Nando atangaza kuacha kutumia dawa za kulevya

ridculouz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
910
Reaction score
499


Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase', Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa za kulevya. Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times Fm.

Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha. Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.

"Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pee pressure na watu niokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi...ni yale maisha ya kujiachia." Amesema Nando.

Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi. "kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au mbili kwa siku."

Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali cha kuvuta bangi katika jimbo la California kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.
 

Attachments

  • nando.JPG
    35.8 KB · Views: 1,622
Hawa vijana sijui wana matatizo gani...lkn wakati mwingine ni ushamba na ulimbukeni..

Mshamba n ww wa kuja, acha kila mtu aishi maisha aliyoyataman kuyaishi


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
pia bangi inasaidia kuacha sigara...wavuta fegi wengi wanaotaka kuacha wanashindwa kujizuia kuvuta hasa ikifika usiku...yani usingizi hauji kabisa...cha kufanya ikifika usiku we nyonga bangi ndefuuu (king size) halafu vuta...hapo lazima ulale...
 
Ndo maana huwa sipendi marafiki wengi.
 
Hivi mshaona sifaa kujitangaza mmeacha madawa?Kwani ukiacha kimyakimya kama ulivyoanza kimyakimya utapungukiwa nini?Ningekuwa na mamlaka ningewakamata wote mnaojitangaza ili mnisaidie kuwakamata wanaowauzia
 
Ulimwengu umejaa wajinga wajinga huu. Sasa huyu ndo nani huyu? Si kituko tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…