Nani alimtuma balozi seif idd ?

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Ni nani alimtuma kiongozi huyu ambaye bungeni anatambulika kama mbunge tu wa jimbo la kitope Zanzibar kuwasemea wazanzibari? Tuanavyojuwa sisi wengine suala la katiba limewekewa utaratibu maalumu kupitia muswaada wa sharia ya awali nani watakuwa wadau muhimu wa suala hili. ufupi wa mambo serikali ni mdau mmoja na taasisi za kiraia,kisheria na makundi maalum kwa upande wa pili. Inashangaza kuona kamati ya BUNGE iliyokuwa na jukumu la kupata maoni ya wananchi(PUBLIC HEARING) haikufanyika Zanzibar kwa sababu za kiuhafidhina za CCM kule Zanzibar(taarifa zilizopo ni kuwa wajumbe 3 wa CCM kutoka Zanzibar na MWENYEKITI WA KAMATI walitumia ghilba kushawishi wengine na kutumia wingi wao kwenye kamati kuharibu mchakato) leo anazuka MBUNGE wa Kitope halafu anasema yeye binafsi kaandika baruwa kuijulisha kamati nakushangaa wanaosema wazanzibari hawakushirikishwa. Huyu kionbgozi vipi? Angalau angesema serikali ilishiriki lakini sio taasisi wadau kwa upande wa Zanzibar, sasa jee kawasemea nani kati ya hawa?1; CCM ndani ya SMZ/GNU? 2. Serikali ya SMZ/GNU? 3.mawazo yake binafsi? au vipi? Ninavyojuwa ni kuwa hana haki yakuzisemea taasisi wadau wa katiba kwa upande wa ZANZIBAR NANI KAMTUMA KIONGOZI HUYU?
 

Hapo ndipo upumbavu unapoanzia. Waliosema Wazanzibari hawakushirikishwa walimaanisha wananchi na asasi za kiraia lakini kwa wengine kumbe Wazanzibari maana yake ni serikali ya Zanzibar. Hapo ndipo mkanganyiko unapokuja kwamba kumbe hata wananchi wasipoulizwa maoni yao lakini serikali ikasema maoni ya wananchi yamechukuliwa basi mambo yatakuwa yameisha.

Wazanzibari ninawatahadharisha: hata kura za kupitisha rasimu ya katiba wasije wakashangaa zikichakachuliwa na mwisho tuambiwe Wazanzibari wanameamua hivi au vile. Mmeporwa haki zenu mara nyingi katika chaguzi zilizopita mkaishia kwenye muafaka na serikali ya umoja wa kitaifa. Subirini katiba ya muafaka na umoja wa Kitaifa. Hivyo ndivyo ilivyo.

CUF baada ya ndoa yao na CCM wakaona kuwa watakuwa salama na hatimaye wakaanza kuwahujumu CDM ila sasa wamegundua kumbe ndoa yao sasa imekuwa chungu. Huko ndani sasa hakukaliki, wameona wajiunge na CDM. CDM wapokeeni CUF na msaidiane katika mambo yale ambayo watawaunga mkono ila msiwaingize jikoni maana hao hawaaminiki kwa sababu ya kutokuwa waaminifu katika ndoa. Si busara kumchukua haraka haraka mwanamke aliyeachika hivi karibuni maana anaweza kukubali muwe pamoja kwa sababu ya kutaka hifadhi ya muda kabla akili haijatulia.
 
Ndugu licha ya kuwa kuna kasoro za hapa na pale Katika GNU ya Zanzibar zaidi kutoka kwa wahafidhina zikiongozwa na Huyu BALOZI Iddi (anajulikana) faida za CUF kuwemo katika serikali hio ni kubwa. huwezi kujuwa kinachoendelea. wewe tazama tu hawa jamaa wanavyohaha na mpaka sasa kwa Zanzibar tunaambiwa serikali haina msimamo wa aina ya serikali watakaoamuwa ni wananchi .Kwa tulivyowazowea hawa jamaa wangalisema wakati serikali inaongozwa na CCM na wakati sera ya CCM ni serikali mbili basi SMZ inaunga mkono serikali mbili lakini leo wapi si wanajuwa hawako peke yao? Nina uhakika hawa jamaa wanapata tabu kufanya yale waliyozowea kwa sababu ya kuwepo CUF tu pale tusibeze. Katika hili la muswaada wa marekebisho wa katiba kinachoshangaza ni kule Balozi kujifanya msemaji wa Wazanzibari kwa hili ilihali akijuwa yeye hata hio serikali basi haiwakilishi bungeni maana ni mbunge tu wa kawaida. Kwa masuala haya ya mchakato wa katiba sharia inamtambuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar na waziri wake kuwa ndio wawakilishi wa serikali ni afadhali hao ndio wangejibu sio yeye. Nafasi yake yeye ni katika baraza la wawakilishi Zanzibar kuitetea serikali. sasa hapo ndipo inaposhangaza na watu wanajuwa ni kutokana na ule UHAFIDHINA wake ndio akawasaliti wazanzibari. hata hivyo najuwa hili suala linatokota hata huko serikalini wewe tulia tu.
 
Hivi Sharia na Sheria ni kitu Kimoja?
 
Kama ndio ungekuwa upo kwenye chumba cha mtihani ndio jibu ambalo ungejibu? na kama ndio hivyo unaweza kufaulu?
Na kama wewe ndiye muandaaji wa huo mtihani halafu majibu ya mtihani huyajui sijui unge sahihisha vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…