Nancy Pelosi awasili nchini Armenia na kuilaumu Azerbaijan kwa mapigano ya mipakani

Nancy Pelosi awasili nchini Armenia na kuilaumu Azerbaijan kwa mapigano ya mipakani

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
Speaker wa Bunge la wawakilishi nchini Marekani,Nancy Pelosi amewasili katika mji Mkuu wa Armenia,Yerevan. Ziara hiyo inakuja baada ya Mapigano makali ya Kijeshi Kati ya Armenia na Azerbaijan yaliyosababisha Vifo vya Wanajeshi zaidi ya 250 kutoka pande zote Mbili. Mapigano hayo yalitokea katika eneo la Mpakani la NARGRO-KARABAHKH ambalo ndilo linalozozaniwa na pende zote Mbili.

Armenia Ni Mwanachama wa Jumuia ya Kiusalama inayoongozwa na Urusi ya Collective Security Treaty Organization (CSTO). Waziri Mkuu wa Armenia Pashnyan ameituhumu Urusi kwa Kushindwa kuisaidia nchi Yake licha ya Kuwa mwanachama wa CSTO badala Yake ameomba msaada wa Kijeshi kutoka Marekani.

Akiongea na Waandishi wa habari mjini Yerevan, Waziri Mkuu wa Armenia amesema kwamba Urusi sio mshirika imara wa Kiusalama kwa Sasa na hivyo Armenia itatafuta Washirika Wengine imara wa Kiusalama ikiwemo Marekani. Pashnyan amesema kwamba,Wakati Marekani ikilinda Usalama wa Kila nchi mwanachama wa NATO tangu mwaka 1949,Urusi imeshindwa kuilinda Armenia kutoka kwenye mashambulizi ya Azerbaijan. Azerbaijan sio mwanachama wa CSTO lakini ni mshirika wa Kiusalama wa Nchi ya Uturuki.

Akiongea na Waandishi wa Habari,Nancy Pelosi ameahidi kwamba Marekani itaangalia namna ya kuimarisha Usalama wa Armenia na Kuituhumu Urusi kwa Kudhorotesha Usalama wa Washirika wake.

Wakati huo huo,Mapigano mapya Kati ya Tajkstan na Kyrgystan yameripotiwa na zaidi ya Wanajeshi 100 kutoka pande zote Mbili wamekufa. Tajkstan na Kyrgystan Ni wanachama wa CSTO. Wachambuzi wanadai kwamba,Udhaifu unaooneshwa na Jeshi la Urusi Nchini Ukraine umeyafanya Mataifa wanachama wa Muungano wa CSTO unaoongozwa na Urusi haufai kwani Urusi iliyoonekana Mlinzi wa Mataifa hayo imeonekana Haina uwezo huo.

Azerbaijan slams Pelosi, saying the ‘unsubstantiated and unfair accusations’ are a serious blow to peace efforts. Pelosi slams Azerbaijan’s ‘illegal’ attacks during Armenia visit
 
Ndio lazima mshindi apatikane tuanze upya na balanced and controlled supremacy.
 
20220919_000240.jpg
 
Armenians ni allies wa Russia na ameshaomba security guarantee toka Russia kuhusu huu mgogoro.

Vilevile Armenians Ni allies wa US.

Sasa unasoma response za watu na kuangalia comments zao, unajifunza wa Tanzania wana akili ndogo Sana.
 
Mshirika wa ukweli wa urusi ni beralusi tu hao wengine wanataka kulindwa lakini Russians wakiwa na operation wanaogopa hata kupeleka askari.
 
Back
Top Bottom