Namwona Abdi Kasimu Babi ndani ya miguu ya Shekhani Ibrahimu

Namwona Abdi Kasimu Babi ndani ya miguu ya Shekhani Ibrahimu

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Abdi Kasim babi ndio ni mmoja wa mafundi wa soka kutokea Zanzibari akibebwa na nguvu/stamina pamoja na ukali wa mashuti yake.

Abdi Kasimu amecheza Yanga kwa mafanikio makubwa na alikua kati ya wachezaji tegemeo wa Yanga kipindi kile, Pia amecheza T/Stars na Zanzibar Heroes kwa kiwango kikubwa ni mchezaji aliyestaafu na mpira wake.

Leo hii kuna kijana mwingine Fundi kabisa kutoka kule kule Zenji wakuitwa Shekhani Ibrahimu aliyesajiliwa na Yanga msimu huu kijana naye anapita mule mule kwa Abdi Kasimu kijana ana uwezo mkubwa wa kupiga ndani ya 18 na nje ya 18 ukitaka kuuliza muulize Kipa wa APR ya Rwanda.

Baada ya Kijana kuingia kipa wa APR alikua ana kazi nzito ya kufanya uokozi wa michomo hatari kutoka kwa Kijana Shekhani na huku moja ikigonga mwamba wa juu.

Miguu ya Kasimu Babi imerudi tena pale Jangwani, sina shaka na wachezaji kutoka Zenji wanajua sana kujitunza na kuwa na mwisho mzuri kwenye Soka.

Pale Jangwani kijana akiongezewa vikitu vichache tu vya kimpira, kujitunza na nidhamu hakika atakua mchezaji wa tegemeo wa Yanga mbali na sifa za Ukasimu ndani yake pale ana Uacho ndani yake sema kamshinda kidogo Dr Aucho kwa mishuti yake ile.

Namwona kijana mbali zaidi .

Roma ikisema imesema.

1704827742475.png

Abdi Kasimu Babi
1704827808525.png

Shekhani Ibrahimu
 
Usitutoneshe vidonda vilivyopoa vya Abdi Kassim Babi Mkuu.

Ila Zanzibar wametuheshimisha sana Yanga, hadi mchezaji wangu bora kwa muda wote pale Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ nae alituachia historia nzuri.
 
Usitutoneshe vidonda vilivyopoa vya Abdi Kassim Babi Mkuu.

Ila Zanzibar wametuheshimisha sana Yanga, hadi mchezaji wangu bora kwa muda wote pale Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ nae alituachia historia nzuri.
Tukumbuke pia ndio mchezaji wa kwanza kufunga goli Uwanja wa mkapa zamani Taifa boonge moja la Shuti na kumwacha golikipa wa Uganda akiruka bila faida pasi tamu kutoka kwa Haruna Moshi Boban
 
Ana hitaji muda kdg ...dogo mwingine pale yanga ni yule Chigombo akipewq nafasi mtaanza kumuandika sana tu
 
Back
Top Bottom