Pre GE2025 Nanauka Foundation yakabidhi kadi za bima ya afya kwa wazee 204, Mtwara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Taasisi ya Joel Nanauka Foundation, chini ya Muasisi wake Dkt. Joel Arthur Nanauka, imeendesha zoezi la ugawaji wa kadi za Bima ya Afya kwa Wazee 204 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Screenshot 2025-03-02 203830.png

Zoezi hilo limefanyika katika Kata ya Chuno, Mtaa wa Ligula B, likihudhuriwa na Wazee kutoka maeneo mbalimbali pamoja na Viongozi wa Serikali.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara, Gwakisa, amepongeza juhudi za Nanauka Foundation kwa kutambua na kuthamini mchango wa wazee kwa kuwapatia kadi za Bima ya Afya. Pia, amewataka watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha wazee wanapata huduma bila vikwazo vyovyote.
Screenshot 2025-03-02 203845.png

Kwa upande wake, Dkt. Joel Nanauka amesema kuwa Nanauka Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi yenye uhitaji kwa lengo la kuboresha maisha yao, huku akisisitiza kuwa huo ndio utamaduni wa taasisi hiyo katika kuwahudumia Wananchi.
Screenshot 2025-03-02 203900.png

Baadhi ya Wazee waliopokea kadi hizo wametoa shukrani zao kwa taasisi ya Nanauka Foundation, wakisema kuwa hatua hiyo itawasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi na bila changamoto kubwa za kifedha “Mimi nimekuwa nikihangaika kupata matibabu kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za hospitali, lakini sasa kupitia kadi hii, nina uhakika wa kupata matibabu bila shida,"

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Ngo hi
Angalieni msifanye wema machoni pa watu ili mpate kutazamwa.
Hakuna haja ya kujitangaza.
oo mkuu zile video na picha unahisi wanapoelekea majunban kuweka ukumbisho??
 
Taasisi ya Joel Nanauka Foundation, chini ya Muasisi wake Dkt. Joel Arthur Nanauka, imeendesha zoezi la ugawaji wa kadi za Bima ya Afya kwa Wazee 204 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
View attachment 3256212
Zoezi hilo limefanyika katika Kata ya Chuno, Mtaa wa Ligula B, likihudhuriwa na Wazee kutoka maeneo mbalimbali pamoja na Viongozi wa Serikali.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara, Gwakisa, amepongeza juhudi za Nanauka Foundation kwa kutambua na kuthamini mchango wa wazee kwa kuwapatia kadi za Bima ya Afya. Pia, amewataka watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha wazee wanapata huduma bila vikwazo vyovyote.
View attachment 3256214
Kwa upande wake, Dkt. Joel Nanauka amesema kuwa Nanauka Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia makundi yenye uhitaji kwa lengo la kuboresha maisha yao, huku akisisitiza kuwa huo ndio utamaduni wa taasisi hiyo katika kuwahudumia Wananchi.
View attachment 3256217

Baadhi ya Wazee waliopokea kadi hizo wametoa shukrani zao kwa taasisi ya Nanauka Foundation, wakisema kuwa hatua hiyo itawasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi na bila changamoto kubwa za kifedha “Mimi nimekuwa nikihangaika kupata matibabu kutokana na kukosa uwezo wa kulipia gharama za hospitali, lakini sasa kupitia kadi hii, nina uhakika wa kupata matibabu bila shida,"
HATA nhif Wana toa kadi za wazee

Shida zinaishia kunnuaa Panadol na aspirin

Wale wazee WANAHITAJI dawa za kueleweka wapone anyway mi SIWEZI kumjaribu Mungu hivi
 
Mwamba aliwahi tangaza nia pengine anaandaa njia atarudi kivngine..any way hongera yake
 
Namkubali sana anauwezo naamini akipata atafanya kwa ukubwa ....
Mungu amfanikishe namuombea
 
Back
Top Bottom