Namuunga Mkono Bwana Kibamba kuhusu Tume huru kwanza, then katiba mpya pole pole

Namuunga Mkono Bwana Kibamba kuhusu Tume huru kwanza, then katiba mpya pole pole

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
Jinsi mwenendo wa Katiba mpya unavyoenda, kuna uwezekano ikachelewa kukamilika na kuundwa kwa tume huru kwa ajili ya Uchaguzi wa 2015!!!!

Mbaya zaidi, Tanzania inakabiliwa na matatizo makubwa ya ufisadi, Ujinga/Elimu duni, Afya Mbaya, na Unga/Levya. Haya matatizo hayatatuliki kwa serikali ya sasa na haya matatizo yanazidi kuwa sugu kwa sababu hakuna hatua mujarabu zinachukuliwa.

Kuna mambo mengi yanaendelea, Suala moja gumu ni Muungano, suala la Tanganyika na Muswada wa katiba.

Bila kuwa na maelewano ya dhati kati ya vyama na maridhiano ya wananchi, hatutapata Katiba mpya kwa wakati.

Ni lazima yawepo masikilizano, ubabe haitakuwa na maana..... kutumia nguvu ya Dola ni umbumbumbu

Pendekezo la Bwana Kibamba (Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba) linaungwa mkono. Tume ya sasa ivunjwe na sasa iundwe tume Huru ya uchaguzi kwa ajili ya Kuboresha daftari la wapiga kura, kusimamia kura ya maoni kama tuwe na Tanganyika ama la na kusimamia uchaguzi serikali za mitaa 2014 na Uchaguzi mKuu 2015.

Mapendekezo/Maoni ambayo yametolewa katika kuunda katiba mpya, yaingizwe katika katiba ya sasa ili kuunda tume Huru ya UChaguzi.


Tume huru iwe na wajumbe huru ifuatavyo.

- Vyama vya siasa
-Jukwaa la katiba
-NGOs
-Dini zote
-Vyuo.

Nawasililisha ili wana JF mujadili na kutoa maoni nini kifanyike.
 
tume kuwa na wajumbe kutoka dini zote ni sahihi. lakini dini zipi? na je zitatoa uwakilishi unaotakiwa?
 
Tishio la Tume ya Katiba mpya kujiuzulu, kuna matatizo mengi hapa.

Watanzania tuombe Tume Huru ya Uchaguzi kwanza, halafu tupate viongozi wenye utashi wa katiba mpya.

Watanzania tuna majanga, Rasili mali zetu tuibiwe, Biashara ya Unga wafanye, ufisadi wafanye, na kuuwa raia kwa mabomu na utekaji..... Halafu na kwenye uchaguzi waibe kura na kuchakachua--- AAAGRRRR ..... MAJANGAAAAA
 
Back
Top Bottom