Ni nani alimtuma kiongozi huyu ambaye bungeni anatambulika kama mbunge tu wa jimbo la kitope Zanzibar kuwasemea wazanzibari? Tuanavyojuwa sisi wengine suala la katiba limewekewa utaratibu maalumu kupitia muswaada wa sharia ya awali nani watakuwa wadau muhimu wa suala hili. ufupi wa mambo serikali ni mdau mmoja na taasisi za kiraia,kisheria na makundi maalum kwa upande wa pili. Inashangaza kuona kamati ya BUNGE iliyokuwa na jukumu la kupata maoni ya wananchi(PUBLIC HEARING) haikufanyika Zanzibar kwa sababu za kiuhafidhina za CCM kule Zanzibar(taarifa zilizopo ni kuwa wajumbe 3 wa CCM kutoka Zanzibar na MWENYEKITI WA KAMATI walitumia ghilba kushawishi wengine na kutumia wingi wao kwenye kamati kuharibu mchakato) leo anazuka MBUNGE wa Kitope halafu anasema yeye binafsi kaandika baruwa kuijulisha kamati nakushangaa wanaosema wazanzibari hawakushirikishwa. Huyu kionbgozi vipi? Angalau angesema serikali ilishiriki lakini sio taasisi wadau kwa upande wa Zanzibar, sasa jee kawasemea nani kati ya hawa?1; CCM ndani ya SMZ/GNU? 2. Serikali ya SMZ/GNU? 3.mawazo yake binafsi? au vipi? Ninavyojuwa ni kuwa hana haki yakuzisemea taasisi wadau wa katiba kwa upande wa ZANZIBAR NANI KAMTUMA KIONGOZI HUYU?