Namwachia nyumba mama mkwe

Esperance

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
364
Reaction score
84
Hamjambo wana jamvi. Mwenzenu namwachia mama mkwe nyumba aishi na mwanae. Ni wiki ya 3 haongei na mimi anapika kwake. Kibaya alichemsha mitishamba ninywe na house girl hakutoa maelezo tukagoma. Anaondoka mchana kurudi usiku. Mume wangu hayupo hadi dec, hali ni tete. Na anamuogopa mamake sana. Hatak kurud kwa mumewe, ndgu wamechoka vikao. Kesha sambaratisha ndoa ya mtoto wake mkubwa anaprefer wanawake wa kabila lake hata wajukuu anawabagua. Nisaidien wandugu na hii hali yangu.

Esperance my dear....sina uzoefu na mambo hayo kivile....lakini nakushauri nenda kapumzike kwa mama yako mpaka mmeo arudi.....khaaa!!....

Ushamweleza mumeo hilo tatizo na mshenga wako.
Ni tatizo kubwa sana ila kabla hujachukua maamuzi yoyote wafikirie watoto wako na huu ni ugomvi wa mama mkwe sio na mumeo
Kama ushamjua kuw ani mvunjaji wa ndoa za watu jaribu ufanye kila njia ulinde ndoa yako maadam wanamuelewa kuwa ni mgomvi na anasambaratisha ndoa
Linda sana ndoa yako na watoto wako na wala usijaribu kuvunja ndoa yako kwa sababu ya mama mkwe. najua ni ngumu sana kuvumilia ila wewe fuata kile ambacho kimekuweka kwa mumeo yaani ndoa yako na maisha ya watoto wako

Mmmh, pole dada. Mumeo anataarifa na yote yanayokutokea? Ongea na mumeo ikiwezekana achukue hatua ya kuongea na baba mkwe arudishwe kwa mumeo. Siyo vema kuikimbia ndoa yako kwa mgeni.

Dada yangu ukiondoka tu anashangilia na utaonekana mbaya mbele za watu na mumeo.

nakumbuka wakati flani uliwahi kuleta malalamiko hpa kuwa huyo mumeo anamsikiliza mama yake kuliko wewe...ukazidi kutiririka kuwa hata mkipanga kitu na mumeo lazima akapate approval toka kwa mama yake........(nisahihishe kama nakosea sio wewe ulileta lalamiko hilo hapa)

kwa kuwa mumeo hayupo kaondoka hadi hiyo dec....na kw kuwa mama mkwe anaendelea na tabia yake basi wasiliana mumeo na umweleze kinachojiri then mwambia kuwa unaenda kwenuhadi hapo atakaporudi mumeo.....

ondoka huyo mama sio mtu mzuri hata kidogo

Hiki sio kilio cha kwanza kusikia kero za mama mkwe. This is too Much. haya ndio madhara ya kuwa mwanaume mtoto wa mama. Full ujinga

Hivi kwanini tunawaachia mama zetu watuharibie ndoa zetu, sisi wanaume inabidi tusimame katika nafasi zetu. maana hata neno la Mungu linasema kijana atamuacha baba na mama ye ataambatana na mkewe nao hawata kuwa wawili tena bali ni mwili mmoja... na vile vile wazazi msiwachokoze watoto wenu......

Wanaume tuwasaidie wake zetu, tutunze ndoa zetu sio kila kitu lazima umuulize mama...

Mshauri wako wa karibu ni mkeo, maana mama ako hawezi fanya kazi za mkeo hata siku moja!!

TUWAPENDE WAKE ZETU KAMA KRISTU ALIVYO LIPENDA KANISA!!

jamani hali yako ndo kama hiyo kwenye avatar? yaani nimekuonea huruma, pole.

mitishamba ya nini sasa hiyo? mlikuwa mnaumwa?
mi nadhani jaribu kuongea na mumeo asaidie kusuluhisha hizo tofauti zenu. hata kama anamuogopa mama yake kwa kweli kuna wakati tu mwanaume inabidi atumie uanaume wake na kuwa jasiri na mwenye busara. anamuogopea nini mamake kama hana kosa? au kukuoa wewe wa kabila lingine na yeye anaona alimkosea mama yake? mi natamani ueleze kidogo msiamo wa mume wako kwenye hili tatizo ambalo hata ndugu wamechoka kusuluhisha ili tupate picha kidogo...

ni kweli Edson nimekuwa nikileta malalamiko hapa na kupata ushauri. Mume wangu anajua kila kitu ila hana maamuz kwa mamake. Baba mkwe keshakuja 2 times kuja kumchukua hataki na anaish dar hapa hapa. Nauli 600tsh. Asante mkuu ntafanya hvyo.

mume wangu anajua kila kitu na mshenga ,wazaz wote wanajua kinachoendelea

Madamu wewe upo kwako, fanya mpango wa kumwambia mama naye arudi kwake kwa kumshirikisha mumeo.
Ikishindikana hapo mwambie mumeo kama unakwenda kwenu mpaka hapo atakaporudi mumeo.
Hilo jambo ni la hatari sana kwa mustakabali wa maisha yenu kwenye ndoa yenu kama huyo mama ana tabia hiyo na anajulikana na jamii inayowazunguka.
Pole sana ndugu Mungu ni mwema wakati wote, wewe mwombe atakusaidia katika janga hilo.

Daah jamani hivi watu wengine wapo kuvunja ndoa za watu?
mama mkwe awanyweshe miti shamba ili iweje.
Jaribu kuwaeleza wazazi wako hili tatizo lazima watakupa ushauri wa hekima na busara

Saa nyingine hata nyie wake zetu mna matatizo bana, hivyo mi sikuamini 100% kwamba mama mkwe ndo mbaya. Jitoe kwanza boriti jichoni mwako.

huyo mama ni mchawi na hafai.......hujaua kwenu dada yangu jiondokeee.nenda nyumbani kwa wazazi wako/ndugu zako ......naamini wanajua yanayoendelea...nenda dada yangu nenda...kapumzike nyumbani hata ikikupasa kutoa sadaka kubwa(kuachana na mumeo) maana yeye amaeamua kumsikiliza mama yake mkorofi....huenda huyo mumeo wakati akiwa mdogo amewahi kufundishwa mambo na huyo mama tena akingali mdogo wa kubebwa mgongoni....haiwezekani akawa nafumbua macho madhira unayofanyiwa......nenda dada yangu ...kapumziike dada yangu akirudi huyo mumeo na akaona umuhimu wako atajifunza.....tena we fanya hiv kwa kuwa umesema huyo mama anaondoka mchana na kurudi usiku...we subiri hayo then badili vitasa nunua solex weka malangoni then jiondokee wewe na H/girl.....hakikisha umefuga nyumba vizuri...magudulia yake muwekee nje hapo....

Esperance my dear....sina uzoefu na mambo hayo kivile....lakini nakushauri nenda kapumzike kwa mama yako mpaka mmeo arudi.....khaaa!!....

Daah jamani hivi watu wengine wapo kuvunja ndoa za watu?
mama mkwe awanyweshe miti shamba ili iweje.
Jaribu kuwaeleza wazazi wako hili tatizo lazima watakupa ushauri wa hekima na busara

na ikitokea hao wakwe ndo 'wazazi' wa Esperance anakimbilia wapi sasa?

tukiachilia mbali hiyo mitishamba na kabila lako, Esperance huna tatizo lingine na mkwe wako? huwezi kuwa pia na wewe unachangia kwenye shida ya hiyo ndoa yako?

Daah jamani hivi watu wengine wapo kuvunja ndoa za watu?

mama mkwe awanyweshe miti shamba ili iweje.

Jaribu kuwaeleza wazazi wako hili tatizo lazima watakupa ushauri wa hekima na busara

FL hiyo mitishamba anadi sijakubaliwa kikwao ni kind of ushirikina. Wazazi wangu/ndgu wameshachoka na vikao, wanataka nirudi nyumbani.

naomba nitofautiane na wengine. Hebu chukulia v2 kama positively,

1. Ni vyema hamkunywa dawa zake,hv wanawake wengine wakoje? Unampa mtoto wa mwenzio mitishamba yako kama ni sumu je?

2. Heri kaamua kujipikia, maana kama anakula na nyie ipo siku ataamua kupika yeye awatilie midawa yake ya ajabu kwenye msosi.

3. Kaamua kununa? Mwache anune hadi avimbe arudi kwa mumewe!

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…