Kama ni nanasi hili hili tunalolijua linapandwa hivi;
Nanasi likisha toa tunda lake halifi,bali huto machipukizi (suckers),haya machipukizi hayatokei chini kama mgomba ufanyavyo bali yanatokea kama matawi kutoka ktk nanasi mama.Lile chipukizi huanza kutoa mizizi hata kabla halijaondolewa toka nanasi mama,lakini mizizi hiyo imefichwa na maganda.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kunyofoa chipukizi toka nanasi mama na kuondoa maganda yanayozuia mizizi isionekane, kisha unapanda ktk udongo kama tunavyopanda miche mingine.
Nisamehe bure kama nimetoa maelezo yasiyotosheleza swali lako.