Nani alimshauri Rais Samia kuwapigia simu wachezaji wa Taifa Stars muda mchache kabla kwenda uwanjani?

Cognizant

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2022
Posts
626
Reaction score
1,409
Mkiambiwa mkae mbali na mambo ya kitaalamu na msiwe na viherehere hamsikii tu.

Kisaikolojia alichokifanya jana Rais Samia kuwapigia simu wachezaji wa timu ya Taifa Stars muda mfupi kabla ya kwenda uwanjani hakikutakiwa na alikosea kwani kilichangia kuharibu maelekezo ya kiufundi ya kocha na akilini mwao wakawa wanawaza kumfurahisha Rais badala ya kuufikiria zaidi mchezo husika.

Endeleeni tu kuhusianisha timu ya taifa stars na Chama cha Mapinduzi na Serikali badala ya kuiacha iwe na sura halisi ya watanzania wote ili ipate baraka zao na siyo ichukiwe kama inavyochukiwa sasa na watu wasiopenda unafiki cognizant nikiwa ni miongoni mwao.

Haya mwambieni na tarehe 21 taifa stars ikicheza na Zambia muda mchache kabla hawajaenda uwanjani awapigie tena simu wachezaji wa taifa stars huku akiviita vyombo vya habari vimpige picha akiwa kaketi katika sofa lake akiongea nao sawa?

Kila la kheri Chipolopolo (Zambia) na Leopard (Congo DR) katika mechi zenu zijazo ambazo mtacheza na Taifa Stars (Tanzania) na cognizant nawaombeni mtufunge ili tutoke haraka na turejee ili ligi kuu yetu iweze kuendelea
 
Lisu acha kujihusisha na mambo ya mipira, mara nyingi ukisha kuwa mshabiki wa mpira , one can not reason! Unaelekea huko....
Wewe kweli na weledi wako Tanzania ichukue kombe? Ukiona nyumbani wote ni wajinga, hata huko ugenini ni wajinga! IGA, miswada ya sheria yote ni ujinga, sasa unategemea CCM supported wawe washindi?
 
Angeongea nao siku 2 au 3 kabla ya mchezo, alichofanya kimeathiri "concentration" ya wachezaji kwa kuwaza simu ya rais badala ya maelekezo ya kocha tena mda mchache kabla ya mchezo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Akawaingiza chaka. Alikuwa anajiandalia Utukufu japo moda wamejitahidi sana kufuta nyuzi zinazohusiana na Taifa stars.
 
Uzuri sijaumia kabisa.
 
Alishauriwa na chawa wa mama akina Mwijaku na baba levo
 
ama hakika wewe ni mpuuzi wa hali ya juu
 
**** swala watu hawalitambui na tumefubwa macho na huu utandawazi na mambo ya haki sawa ila mwanamke hafai kuwa kiongozi lolote atakalo jihusisha nalo litakwenda ndivyo sivyo naweza jikawa nakosea kwa mitazamo ya wengine ila tz tulibugi tulipompa huyu maza kiti bora yangezuka mchafuko kuliko kusema nchi ina kiongozi alafu mambo yako hivi......

Ni sawa na mwanamke alieko kwenye siku zake kichuma tembele kesho hulikuti lote limekauka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…