SoC02 Nani alaumiwe? Nuru au Sinza Afrika-Sana?

SoC02 Nani alaumiwe? Nuru au Sinza Afrika-Sana?

Stories of Change - 2022 Competition

Kacha_Boy

New Member
Joined
Aug 8, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Ni usiku wa manaani japo watu wengi wanapenda kuita usiku wa manane, wahuni wamelegeza kwa kuita night kali, ndani ya jiji la Amos makala heka heka zikiwa zinaendelea, huku baridi iliyoambatana na manyunyu ya mvua kwa mbali zikiwa zimefunika jiji la Dar es salaam. Nchi ilikuwa imemezwa na giza zito pamoja na ukimya wa kutisha, nikiwa natoka kwenye mishe mishe zangu nikikatiza mitaa ya Sinza Afrika-sana, nikiwa katika dimbwi la mawazo nikiiwaze siku ya kesho itakuwaje, nipo hai kimwili lakini mfu kifikra

Moyo wangu ulipigwa na butwaa pale nilipokutana na binti ambaye inaonekana kumfahamu. Macho yangu yaligoma kuamini kile ninachokiona niliamini kuwa macho yangu yamenisaliti kutokana na uchovu wa ubongo wangu kufanya kazi masaa mengi. Nilijitahidi kumsogelea binti yule lakini giza zito lilitazamana na macho yangu nilishindwa kumfahamu yule binti, ghafla yule binti aliniita kwa jina langu, sauti yake niliifahamu kiurahisi kumbe alikuwa ni "Nuru" binti mrembo, hakuna mwanaume ambaye asingethubutu kurudisha shingo yake na kumtazama kwa mara ya pili pale munapopishana. Alikuwa mnene kiasi, mweupe kama malaika, alikuwa ana sura nzuri iliyosadifu jina lake ' Nuru' ni ndoto ya kila mwanaume kummiliki binti kama Nuru, bacteria wa huzuni waliendelea kuutafuna moyo wangu pale nilipondua kuwa Nuru alikuwa katika mitaa ile ya Sinza Afrikasana lakini alikuwa anajiuza ' Dada poa'

Nguo alizovaa zilisadifu mazingira aliyokuwa kwa wakati ule, Nuru kadri alivyonisogelea alizidi kudondosha machozi ya majuto. Nikagundua wanawake wengi katika jamii yetu wanafanya mambo kwa majuto lakini majuto yote yanatokana na mitaa jinsi inavyotulea. Mitaa mingi sasaivi imekuwa mitaa ambayo sio rafiki katika ukuwaji wa watoto zetu, Nani alaumiwe?

NANI WAKULAUMIWA?
Wazazi/walezi, moja ya sababu ya wanawake wengi kuingia katika tabia tofauti tofauti ambazo sio rafiki kwa jamii ni kwa sababu ya ukosefu wa malezi bora kutoka kwa walezi au wazazi wetu, malezi bora hupelekea ukuwaji nzuri wa tabia njema kwa watoto wetu hivyo wazazi na walezi wa watoto ndio watu wa kwanza wa kulaumiwa kama mtoto wa kike ataingia katika makundi mabaya katika jamii, jambo moja kubwa la kuzingatia ili mtoto akuwe katika maadili mema ni mzazi au mlezi kuhakikisha mtoto anakuwa katika maadili ambayo yanampendeza Mungu.

Kundi rika/ katika ukuwaje wa mtoto anapitia katika makundi mbali mbali ambayo yatamwezesha kuiga tabia mbali mbali kutoka katika makundi hayo hivyo basi wazazi au walezi wanapaswa kuzingatia makundi ambayo mtoto anakuwa nayo, kama mzazi atashindwa kuzingatia makundi ambayo mtoto anacheza nayo itapelekea mtoto kuiga tabia ambazo sio rafiki katika jamii mfano uvutaji wa sigara, matumizi ya bangi, udada poa, matumizi ya madawa ya kulevya, na tabia nyingine ambazo sio rafiki. Hivyo mzazi/mlezi ni muhusika mkuu katika kuzingatia ukuwaji wa mtoto ili mtoto asiingie katika makundi rika ya hovyo.

Jamii/ katika ukuwaje wa mtoto mazingira ambayo yanamzungika ni jamii kwa ujumla, hivyo tabia ya mtoto urithi kutoka kwa jamii. Hivyo basi ni muhimu jamii inayomzungika mtoto katika ukuwaji kuzingatia maadili yaliyo mema ili kusaidia kuchochea kwa ukuwaji bora wa watoto zetu

NINI KIFANYIKE?
Jamii inapaswa kubadilika ili kuleta malezi bora ya watoto wetu, uwepo wa sayansi na technolojia imerahisisha njia za kuwasilisha elimu kwa jamii, hivyo elimu ya malezi bora kwa watoto wetu lazima itolewe katika jamii ili kuwezesha ukuwaji wa kizazi bora.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na technolojia elimu hiyo inaweza kusambazwa kutumia vifaa mbali mbali kama vile simu za mkononi( smartphone), Elimu kuhusu ukuwaji wa mtoto ili awe na maadili mema inaweza ikafundishwa katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter na instagram, hivyo basi ili tupate kizazi kijacho bora lazima jamii ibadilike katika malezi ya watoto wetu.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom