namwachia house girl nyumba nimechoka


I am proud of you walimu wangu King'asti, wewe, nyamayao, kaunga, nyumba kubwa, AshaDii na JF crew nzima mmeninoa kisawa sawa. Na Bahati nzuri na mwandani naye ni mwalimu tosha yaani Am so proud of you guys.! Nilikuwa wapi muda wote?
 
mbona umeongea na hasira hivyo...beki 3 walishakutendea nini??
mtotowamjini, beki 3 ndio kina nani? Kwangu mie huyo ni mwanamke mwenzangu, mwenye needs kama zangu na haki ya kupenda/pendwa kama mie. Hatuna tofauti kubwa zaidi ya nafasi katika maisha hasa kiuchumi, kuwa mie nimebarikiwa nikamwajiri (of which ingeweza kuwa mie niliyeajiriwa naye).

Tatizo langu si yeye kuwa msichana wa kazi (au Beki 3 ulivyomuita). Nimechukizwa na mtoa mada anayetuletea malalamiko ya mtu ambaye anaHISI/WASIWASI kuwa msichana wake wa kazi anatembea na mumewe. Nilitegemea angekuja na uthibitisho mf. kawafumania n.k. But wasiwasi?? do not work for me kwa kweli.

Aje na ushahidi ndio nitajua jinsi ya kumshauri amfanye nini huyo mumewe anayetembea na MWANAMKE MWINGINE nje ya ndoa yake.
 
Last edited by a moderator:
Unamzidi kwa uzuri, unamzidi kwa usomi, unamzidi kwa akili, unamzidi kwa ku-socialize, unamzidi kwa kila kitu inakuwaje akuzidi 'hapo tu' ? Jifunze na ubadirike mwanamke usiwe jiwe
 
mfukuze house girl.. mrudishe ulipomtoa! mbona unajaribu ku complicate mambo kukimbia weye!
 
he makubwa, mie hata nikifumani simuachi sembuse hisia tu
 
Duh huyo hg (kwetu tulikuwa tunawaita maTX) anaonekana yuko makini sana...mwambie huyo mama achangamke dunia ya ushindani hii.....
 
Mkumbushe huyo alokutuma kuwa Mwanamke Mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Wasiwasi tu umfanye amuachie nyumba mwanamke mwenzie??

Asituchoshe akili hapa akha!

Kama unamwachia hausi gelo kazi zote mpaka kumfulia mmeo boxer kwa nini asilale nae?
 
Na wasiwasi ananiibia mume bora nimuachie kabisa.
Nimepewa ujumbe niwaletee!

Loly kama haujiamini vile! Ujumbe huo una ushahidi wa kutosha? Na pia umeuthibitisha? Au unaishi kwa kusikiliza maneno ya watu na kuyafanyia kazi bila uchunguzi? Kumbuka kuwa wengine huishi na kufurahi kuharibu ndoa za watu ili wao wapate nafasi na wengine hawapendi kuona wenzao wanaishi maisha ya amani na familia zao, ingawaje inawezekana kuna ukweli wa hilo lililosemwa.

Fanya uchunguzi, na ukithibitisha ni kweli timua housegel na mwonye mumeo aache tabia mbaya. Pia jiangalie na wewe mwenyewe ulikosea wapi mpaka mumeo akaamua kujipoza kwa housegel! Tafakari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…