Namungo FC ya Ruangwa-Lindi, yatinga ligi kuu

Ni Namungo, mkuu... shukran kwa udadavuzi tho
 
Naona PM kajipandishia team yake!!! Soccer la bongo itaendelea kudumaa milele.
Hapo ndipo wenye maono na kuelewa mambo wanasema itachukua karne kadhaa kukuza kiwango cha michezo tz.
Suluhisho ni kuwa na vyama vya michezo vinavyowajibika kwa wanachama wao (timu) badala ya hivi ambavyo vinawajibika kwa watawala. Kwa haraka haraka unaweza kuona ni mafanikio lakini sehemu yanye lundo la vipaji kama Kigoma haiwakilishwi ligi za juu kwa vile eti hapana 'mwenye cheo' wa kuwabeba!
 
Hivi unaweza kunitajia sababu MOJA TU inayowafanya muasiamini Namungo imepanda kutokana na uwezo wake?!

Btw, hivyo vipaji vya Kigoma vita-shine vp ikiwa hakuna support?! Zamani Kigoma kulikuwa na timu kama TRC (sikumbuki vizuri jina) ambayo ilikuwa ni timu ya kampuni yenye resources; what about siku hizi?!
 
Hahaahahahahahahaha uchawi hauvuki mpaka
 
Mtashuka tu kama wanafunzi wa alliance
 
Asante kwa kutokuwa shabiki na badala yake umeibua hoja inayoweza kuanzisha mjadala endelevu.
Tunavyosema support inabidi itokane na industry ya mpira wenyewe, mfano kuwa na ligi kuu imara, ligi daraja la kwanza imara angalau hadi ligi daraja la pili na confederation competition zenye kuaminika. Ikipendekezwa kuwa timu inayoshiriki ligi kuu hata isiyo na mfadhili minimun pay (weekly/monthly, annually nk) iwe kiwango fulani na hiyo pesa itolewe na sponsor wa ligi utakuwa umeepuka timu ya ligi kuu kukopeshwa nauli na wabongo fleva ambapo ni aibu.
Chama cha mpira kingekuwa kinawajibika kwa wanachama wake kwa hakika wasingecheza ligi bila sponsor hivyo kuweza kubalance consistency ya timu shiriki ikiwa ni pamoja na kuibua timu mpya zenye msukumo wa wapenda mchezo badala ya msukumo wa 'fulani'.
 
Nakubaliana na maelezo yako kwa 100% lakini ninachoona tuhuma za watu dhidi ya Namungo ni kama wanaona imepanda kutokana na kupendelewa!!

Ninavyofahamu, ligi Daraja la Kwanza imejaa ukata mtupu! Matokeo yake, pakitokea na timu yenye uwezo wa kuwalipa wachezaji hata Sh. 50K kwa mechi basi kuna uwezekano timu hiyo inaweza kufanya vizuri hata kama inaweza isiwe na ubora! Inaweza kufanya vizuri kwa sababu, wakati wao wanaweza kuwalipa wachezaji Sh.50K, kwa upande mwingine watakuwa wanapambana na timu ambazo hazina uwezo wa kulipa hata Sh. 10K!!

Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana timu ya daraja hata ikipata ufadhili uchwara, utakuta inafanya vizuri na kupanda daraja! Lakini kwavile haikupanda daraja kutokana na ubora wake bali kutokana na kuwazidi wapinzani waliokuwa na njaa; ndipo wanapotua tu Ligi Kuu wanaishia kufanya viroja!!!

Kila nikiiangalia Namungo, naiona ina resources karibu zote muhimu! Wana kocha aliyetoka Ligi Kuu ambae anasaidiwa na ex-Premier League Player! Hawa kwa umaskini uliopo kwenye timu za daraja za kwanza, Namungo unaweza kusema ni miongoni mwa timu tajiri!!

So, inawezekana kabisa kwamba isiwe na ubavu wa kushindana na timu zilizojitosheleza za ligi kuu lakini wanapokutana na wale wenzangu mimi wa Daraja la Kwanza ambao si ajabu hata jezi za kubadilisha ni mtihani, siwezi kushangaa nikisikia Lyamungo ana-shine mbele yao!
 

Mkuu Chige ile gari ina namba zinazosomeka SM, bila shaka lile basi ni mali ya Serikali pia inawezekana na timu ikawa mali ya halmashauri ya Ruangwa maana sidhani kama wanaweza kupewa basi huku hawana mahusiano na Serikali..
 

Ilulu pale nina kahistoria napo fulani, Kariakoo ya Lindi naikumbuka sana kwa fitina zake pale Ilulu. Yanga ilibidi watue na ndege mchana maana Ilulu na Lindi paliogopeka sana kwa wageni... Its a good memory kwa kweli..
 
PM akiacha uwaziri mkuu na timu kwishney. Haaahhah bongo burudani sana.

Hivi Chato hakuna timu tuipandishe daraja?
 
Mkuu Chige ile gari ina namba zinazosomeka SM, bila shaka lile basi ni mali ya Serikali pia inawezekana na timu ikawa mali ya halmashauri ya Ruangwa maana sidhani kama wanaweza kupewa basi huku hawana mahusiano na Serikali..
Timu sio mali ya Halmashauri isipokuwa baada ya kupanda daraja, wilaya na mkoa wakaipa support! Moja ya support ambayo walitoa ni hiyo gari!! Unajua Kusini kwavile timu zinapanda kwa msimu basi ikitokea moja ikafika sehemu nzuri, wadau wote wanaelekeza nguvu kwenye hiyo timu!
 
Ilulu pale nina kahistoria napo fulani, Kariakoo ya Lindi naikumbuka sana kwa fitina zake pale Ilulu. Yanga ilibidi watue na ndege mchana maana Ilulu na Lindi paliogopeka sana kwa wageni... Its a good memory kwa kweli..
Don't tell me! Yaani ile suluhu ambayo Yanga tuliipata ilikuwa ni baada ya Yanga kucheza kama akina Chuck Norris?! Au nimesahau? Manake ninachokumbuka ni kwamba, timu ambayo ilipona pale Ilulu ni Yanga pekee na kupona kwenyewe ni kupata suluhu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…