Mwl Philemon
Member
- Nov 29, 2018
- 63
- 70
Kumekuwa na ongezeko la matamko na vitisho kwa walimu katika nyanja hii ya elimu.
Lakini je tatizo ni mwalimu ndio maana elimu inashuka?
Nafikiri jibu ni hapana.
Kuna mambo mengi yasiyo tajwa juu ya tatizo hili.
Kwa ukweli na uwazi haya ni baadhi ya mambo yanayopelekea kushuka kwa elimu katika nchi yetu :
1. Upungufu wa walimu na mgawanyo mbovu
Hapa iko wazi na haina ubishi walimu bado ni wachache na hata waliopo utawakuta wamerundikana katika shule chache zenye mazingira mazuri huku shule nyingi zenye mazingira magumu zikiwa na walimu wachache. Unakuta shule yenye vyumba nane vya madarasa ina walimu wa nne.
2. Motisha ndogo
Zaidi ya matamko na vitisho walimu hawahamasishwi vizuri kuifanya kazi kwa moyo. Hatutafanikiwa kwa kuwaambia hamtapanda madaraka au tutawafukuza kazi. Tunajenga usugu ndani ya utumishi na kuwafanya watumishi kujiandaa kuishi nje ya mfumo.
Namna tunaweza kuchochea uwajibikaji
-kutengeneza ratiba rafiki kwa watumishi mfano iishie saa 8:30 nchi nzima.
-kupunguziwa idadi ya masomo/vipindi mfano kusiwe na mwl mwenye masomo zaidi ya 3 au vipindi 16 kwa wiki hii tofauti na sasa ambapo kuna walimu wana vipindi mpaka vinagoma kuweka kwenye ratiba.
-kuwe na posho katika ya mwezi walau 50000 hii itapunguza ugumu wa maisha nakuongeza uwajibikaji.
-walimu wapongezwe kwa kuzingatia vigezo na maeneo yao mfano mjini na vijijini hakufanani hivyo huwezi ringanisha au kuwapambanisha kwa vipimo sawa.
3. Mfumo wa elimu
Nionavyo mimi mfumo umeendelea kuleta udhaifu katika elimu.
Kuna utofauti kwa kila ngazi ambao hauleti msingi wa muendelezo katika elimu
Mfano Kiswahili msingi na English sekondari
Kuchagua msingi na kujieleza sekondari na
mabadiliko ya mitaala kutokana na matakwa ya mawaziri badala ya mahitaji ya Taifa haya ni matatizo yasiyotupiwa macho.
Yako mengi ila hatuna shabaha na tunachokilenga elimu yetu bado ni tatizo na sio mwalimu awe tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app