilwa.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaasa wachezaji kuwa mpira ni ajira hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha nidhamu, kujituma na ushirikiano una tawala kati yao.

"Hakuna mafanikio yanayokuja bila kujituma, hamuwezi kupanda bila jitihada, mpira ni ajira yenu muipende na kuithamini mtafika mbali " amesema Mgandilwa.

Naye Naibu mwenyekiti wa timu Francis Mwigila,ametoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa anaoendela kuutoa kweny timu tangu inaanza mpaka ilipofikia

Mwigila ameishukuru pia ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ushirikiano walioutoa wa ndani na nje kwa timu hiyo.View attachment 1089286View attachment 1089287View attachment 1089288View attachment 1089289View attachment 1089290
Team haichangiwi na wanachi acha uongo, timu inachangiwa na wachimbaji wa mgodi wa namungo wakisaidiwa na Mbunge wao.
 
Hakuna jipya team Za kisiasa aka za uchaguzi. Ikidumu hata misimu mitatu bahati otherwise PM a invest billions of Tsh.
 
Back
Top Bottom