Nani aligundua pesa na lini ilianza kutumika?

Nani aligundua pesa na lini ilianza kutumika?

IKIRIRI

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
2,734
Reaction score
3,023
Ukifuatilia dhana ya kidunia utagundua kuna uongo mkubwa sana juu ya matumizi na kuanzishwa kwa pesa...
Nimefuatilia kwa wasomi wanasema pesa imeanza kutumika kuanzia Miaka ya 1870+, Hii ni baada ya mapinduzi ya viwanda.
Na nimeambiwa waingereza ndio taifa la kwanza kuanza kutumia pesa

Lakini napatwa na ukakasi juu ya hizo za kisomi ambazo wengi humu jf mnaziamini baada ya kudanganywa na wazungu...
Hoja yangu ya msingi ni kwamba ukifuatilia mtazamo wa kidini mfano biblia ukifuatilia kitabu cha luka19 utakutana na jina la mtoza ushuru Zakayo kumbuka alikuwa anatoza pesa..ukimsoma zakayo anaelezwa alikuwa tajiri wa Mali na pesa

Pia Qurani inameeleza kiunaga ubaga kuhusu dhambi ya riba surah Al baqarah 2 surah 275 utaona dhambi ya riba...
Hivi vitabu vilianza kabla ya 1870+ swali la msingi kwanini wazungu wanatudanganya?

Middle East ndio walianza kutumia pesa au mmesahau Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande30 vya pesa?
Katika hili lazima tutafakari na kupeana majibu ya maana

Karibu tujadili pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka dunia ni zaidi ya uijuavyo.Historia ya ubinadamu ina mikanganyiko mingi kiasi inachanganya sana vivyo hivyo kwa pesa.Si kipindi cha Yesu tu hata kipindi cha mfalme daudi pesa ilikuwepo japo haikua na nguvu ilizonazo leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta pesa ule raha za dunia. Kujua historia ya pesa hakukusaidii kitu chochote. Unapaswa kujua kwamba money is the medium of exchange, you need to have something A that you can exchange with another something B with the help of the unit called money.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa inatakiwa kufahamu pesa Ni nini ndo tutajua lini ilianza
 
Naomba mwenyezi Mungu anijalie hizo pesa za kutosha ili na mimi niweze kutatua mahitaji yangu yanayohitaji bidhaa hiyo na kuweza kuwasaidia na wengine pia.
Basi sote tuseme In shaa Allah.
 
Labda noti ndo inaweza kuwa ileletwa na huyo mwingireza ila pesa imekuwapo miaka 4500BC na uzur historia haidangany
 
Pesa kimsingi ni kitu ambacho jamii fulani imekubaliana kuwakilisha thamani wakati wa kununua au kuuza bidhaa na huduma au kuhifadhi Mali. Thamani ya pesa haipo katika yenyewe Bali katika fikra za watumiaji wake.


Binadamu wa kwanza hakutumia pesa, na jamii ya kwanza ya wakulima katika Agricultural Revolution hakutumia pesa mwanzoni, bali walitumia barter trade yaani kubadilishana Mali kwa Mali. Lakini baada ya kazi kuimarika na miji kujengeka na watu Kuwa na specialization ubadilishanaji wa bidhaa ulikuwa mgumu kutokana na ugumu wa kuthaminisha bidhaa moja na bidhaa nyingine.


Kutokana na hilo ndipo ilipoanza pesa katika aina mbalimbali kama simbi (shells), Sarafu, ngozi, chumvi, Shanga, noti nk. Simbi zimetumika hapa Afrika Mashariki na pengine duniani kwa zaidi ya miaka 4000.


Pesa ya kwanza inasemekana iliundwa mnamo mwaka 3000 BC, huko Mesopotamia ikiitwa Shekeli ambapo shekeli moja ilikuwa sawa sawa na Gramu 8 za Silver. Na Sarafu ya,kwanza iliundwa Miaka ya 640 BC na Mfalme Alyates huko Lydia Anatolia ndio Sarafu iliyokuwa na chapa ya kiasi cha madini pamoja na mamlaka iliyotoa Sarafu hiyo, kawaida ilikuwa katika madini ya silver na dhahabu.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom